Asalaam Aleiykum
Baada ya hizo sekunde nne ndio maridhiano au ugonvi vinaanza kutokea, Na kama umeridhia macho yanaanza mazungumzo (Bubu)ya ishara, unaweza kuandika (Love Story)nzima ya mapenzi, inaweza kutoka Amri ya mtu auliwe kwa ajili ya macho, Ikapelekwa posa pahala kwa ajili ya jicho, Akaumwa mtu maradhi ya kutoka na roho kwa ajili ya jicho, ikaingia pahala hasada kwa ajili ya jicho, Kwanini ikawa jicho?.
Kwa sababu jicho ni (Dirisha la Roho) Na Roho ni (Very Powerful Being)ndio maana ukimuona mwanamme au mwanamke ndani unachemka(Energy)inaanza kunyanyuka, na ikinyanyuka inachukua muda kutulia na Akili kuvurugika, Na kutokana na hilo jicho hapo tena (Mind) inakamata kazi yake, na (Body)inajiweka tayari kwa kutayarisha silaha za mapambano, Hapo tena Akili ya (Mja)ikichafuka Mtu anaweza kufukuzwa kazi au kupandishwa cheo, hiyo ndio Athari ya Jicho na madhara yake, ndio maana unaambiwa liangushe likustiri, kwani kwenye kuliangusha Jicho kuna siri kubwa ndio maana aya ikamalizia na (Wahifadhi Tupu zao) Kwanini Uhifadhi tupu?.
Kwa sababu kwa kufanya hivyo unahifadhi kitu adhimu kabisa ndani ya huo Mwili wako(Body), "Wewe una Mali ghafi" kama utaitunza ndio unaupata huo utakaso (Pureness)Na kama utatumia hiyo mali ghafi yako ovyo ovyo basi utaangamia kwa kuzorota kwa afya yako, utakua huwezi kazi, zitakuvaa tafran tupu kichwani, kwa hiyo unaambiwa hifadhi hicho ulichonacho usipite ukakitupa ovyo kwa furaha ya sekunde nne, uonee huruma mwili wako kwa kuupunguzia kazi za (Overtime)kutengeneza mali ghafi(Material)kila baada ya masaa 24, Halafu tena unaambiwa jiepushe na mazungumzo, kwa sababu mazungumzo au (Sauti) ndio daraja la majaribio, hapo ndipo vinapoanza vimbunga vyote, Fitna zote zinaanzia hapo, Ndio maana utaona wanaadamu tumepewa jambo hili muhimu sana la kuzungumza, Mazungumzo ni mawasiliano, hapo ndipo unapoonesha chuki na mapenzi, kwa kutumia mazungumzo ndio unaonesha hamaki na hasira, kwa hiyo ndio maana ukaambiwa jiepushe hata na mazungumzo sio macho pekee na huyo mwanamke au mwanamme, ila ukiwa ushafikia daraja la kuweza kujimiliki(Control), vipi kujimiliki huko ni pale ukiijua maana ya "(Maneno matamu humtoa nyoka pangoni)" sasa maana hiyo utaijua vipi, kwanza lazima ufahamu nyoka hasikii vipi utamtoa pangoni, basi kujimiliki nikule kumrejesha nyoka pangoni akatulie, ukifikia daraja hiyo wewe utakua katika wale walotajwa kwenye aya ya 31 ambayo hawana dhara ima wakitizama au wakizungumza, Wana uwezo wa kumuweka Nyoka pangoni hata asitamani kutoka. Ukifikia daraja hiyo hapo tena unaweza kuzungumza unaweza kuangalia hakuna chenye kukushughulisha na wala Akili yako haisumbuliwi tena na matukio ya Nje, hiyo ndio maana ya kuambiwa jiepushe na Athari za macho na sauti.
No comments:
Post a Comment