Sunday, December 20, 2015

KUTANA NA NAFSI YAKO PART 3

Asalaam Aleiykum

Nadhani kwa maswali hayo manne imetosheleza kwa kiasi fulani majibu niloyatoa, Sasa umefika wakati wa kulihudhuria somo letu la leo ili kama lina manufaa basi likusaidie katika maisha yako.
Kwani utakapo kutana na miujiza hiyo itakubadilisha kuwa mtu wa aina nyengine kabisa utakua (Transform), Lakini kwanza napenda nitoe tahadhari kwa wale watakaoamua kulifanya zoezi au somo hili kwamba mimi sina dhamana kwa lolote litakalotokezea kinyume cha matarajio.
Kwanini nikasema hivyo kwa sababu mambo haya yanataka lazima awepo Muangalizi mjuzi wa funzo hili la kukutana na nafsi yako, lakini kwa kuwa mna kiu ya kujua elimu hizi nimeona kuna haja ya kuituliza kiu hiyo kwa kuyaleta mafunzo haya.
Basi moja kwa moja tunaingia kwenye darsa hii kwa kuchukua aya ndani ya Quran ili iweze kutufungulia somo hili, aya yenyewe inasema hivi(Saffat aya ya 138) وَبِٱلَّيۡلِ‌ۗ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ "Na Usiku je Hamzingatii"
Hapo kuna changa moto (Motisha)ya "Fahamu"au (Sense) au kuzingatia ita upendavyo, Nini Kuzingatia? kuzingatia ni tendo la kwenda (Beyond Mind) ukitumia Akili ina maana unafikiri, na fikira zinakaa kwenye (Memory lane) fikira ni kukumbuka yalopita,katika fikira hakuna jambo jipya(Mambo yote ya zamani) ima utakua una waza yalopita au kupanga yanokuja lakini kwa uwezo wako wa mambo yalopita.
Lakini kuzingatia ni ule wakati ulo nao, na hapa umetajwa usiku,huu usiku una nini?.Usiku ni wenye kuficha siri nyingi, usiku ndio wenye kutisha na mambo yote ya ajabu yamo na yanatokea usiku.
Usiku ni jambo maalum lakini kuujua lazima japo siku moja uishi ndani ya usiku, najua maneno yana kustaajabisha, lakini ndio ilivyo hivi sasa unapita tu kwenye jambo linaloitwa usiku, vipi kuishi kwenye usiku? Ni pale ambapo usiku unakutana na Roho yako(Tukajaalia huo usiku kama guo lenye kuwafunika)sio kukutana na Akili yako kama ilivo sasa, sasa vipi utakutana na huo usiku, utafanya hivi, Nenda Kijijini au Shamba  kakae japo siku tatu huko utakutana na usiku, huko Giza litaifunika Roho yako, Ni jambo la kutisha sana, unaweza kutoka mbio, ee hichi kiza kidogo cha mjini unaanza kuimba na kupiga miluzi, unatizama nyuma mwili wote unatetemeka,mara unakohoa na hapo ndio hakuna kiza cha kweli sasa nini habari yako utakapo kwenda kukutana na kiza cha kweli,sasa kwanini nikakwambia uende shamba, kwa sababu huku mjini huupati usiku, Mataa yalivoshamiri mpaka ndege hawapati usingizi.
Sasa vipi utauzingatia Usiku wacha nikupe maajabu ya usiku halafu utaanza kuzingatia, Nini kuzingatia?kuzinga-Tia ni kuizuia au kuikinga Akili yako au kuisimamisha ikawa haikumbuki chochote au kui(Shut-down) kwa hiyo ukiambiwa zingatia sio ulete fikira zako ila litizame jambo ukiwa huna wazo lolote na ukifanikiwa tu mara utaona majawabu yanakuteremkia bila ya kutarajia, lakini huwezi kufanya hivyo mpaka upate nyenzo ya kukupeleka kwenye hilo zingatio, kwa kuwa leo tumeutaja usiku basi nyenzo ya leo ninayokupa uifanyie kazi ni hii, Nakuomba zingatia kwanini "Wanaadamu asilimia 97 wanazaliwa na kufa usiku" nenda (Deep)Jiulize (Why)jawabu utakalolipata lina faida kubwa na wewe.
Tumepita kwenye aya inotukumbusha kuuzingatia Usiku na maajabu yake, Na Usiku huo huo ndio utatuonesha mengine yalojificha ndani ya usiku, Na mfano wa kwanza ni ule wa nyota, Nyota zipo lakini mchana hatuzioni mpaka uje Usiku kwa hiyo Usiku ni kama Kioo chetu kinacho tuonesha nyota na mambo mengine, Basi na sisi tutautumia usiku huo huo kwa kukutana na kile kisichojulikana.
Vipi Tutafanya hivyo, umetaka ujue elimu za ajabu sasa ni wakati wake soma kwa makini uwe mkakamavu kufanya majaribio haya.
(Quraan aya sura ya Qiyama aya ya 14)
بَلِ ٱلۡإِنسَـٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَةٌ۬ 
Bali Mwanaadamu ni shahidi juu ya Nafsi yake.
Mwanaadamu ana uwezo wa kuona (Nje na Ndani)kuona matendo yake,na vile vile kujiona Mwenyewe. Na hili ndilo somo letu la leo (Kujiona Nafsi yako) ziko njia mbili ya kwanza ni ngumu na unaweza kuifanya wakati wowote kukutana na nafsi yako, mimi nimekuchagulieni hii ya Rahisi ambayo utaifanya usiku.
Ikiwa kweli unataka kukutana na Nafsi yako, kukujiua kile wewe chenye kuishi ndani ya huo Mwili au (Body) yako basi utafanya hivi (Chukua Mishumaa Miwili Na Kioo kikubwa) weka Mbele yako kwenye chumba cha giza nene, washa mishuma halafu tizama moja kwa moja kwenye hicho kioo bila ya (Kupepesa)au kufunga macho,hakikisha macho yako hayafungiki hata mara moja, utafanya zoezi hili kwa muda wa saa moja, baada ya dakika arobaini utatokwa na mchozi (Kama ulopatwa na msiba)mengi yatamiminika kutokana na macho hayajafungwa kwa kipindi kirefu, machozi yakikauka utaanza kuona sura za kutisha na maajabu makubwa makubwa, unaweza kutoka mbio au akili zikakupotea kwa muda lakini usiogope hayo ni mataarisho ya kukutana na nafsi yako, baada ya saa moja kila kitu kitapotea mbele yako mfano wa kipofu, na hapo ndio utakua tayari kukutana na (Unknown)hicho kisichojulikana, mie siwezi kuhadithia nenda ukayaone Mwenyewe, ila tahadhari wakati huo usije ukawa mchafu,au ukawa unataka kufa au unataka jambo baya litokee na hivi na vile chochote kilichokua katika nia yako ujue kitatimizwa, na hiyo ndio hatari niloisema hapo mwanzo. Meomba kujua elimu za ajabu namie nimeitikia ombi lenu. Nafunga Darsa kwa kumuomba Mollah wetu atusamehe dhanmbi zetu, atutie mapenzi ya kumpenda yeye na Binaadamu wenzetu, hususan mayatima na maskini na kwa wale wasojiweza.Tunamuomba Mollah wetu awasamehe walotangulia pamoja na sisi wenye kufatia, atupe mazuri tuwe pamoja na waja wema.Msinisahau kwa dua zenu kama mimi nisivo kukusahauni kwa Dua zitokazo kwa Mollah wangu. Amin


No comments:

Post a Comment