Asalaam Aleiykum
(2)Swali la pili, Hivi kweli Sheikh unafuga Majini?. Napenda kufahamisha kuwa Majini siwanyama kwa hiyo huwezi kuwafuga, ila wanaweza kuwa marafiki zako kama walivo marafiki zangu mimi.
(3)Swali la tatu, Hivyo inawezekana kuwaona Malaika?. Inawezekana lakini kwanza mpaka uisome darsa ya leo, ukiweza kuifahamu na kufanikiwa kutekeleza hayo mafunzo basi utakua na nafasi ya karibu kuwaona, lakini mpaka ukione hicho ntakacho fundisha leo pengine utapata uwezekano wa kuona na hayo mengine, kwanini nikasema hivyo kwa sababu Malaika wameumbwa kwa Nuru, Sasa swali la kujiuliza jee unaijua Nuru?,ushapata kuiona Nuru, ukiweza kuiona Nuru itakua rahisi pia kuwaona Malaika. Lakini kwa hivi sasa kuona kwako unategemea Akili, Yapo Mafunzo ambayo ukiyapata unaweza kuona viumbe wengine wa ajabu.
(4)Swali la Nne, Sheikh tumeona unajibu baadhi ya maswali ya ndoto, Jee unatumia kigezo gani kujibu maswali hayo?.
Naam kweli najaribu kujibu maswali ya ndoto au kutafsiri ndoto hizo, Nini Ndoto? Ndoto ni ujumbe unaokuja kwa lugha usiyofahamu, napenda ukumbuke kwenye ufalme wa Mwenye enzi Mungu hakuna lugha maalum inayotumika kuwasiliana na wewe isipokua kwa njia ya Alama au (Picha). Basi utakapo pata baraka za kuzijua Alama hizo na kusudio lake, hapo ndio tayari utaweza kuzitafsiri ndoto na alama zengine. Na kuthibitisha hayo kihudhurie kisa cha Nabii Yusuf a.s (Sura ya Yusuf aya ya 4)
إِذۡ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَـٰٓأَبَتِ إِنِّى رَأَيۡتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوۡكَبً۬ا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ رَأَيۡتُہُمۡ لِى سَـٰجِدِينَ
(Kumbusha)Yusuf alipomwambia Baba yake, Ewe Babaangu hakika nimeona (Katika ndoto)Nyota kumi na moja na Mwezi, Nimeviona (vyote hivi) Vikinisujudia.
Hapa maneno haya kayasema wakati yuko mdogo alipofikia umri wa (Baleghe)ndio akapewa hiyo elimu ya kutafsiri hizo ndoto kama isemavyo aya ya 22. Na zaidi utayapata katika kisa hichi kuanzia aya ya 46 ya sura hii ya (Yusuf).
Kwa leo namalizia hayo maswali manne na sasa tunaanza darsa yetu tulokusudia.
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment