Asalaam Aleiykum
Nakuletea Mafunzo haya kusudio langu ni kukutaka uende (deep), kukupa uchu wakutaka kujijua wewe nani na ukweli wa mambo ukoje, Upate kuelewa upande wa pili kuna nini?, ni changa moto ya kukupa au kukuwezesha ufanye uchunguzi wa kibinafsi katika jambo hili la kukutana na nafsi yako.
Kwanini leo ikawa nimeleta fundisho hili (Kinaga Ubaga)unajua nini maana ya kinaga ubaga?, Maana yake ni jambo kuwekwa wazi, Nimefanya hivi kwa sababu kuna baadhi ya Watu wamediriki kusema (Sheikh) katika mafundisho yake anataja mambo mengi ya elimu za ajabu,elimu za Mashetani na mengi mengineyo, lakini hakuna hata siku moja tulopata fundisho kamili la elimu hizo za ajabu. Sisi tutakavyo japo siku moja tunataka kutuliza kiu chetu cha kujua kwamba hayo utuambiayo ni kweli unayafahamu.
Naam leo ni siku yangu ya kutekeleza matakwa yenu, lakini cha kunihuzunisha kuwa mnataka kunijua mimi kwamba niyasemayo ni kweli, ni dhumuni la kutaka kunipima kama kweli najua, sio kwa faida yenu ya kutaka kuzijua elimu hizo, na hilo halitosaidia chochote nafsi zenu, na kwa kufanya hivyo siku zote mtabaki kusema fulani anajua na sio mimi najua.
Kumbuka chenye faida na wewe na kukusaidia ni kile ulichojua Mwenyewe kwa kwenda (Deep), Sasa kabla ya kugusa fundisho letu la leo wacha niyajibu maswali yenu ya ajabu ili kila mtu aridhike ipasavyo na majawabu nitakayo yatoa.
(1)Swali la kwanza?Jee wewe Sheikh unafanya Utabiri?.
Jawabu:Utabiri upo wa aina tatu, kuna ule wa aina ya kwanza wa (Mzungu kalala wapi)huu ni wa kubahatisha, Na kuna ule wa pili wa Kupewa na Mollah wako wa kuyaona mambo yalokwisha katiwa amri kutokea, huo unapata kwa njia ya (Ilham), Na njia ya tatu ni ile ya kuwatumia wale wenye kwenda kusikiliza habari wakapata ya kupata na kuja kukuhadithia na hao ni (Majini) kama walivotajwa kuwa wanakwenda Mbingu ya kwanza kusikiliza amri zilizotolewa na kuchukua siri hizo kuzileta ardhini kabla hazijatekelezwa, ndio maana wanapigwa kwa vijinga vya moto, Ama kuhusu mimi kutabiri sifanyi jambo hilo, hata kama najua habari hizo basi ni kwa faida yangu mwenyewe.
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment