Sunday, December 6, 2015

MIUJIZA YA QADARA PART 3

Asalaam Aleiykum

Napenda kukufahamisha hiyo Qadara ndio ilokuweka hapo ulipo,ndiyo ilokupa hicho ulonacho, wewe Mwenyewe huna uwezo wa amri kupata zaidi ya hayo ulonayo mpaka uondoke kwenye njia ya Qadara na kuanza kuhangaika, uchukue uhuru wako na kuanza kufanya jitihada yako kinyume cha Qadara, utafanikiwa kiasi lakini utafika wakati utajuta, utafika wakati utaona kwanini nilihangaika.
Lakini ukisubiri Qadara ikufanyie basi kwa njia za Miujiza utaelekezwa na mara kwa mshangao limekua lile alitakaloMollah wako, Sasa miujiza hii ufanye nini na wewe uipate, au hao waloipata walifanya nini hata wakafanikiwa.
Hilo ndio kazi za Dini zote kukumbusha, kwanini ikawa kukumbusha? sababu una sahau sana. Kwa sababu wewe unaishi ndani ya hiyo Qadir, lakini tatizo lako hukumbuki, kwani ukikumbuka unarejea Nyumbani kama mtoto alopotea, ukikumbuka kila kitu kina (Dis-Appear) Nimesema (Dis-Appear) kwa sababu hiyo ndio taratibu ya Ulimwengu huu, kila kitu kina Athari hizo, mara umelala ume(Dis)mara umeamka ume(Appear) mara umekumbuka mara umesahau, kwa hiyo muujiza ninao uzungumza hapa ni ule ukipata ile hali ya kukumbuka moja kwa moja ndio unakua ume (Master) umepata huo muujiza wa kuona kote kote, kwenye dhahir(Dis) na kwenye Batin (Appear).
Utakapofikia daraja hiyo hakuna chochote kitakacho kukugusa, Maradhi yakija yatakua yanashambulia mwili (Body)lakini wewe huna maumivu, Umasikini umekufika lakini wewe huna huzuni na wala haukugusi, Msiba unatokea lakini haukugusi, Mali imeibiwa wewe haikugusi, mtu kakutukana wewe hujali tena unaona anatukana jina lakini mimi halinigusi, mateso yanakuja wewe hayakugusi, Raha zinakuja wewe hazikushughulishi uko umetulia kwenye Ufalme wa Qadara.
Sasa ufanye nini kuupata muujiza huu wa Qadara?
Utashangaa vipi unapatikana muujiza huu, utashangaa urahisi wake,na pia utastaajabu ugumu wake wa jambo hilo, hakuna jengine ila neno moja unalolisema bila ya mazingatio, huku neno hilo likiwa limebeba muujiza huu mkubwa wa kukupa raha na starehe ya kuishi maisha yako bila ya dhiki, bila ya huzuni, bila ya shida,bila ya lawama.
Hakuna jengine isipokua neno la Shukurani, neno hilo (Alhamdulillah) unatakiwa neno hili litoke moyoni mwako (Deep)kwenye hazina yako ya kusubiri, iwe kila kinachokufika unashukuru, maradhi yakija jua Mollah kanikumbuka, furaha ikija jua pia umekumbukwa,shida zikikuzonga jua Mwenye Qadara anataka iwe hivyo, kumbuka kila kitu kinaletwa na Mollah wako, kama kula yako, kulala kwako, kuamka kwako, kusema kwako, kuhema kwako, jitahidi kujiweka katika hali hiyo kwa miezi sita uwe bila ya kusita unakumbuka jambo hilo la shukurani kwa kila kinacho tokea katika maisha yako, baada ya miezi sita, shida itakuja utaiangalia, maradhi yatakuja utakua unayaangalia yana udhuru mwili wako lakini wewe hayakugusi, Umasikini upo lakini unaungalia haukugusi,kwa sababu shukurani inakutenganisha wewe na Mwili wako, wewe na mambo yako, na unabakia Roho ilo shahidi wa hayo yote, na huo ndio muujiza kama ulivokuja huna dhara yoyote iliyokugusa, na hivyo ndio utakavo ondoka huna chochote kitacho kugusa katika Ulimwengu huu. Hakuna cha kukumbusha isipokua Kumshukru yule alokupa Uhai na uka (surrender) kwake na kuwa Muislam kamili. (Just be thanks full and Surrender) uishi katika muujiza wa Qadara.

No comments:

Post a Comment