Sunday, December 6, 2015

MIUJIZA YA QADARA PART 2

Asalaam Aleiykum

Mwenye enzi Mungu ndio Mwenye uwezo wa kila jambo yeye ndio Mwenye kupanga kila kitu na huku kakupa uhuru wa kuamua akijua marejeo yako yatakua ni kwake, Ikiwa utafata mipango ya Mwenye enzi Mungu hutopata tabu, wala hutoteseka, shida zitakuondokea ,kinacho kutesa hivi sasa ni hiyo sahau yako inochukua 95% ya Uhai wako, basi wacha nikutoe kidogo katika ufalme wa sahau nikukumbushe mambo ambayo pengine yanaweza kuamsha kitu ukaweza kujua vipi wewe umemilikiwa na huo uwezo wa (Qadara).
Jitizame wewe kuanzia Usingizi wako, vipi unaupata mbona huna mamlaka nao ukija lazima ulale, nini habari yako wewe mbona ikikushika njaa unapaparika kutafuta chakula nani alo miliki tumbo lako,jee na nini habari ya kuamka kwako nani mwenye kukuamsha ukaishi tena, Nani huyu anokupa uwezo huo wa kusema, Nani Mwenye kukuletea hicho chakula ukawa unaweza kula ukapata maisha yako ya afya njema, basi ukiyajua hayo machache yakakuingia ndani ya moyo wako utajua maana ya hiyo aya kuwa Mwenye enzi Mungu amekizunguka kila kitu kwa elimu yake, Na pia anajua kila kinachoendelea kwa mmoja wetu pamoja na matokeo yake.
Yeye ndie Mwenye kumpa huyu kidogo yule akampa kingi, Yeye ndie Mwenye kumpa Maradhi fulani na fulani akaendelea na afya yake(Kwa sababu mpaka huo mwili wako yeye ndie mwenye kuuhifadhi)Yeye ndie Mwenye kumpa huyu watoto yule akamfanya tasa, yote hayo kwa uwezo wa Qadara yake.
Sasa najua bado unajiuliza haya yote yenye kukufika yanatokea vipi?, Cha kwanza kabisa kinachotokea ni wewe kuondoka karibu na Mollah wako, Unapokua mdogo unakuwa karibu na Mollah wako bila wewe kujijua, ukifikia Umri fulani unaanza kukimbia kutoka kwa Mollah wako, kama vile unavoanza kutowasikiliza wazazi wako, mpaka huyoo unaenda arijojo(unapotea), na unapofikia umri wa utu uzima unaanza kurejea taratibu kuwa karibu na Mollah wako, unatafuta mambo ya dini yakoje, unakua mkali lazima watu wakusikilize, kumbe masikini unajuta makosa yako.
Kwa hiyo wakati umekimbia inakujia dhana kila ulichofanya au kukipata ni kwa ajili ya juhudi zako ndio maana ukafanikiwa, Sasa unataka nikujulishe nini juhudi zako zinakupa?, hakuna ila madhila, mateso, maradhi na haramu tupu. Kwanini ikawa hivyo?, kwa sababu Juhudi zinatawaliwa na ujanja, ulaghai, dhuluma, juhudi inatawaliwa  na harakati. Lakini (Qadir)inatawaliwa na subira, kwenye (Qadara)hakuna harakati, kila kitu kinakwenda kama kilivo pangwa,(Mfano niloutaja mwanzoni)Kula kwako,usingizi wako,Kuamka kwako, Utajiri wako, Afya yako,Maradhi yako wewe huna (Control)yoyote isipokua alitakalo Mollah wako, ndio maana ukaambiwa (haukufiki Msiba wowote usipokua kabla ya hapo umeandikwa).
Kwanini ikawa msiba kwa sababu (Nature)yako ni ya Raha na Furaha, ila ukitoka katika vigezo hivyo ndio misiba inakukumba kwa kuisababisha wewe mwenyewe kwa juhudi zako, Kwa mikono yako mwenyewe una (Create Action)unapata(Reaction)na hiyo ndio maana ya kuandikwa.
Ukiishi kwenye (Qadara)ndio utajua ama kweli Mwenye enzi Mungu ndie Mwenye uweza, anampa Umri mrefu amtakaye na kumpa Umri mfupi amtakaye, anamnyanyua amtakaye na kumshusha amtakaye, anamruzuku kingi amtakaye na kidogo amtakaye bila ya hesabu.
Hiyo ndio Qadara ambayo nakujulisha ili upate japo kwa uchache kujua nani Mwenye kuyapanga haya yote, nisije nikasema (Qadara)ukafahamu kumbe kila kitu kishapangwa, ukaacha kazi yako ya kufagia, usiwe umechoka kuuza duka au kufanya Biashara ukasema nimeambiwa Mambo yote yanapangwa Mbinguni, Usije ukaacha kazi yako ya uvuvi ukasingizia unaisubiri Qadara, utakua unafanya makosa makubwa, Kwani Qadara inakutaka ufanye nini?.
Endelea part 3

No comments:

Post a Comment