Asalaam Aleiykum
Unataka nikufundishe kitu chenye faida na wewe ambacho unacho lakini hukitumii, hutopenda wewe madhila ya maradhi na shida za machungu zikukimbie?, Basi leo nitakujulisha jambo kama utaweza kulifanya litakuwezesha kuishi maisha yako yote kwa furaha na utulivu.
Binaadamu tuko kwenye mateso makubwa kutokana na tabia zetu za kuto kuikubali(Qadir)au kuto kuifahamu hukumu au sifa hii ya Mwenye enzi Mungu, Kila Mmoja wetu yumo katika kuteseka na kubishana na uwezo huu wa (Qadir), matatizo yote yanatokea kwa kukisahau kitu fulani chenye kuishi ndani ya nafsi yako. Na kutokana na sababu hiyo ndio tutaendelea kuteseka mpaka tunaondoka hapa Ulimwenguni.
Sasa ni kitu gani hicho?, Kukijua kitu hicho lazima upite kwenye mfumo wa fahamu, na jambo la mwanzo katika mfumo wa Fahamu lazima ujijue udhaifu wako kuwa wewe umeumbwa na yupo Muumbaji, Na kwa ajili hiyo uamini kwa dhati kuwa kila jambo lako limemilikiwa na huyo alokuumba, na hili lisiwe jambo la kipuuzi kwako, ni lazima lende ndani ya moyo wako na ukumbuke kila wakati.
Jambo la pili uelewe fika kila jambo lenye kutokezea katika maisha yako yeye ndie mpangaji na wewe Kiumbe huna maamuzi katika hilo, Hiyo ndio (Qadir) ambayo ukiikubali basi wewe Muislam kamili, sasa nini kinatokea mpaka jahazi ikenda Mrama?.
Kinachotokezea hapo unaicha njia hiyo ya (Qadara) ya Mwenye enzi Mungu na kujitenga nayo mbali kabisa, Na ukijitenga tu jambo la mwanzo lenye kutokea ni kukumbwa na Sahau, kwani wewe hujaisoma aya ya Mwenye enzi Mungu inosema.(Quran sura ya Talaq aya ya 12)
ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَ سَبۡعَ سَمَـٰوَٲتٍ۬ وَمِنَ ٱلۡأَرۡضِ مِثۡلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ ٱلۡأَمۡرُ بَيۡنَہُنَّ لِتَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىۡءٍ۬ قَدِيرٌ۬ وَأَنَّ ٱللَّهَ قَدۡ أَحَاطَ بِكُلِّ شَىۡءٍ عِلۡمَۢا
Mwenye Enzi Mungu ni yule ambaye ameziumba Mbingu saba na ardhi kuwa mfano wa hizo, Amri (Zake)zinashuka baina yao, ili mjue kwamba Mwenye enzi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu(Qadir), Na kwamba Mwenye enzi Mungu amekizunguka kila kitu kukijua(Kwa elimu yake).
Yanatosha maneno yaliyomo kwenye aya hii kuwa ukumbusho juu yetu lakini bado tumo kwenye lepe lepe la usingizi ndio maana tunafanya kazi hii ya kuamshana.
endelea part 2
No comments:
Post a Comment