Sunday, December 20, 2015

KUTANA NA NAFSI YAKO PART 1

Asalaam Aleiykum

Nakuletea Mafunzo haya kusudio langu ni kukutaka uende (deep), kukupa uchu wakutaka kujijua wewe nani na ukweli wa mambo ukoje, Upate kuelewa upande wa pili kuna nini?, ni changa moto ya kukupa au kukuwezesha ufanye uchunguzi wa kibinafsi katika jambo hili la kukutana na nafsi yako.
Kwanini leo ikawa nimeleta fundisho hili (Kinaga Ubaga)unajua nini maana ya kinaga ubaga?, Maana yake ni jambo kuwekwa wazi, Nimefanya hivi kwa sababu kuna baadhi ya Watu  wamediriki kusema (Sheikh) katika mafundisho yake anataja mambo mengi ya elimu za ajabu,elimu za Mashetani na mengi mengineyo, lakini hakuna hata siku moja tulopata fundisho kamili la elimu hizo za ajabu. Sisi tutakavyo japo siku moja tunataka kutuliza kiu chetu cha kujua kwamba hayo utuambiayo ni kweli unayafahamu.
Naam leo ni siku yangu ya kutekeleza matakwa yenu, lakini cha kunihuzunisha kuwa mnataka kunijua mimi kwamba niyasemayo ni kweli, ni dhumuni la kutaka kunipima kama kweli najua, sio kwa faida yenu ya kutaka kuzijua elimu hizo, na hilo halitosaidia chochote nafsi zenu, na kwa kufanya hivyo siku zote mtabaki kusema fulani anajua na sio mimi najua.
Kumbuka chenye faida na wewe na kukusaidia ni kile ulichojua Mwenyewe kwa kwenda (Deep), Sasa kabla ya kugusa fundisho letu la leo wacha niyajibu maswali yenu ya ajabu ili kila mtu aridhike ipasavyo na majawabu nitakayo yatoa.
(1)Swali la kwanza?Jee wewe Sheikh unafanya Utabiri?.
Jawabu:Utabiri upo wa aina tatu, kuna ule wa aina ya kwanza wa (Mzungu kalala wapi)huu ni wa kubahatisha, Na kuna ule wa pili wa Kupewa na Mollah wako wa kuyaona mambo yalokwisha katiwa amri kutokea, huo unapata kwa njia ya (Ilham), Na njia ya tatu ni ile ya kuwatumia wale wenye kwenda kusikiliza habari wakapata ya kupata na kuja kukuhadithia na hao ni (Majini) kama walivotajwa kuwa wanakwenda Mbingu ya kwanza kusikiliza amri zilizotolewa na kuchukua siri hizo kuzileta ardhini kabla hazijatekelezwa, ndio maana wanapigwa kwa vijinga vya moto, Ama kuhusu mimi kutabiri sifanyi jambo hilo, hata kama najua habari hizo basi ni kwa faida yangu mwenyewe.
Endelea part 2


KUTANA NA NAFSI YAKO PART 2

Asalaam Aleiykum

(2)Swali la pili, Hivi kweli Sheikh unafuga Majini?. Napenda kufahamisha kuwa Majini siwanyama kwa hiyo huwezi kuwafuga, ila wanaweza kuwa marafiki zako kama walivo marafiki zangu mimi.
(3)Swali la tatu, Hivyo inawezekana kuwaona Malaika?. Inawezekana lakini kwanza mpaka uisome darsa ya leo, ukiweza kuifahamu na kufanikiwa kutekeleza hayo mafunzo basi utakua na nafasi ya karibu kuwaona, lakini mpaka ukione hicho ntakacho fundisha leo pengine utapata uwezekano wa kuona na hayo mengine, kwanini nikasema hivyo kwa sababu Malaika wameumbwa kwa Nuru, Sasa swali la kujiuliza jee unaijua Nuru?,ushapata kuiona Nuru, ukiweza kuiona Nuru itakua rahisi pia kuwaona Malaika. Lakini kwa hivi sasa kuona kwako unategemea Akili, Yapo Mafunzo ambayo ukiyapata unaweza kuona viumbe wengine wa ajabu.
(4)Swali la Nne, Sheikh tumeona unajibu baadhi ya maswali ya ndoto, Jee unatumia kigezo gani kujibu maswali hayo?.
Naam kweli najaribu kujibu maswali ya ndoto au kutafsiri ndoto hizo, Nini Ndoto? Ndoto ni ujumbe unaokuja kwa lugha usiyofahamu, napenda ukumbuke kwenye ufalme wa Mwenye enzi Mungu hakuna lugha maalum inayotumika kuwasiliana na wewe isipokua kwa njia ya Alama au (Picha). Basi utakapo pata baraka za kuzijua Alama hizo na kusudio lake,  hapo ndio tayari utaweza kuzitafsiri ndoto na alama zengine. Na kuthibitisha hayo kihudhurie kisa cha Nabii Yusuf a.s (Sura ya Yusuf aya ya 4)

إِذۡ قَالَ يُوسُفُ لِأَبِيهِ يَـٰٓأَبَتِ إِنِّى رَأَيۡتُ أَحَدَ عَشَرَ كَوۡكَبً۬ا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ رَأَيۡتُہُمۡ لِى سَـٰجِدِينَ 
(Kumbusha)Yusuf alipomwambia Baba yake, Ewe Babaangu hakika nimeona (Katika ndoto)Nyota kumi na moja na Mwezi, Nimeviona (vyote hivi) Vikinisujudia.
Hapa maneno haya kayasema wakati yuko mdogo alipofikia umri wa (Baleghe)ndio akapewa hiyo elimu ya kutafsiri hizo ndoto kama isemavyo aya ya 22. Na zaidi utayapata katika kisa hichi kuanzia aya ya 46 ya sura hii ya (Yusuf).
Kwa leo namalizia hayo maswali manne na sasa tunaanza darsa yetu tulokusudia.
Endelea part 3


KUTANA NA NAFSI YAKO PART 3

Asalaam Aleiykum

Nadhani kwa maswali hayo manne imetosheleza kwa kiasi fulani majibu niloyatoa, Sasa umefika wakati wa kulihudhuria somo letu la leo ili kama lina manufaa basi likusaidie katika maisha yako.
Kwani utakapo kutana na miujiza hiyo itakubadilisha kuwa mtu wa aina nyengine kabisa utakua (Transform), Lakini kwanza napenda nitoe tahadhari kwa wale watakaoamua kulifanya zoezi au somo hili kwamba mimi sina dhamana kwa lolote litakalotokezea kinyume cha matarajio.
Kwanini nikasema hivyo kwa sababu mambo haya yanataka lazima awepo Muangalizi mjuzi wa funzo hili la kukutana na nafsi yako, lakini kwa kuwa mna kiu ya kujua elimu hizi nimeona kuna haja ya kuituliza kiu hiyo kwa kuyaleta mafunzo haya.
Basi moja kwa moja tunaingia kwenye darsa hii kwa kuchukua aya ndani ya Quran ili iweze kutufungulia somo hili, aya yenyewe inasema hivi(Saffat aya ya 138) وَبِٱلَّيۡلِ‌ۗ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ "Na Usiku je Hamzingatii"
Hapo kuna changa moto (Motisha)ya "Fahamu"au (Sense) au kuzingatia ita upendavyo, Nini Kuzingatia? kuzingatia ni tendo la kwenda (Beyond Mind) ukitumia Akili ina maana unafikiri, na fikira zinakaa kwenye (Memory lane) fikira ni kukumbuka yalopita,katika fikira hakuna jambo jipya(Mambo yote ya zamani) ima utakua una waza yalopita au kupanga yanokuja lakini kwa uwezo wako wa mambo yalopita.
Lakini kuzingatia ni ule wakati ulo nao, na hapa umetajwa usiku,huu usiku una nini?.Usiku ni wenye kuficha siri nyingi, usiku ndio wenye kutisha na mambo yote ya ajabu yamo na yanatokea usiku.
Usiku ni jambo maalum lakini kuujua lazima japo siku moja uishi ndani ya usiku, najua maneno yana kustaajabisha, lakini ndio ilivyo hivi sasa unapita tu kwenye jambo linaloitwa usiku, vipi kuishi kwenye usiku? Ni pale ambapo usiku unakutana na Roho yako(Tukajaalia huo usiku kama guo lenye kuwafunika)sio kukutana na Akili yako kama ilivo sasa, sasa vipi utakutana na huo usiku, utafanya hivi, Nenda Kijijini au Shamba  kakae japo siku tatu huko utakutana na usiku, huko Giza litaifunika Roho yako, Ni jambo la kutisha sana, unaweza kutoka mbio, ee hichi kiza kidogo cha mjini unaanza kuimba na kupiga miluzi, unatizama nyuma mwili wote unatetemeka,mara unakohoa na hapo ndio hakuna kiza cha kweli sasa nini habari yako utakapo kwenda kukutana na kiza cha kweli,sasa kwanini nikakwambia uende shamba, kwa sababu huku mjini huupati usiku, Mataa yalivoshamiri mpaka ndege hawapati usingizi.
Sasa vipi utauzingatia Usiku wacha nikupe maajabu ya usiku halafu utaanza kuzingatia, Nini kuzingatia?kuzinga-Tia ni kuizuia au kuikinga Akili yako au kuisimamisha ikawa haikumbuki chochote au kui(Shut-down) kwa hiyo ukiambiwa zingatia sio ulete fikira zako ila litizame jambo ukiwa huna wazo lolote na ukifanikiwa tu mara utaona majawabu yanakuteremkia bila ya kutarajia, lakini huwezi kufanya hivyo mpaka upate nyenzo ya kukupeleka kwenye hilo zingatio, kwa kuwa leo tumeutaja usiku basi nyenzo ya leo ninayokupa uifanyie kazi ni hii, Nakuomba zingatia kwanini "Wanaadamu asilimia 97 wanazaliwa na kufa usiku" nenda (Deep)Jiulize (Why)jawabu utakalolipata lina faida kubwa na wewe.
Tumepita kwenye aya inotukumbusha kuuzingatia Usiku na maajabu yake, Na Usiku huo huo ndio utatuonesha mengine yalojificha ndani ya usiku, Na mfano wa kwanza ni ule wa nyota, Nyota zipo lakini mchana hatuzioni mpaka uje Usiku kwa hiyo Usiku ni kama Kioo chetu kinacho tuonesha nyota na mambo mengine, Basi na sisi tutautumia usiku huo huo kwa kukutana na kile kisichojulikana.
Vipi Tutafanya hivyo, umetaka ujue elimu za ajabu sasa ni wakati wake soma kwa makini uwe mkakamavu kufanya majaribio haya.
(Quraan aya sura ya Qiyama aya ya 14)
بَلِ ٱلۡإِنسَـٰنُ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦ بَصِيرَةٌ۬ 
Bali Mwanaadamu ni shahidi juu ya Nafsi yake.
Mwanaadamu ana uwezo wa kuona (Nje na Ndani)kuona matendo yake,na vile vile kujiona Mwenyewe. Na hili ndilo somo letu la leo (Kujiona Nafsi yako) ziko njia mbili ya kwanza ni ngumu na unaweza kuifanya wakati wowote kukutana na nafsi yako, mimi nimekuchagulieni hii ya Rahisi ambayo utaifanya usiku.
Ikiwa kweli unataka kukutana na Nafsi yako, kukujiua kile wewe chenye kuishi ndani ya huo Mwili au (Body) yako basi utafanya hivi (Chukua Mishumaa Miwili Na Kioo kikubwa) weka Mbele yako kwenye chumba cha giza nene, washa mishuma halafu tizama moja kwa moja kwenye hicho kioo bila ya (Kupepesa)au kufunga macho,hakikisha macho yako hayafungiki hata mara moja, utafanya zoezi hili kwa muda wa saa moja, baada ya dakika arobaini utatokwa na mchozi (Kama ulopatwa na msiba)mengi yatamiminika kutokana na macho hayajafungwa kwa kipindi kirefu, machozi yakikauka utaanza kuona sura za kutisha na maajabu makubwa makubwa, unaweza kutoka mbio au akili zikakupotea kwa muda lakini usiogope hayo ni mataarisho ya kukutana na nafsi yako, baada ya saa moja kila kitu kitapotea mbele yako mfano wa kipofu, na hapo ndio utakua tayari kukutana na (Unknown)hicho kisichojulikana, mie siwezi kuhadithia nenda ukayaone Mwenyewe, ila tahadhari wakati huo usije ukawa mchafu,au ukawa unataka kufa au unataka jambo baya litokee na hivi na vile chochote kilichokua katika nia yako ujue kitatimizwa, na hiyo ndio hatari niloisema hapo mwanzo. Meomba kujua elimu za ajabu namie nimeitikia ombi lenu. Nafunga Darsa kwa kumuomba Mollah wetu atusamehe dhanmbi zetu, atutie mapenzi ya kumpenda yeye na Binaadamu wenzetu, hususan mayatima na maskini na kwa wale wasojiweza.Tunamuomba Mollah wetu awasamehe walotangulia pamoja na sisi wenye kufatia, atupe mazuri tuwe pamoja na waja wema.Msinisahau kwa dua zenu kama mimi nisivo kukusahauni kwa Dua zitokazo kwa Mollah wangu. Amin


Sunday, December 6, 2015

MIUJIZA YA QADARA PART 1

Asalaam Aleiykum

Unataka nikufundishe kitu chenye faida na wewe ambacho unacho lakini hukitumii, hutopenda wewe madhila ya maradhi na shida za machungu zikukimbie?, Basi leo nitakujulisha jambo kama utaweza kulifanya litakuwezesha kuishi maisha yako yote kwa furaha na utulivu.
Binaadamu tuko kwenye mateso makubwa kutokana na tabia zetu za kuto kuikubali(Qadir)au kuto kuifahamu hukumu au sifa hii ya Mwenye enzi Mungu, Kila Mmoja wetu yumo katika kuteseka na kubishana na uwezo huu wa (Qadir), matatizo yote yanatokea kwa kukisahau kitu fulani chenye kuishi ndani ya nafsi yako. Na kutokana na sababu hiyo ndio tutaendelea kuteseka mpaka tunaondoka hapa Ulimwenguni.
Sasa ni kitu gani hicho?, Kukijua kitu hicho lazima upite kwenye mfumo wa fahamu, na jambo la mwanzo katika mfumo wa Fahamu lazima ujijue udhaifu wako kuwa wewe umeumbwa na yupo Muumbaji, Na kwa ajili hiyo uamini kwa dhati kuwa kila jambo lako limemilikiwa na huyo alokuumba, na hili lisiwe jambo la kipuuzi kwako, ni lazima lende ndani ya moyo wako na ukumbuke kila wakati.
Jambo la pili uelewe fika kila jambo lenye kutokezea katika maisha yako yeye ndie mpangaji na wewe Kiumbe huna maamuzi katika hilo, Hiyo ndio (Qadir) ambayo ukiikubali basi wewe Muislam kamili, sasa nini kinatokea mpaka jahazi ikenda Mrama?.
Kinachotokezea hapo unaicha njia  hiyo ya (Qadara) ya Mwenye enzi Mungu na kujitenga nayo mbali kabisa, Na ukijitenga tu jambo la mwanzo lenye kutokea ni kukumbwa na Sahau, kwani wewe hujaisoma aya ya Mwenye enzi Mungu inosema.(Quran sura ya Talaq aya ya 12)
ٱللَّهُ ٱلَّذِى خَلَقَ سَبۡعَ سَمَـٰوَٲتٍ۬ وَمِنَ ٱلۡأَرۡضِ مِثۡلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ ٱلۡأَمۡرُ بَيۡنَہُنَّ لِتَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَىۡءٍ۬ قَدِيرٌ۬ وَأَنَّ ٱللَّهَ قَدۡ أَحَاطَ بِكُلِّ شَىۡءٍ عِلۡمَۢا 
Mwenye Enzi Mungu ni yule ambaye ameziumba Mbingu saba na ardhi kuwa mfano wa hizo, Amri (Zake)zinashuka baina yao, ili mjue kwamba Mwenye enzi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu(Qadir), Na kwamba Mwenye enzi Mungu amekizunguka kila kitu kukijua(Kwa elimu yake).
Yanatosha maneno yaliyomo kwenye aya hii kuwa ukumbusho juu yetu lakini bado tumo kwenye lepe lepe la usingizi ndio maana tunafanya kazi hii ya kuamshana.
endelea part 2


MIUJIZA YA QADARA PART 2

Asalaam Aleiykum

Mwenye enzi Mungu ndio Mwenye uwezo wa kila jambo yeye ndio Mwenye kupanga kila kitu na huku kakupa uhuru wa kuamua akijua marejeo yako yatakua ni kwake, Ikiwa utafata mipango ya Mwenye enzi Mungu hutopata tabu, wala hutoteseka, shida zitakuondokea ,kinacho kutesa hivi sasa ni hiyo sahau yako inochukua 95% ya Uhai wako, basi wacha nikutoe kidogo katika ufalme wa sahau nikukumbushe mambo ambayo pengine yanaweza kuamsha kitu ukaweza kujua vipi wewe umemilikiwa na huo uwezo wa (Qadara).
Jitizame wewe kuanzia Usingizi wako, vipi unaupata mbona huna mamlaka nao ukija lazima ulale, nini habari yako wewe mbona ikikushika njaa unapaparika kutafuta chakula nani alo miliki tumbo lako,jee na nini habari ya kuamka kwako nani mwenye kukuamsha ukaishi tena, Nani huyu anokupa uwezo huo wa kusema, Nani Mwenye kukuletea hicho chakula ukawa unaweza kula ukapata maisha yako ya afya njema, basi ukiyajua hayo machache yakakuingia ndani ya moyo wako utajua maana ya hiyo aya kuwa Mwenye enzi Mungu amekizunguka kila kitu kwa elimu yake, Na pia anajua kila kinachoendelea kwa mmoja wetu pamoja na matokeo yake.
Yeye ndie Mwenye kumpa huyu kidogo yule akampa kingi, Yeye ndie Mwenye kumpa Maradhi fulani na fulani akaendelea na afya yake(Kwa sababu mpaka huo mwili wako yeye ndie mwenye kuuhifadhi)Yeye ndie Mwenye kumpa huyu watoto yule akamfanya tasa, yote hayo kwa uwezo wa Qadara yake.
Sasa najua bado unajiuliza haya yote yenye kukufika yanatokea vipi?, Cha kwanza kabisa kinachotokea ni wewe kuondoka karibu na Mollah wako, Unapokua mdogo unakuwa karibu na Mollah wako bila wewe kujijua, ukifikia Umri fulani unaanza kukimbia kutoka kwa Mollah wako, kama vile unavoanza kutowasikiliza wazazi wako, mpaka huyoo unaenda arijojo(unapotea), na unapofikia umri wa utu uzima unaanza kurejea taratibu kuwa karibu na Mollah wako, unatafuta mambo ya dini yakoje, unakua mkali lazima watu wakusikilize, kumbe masikini unajuta makosa yako.
Kwa hiyo wakati umekimbia inakujia dhana kila ulichofanya au kukipata ni kwa ajili ya juhudi zako ndio maana ukafanikiwa, Sasa unataka nikujulishe nini juhudi zako zinakupa?, hakuna ila madhila, mateso, maradhi na haramu tupu. Kwanini ikawa hivyo?, kwa sababu Juhudi zinatawaliwa na ujanja, ulaghai, dhuluma, juhudi inatawaliwa  na harakati. Lakini (Qadir)inatawaliwa na subira, kwenye (Qadara)hakuna harakati, kila kitu kinakwenda kama kilivo pangwa,(Mfano niloutaja mwanzoni)Kula kwako,usingizi wako,Kuamka kwako, Utajiri wako, Afya yako,Maradhi yako wewe huna (Control)yoyote isipokua alitakalo Mollah wako, ndio maana ukaambiwa (haukufiki Msiba wowote usipokua kabla ya hapo umeandikwa).
Kwanini ikawa msiba kwa sababu (Nature)yako ni ya Raha na Furaha, ila ukitoka katika vigezo hivyo ndio misiba inakukumba kwa kuisababisha wewe mwenyewe kwa juhudi zako, Kwa mikono yako mwenyewe una (Create Action)unapata(Reaction)na hiyo ndio maana ya kuandikwa.
Ukiishi kwenye (Qadara)ndio utajua ama kweli Mwenye enzi Mungu ndie Mwenye uweza, anampa Umri mrefu amtakaye na kumpa Umri mfupi amtakaye, anamnyanyua amtakaye na kumshusha amtakaye, anamruzuku kingi amtakaye na kidogo amtakaye bila ya hesabu.
Hiyo ndio Qadara ambayo nakujulisha ili upate japo kwa uchache kujua nani Mwenye kuyapanga haya yote, nisije nikasema (Qadara)ukafahamu kumbe kila kitu kishapangwa, ukaacha kazi yako ya kufagia, usiwe umechoka kuuza duka au kufanya Biashara ukasema nimeambiwa Mambo yote yanapangwa Mbinguni, Usije ukaacha kazi yako ya uvuvi ukasingizia unaisubiri Qadara, utakua unafanya makosa makubwa, Kwani Qadara inakutaka ufanye nini?.
Endelea part 3

MIUJIZA YA QADARA PART 3

Asalaam Aleiykum

Napenda kukufahamisha hiyo Qadara ndio ilokuweka hapo ulipo,ndiyo ilokupa hicho ulonacho, wewe Mwenyewe huna uwezo wa amri kupata zaidi ya hayo ulonayo mpaka uondoke kwenye njia ya Qadara na kuanza kuhangaika, uchukue uhuru wako na kuanza kufanya jitihada yako kinyume cha Qadara, utafanikiwa kiasi lakini utafika wakati utajuta, utafika wakati utaona kwanini nilihangaika.
Lakini ukisubiri Qadara ikufanyie basi kwa njia za Miujiza utaelekezwa na mara kwa mshangao limekua lile alitakaloMollah wako, Sasa miujiza hii ufanye nini na wewe uipate, au hao waloipata walifanya nini hata wakafanikiwa.
Hilo ndio kazi za Dini zote kukumbusha, kwanini ikawa kukumbusha? sababu una sahau sana. Kwa sababu wewe unaishi ndani ya hiyo Qadir, lakini tatizo lako hukumbuki, kwani ukikumbuka unarejea Nyumbani kama mtoto alopotea, ukikumbuka kila kitu kina (Dis-Appear) Nimesema (Dis-Appear) kwa sababu hiyo ndio taratibu ya Ulimwengu huu, kila kitu kina Athari hizo, mara umelala ume(Dis)mara umeamka ume(Appear) mara umekumbuka mara umesahau, kwa hiyo muujiza ninao uzungumza hapa ni ule ukipata ile hali ya kukumbuka moja kwa moja ndio unakua ume (Master) umepata huo muujiza wa kuona kote kote, kwenye dhahir(Dis) na kwenye Batin (Appear).
Utakapofikia daraja hiyo hakuna chochote kitakacho kukugusa, Maradhi yakija yatakua yanashambulia mwili (Body)lakini wewe huna maumivu, Umasikini umekufika lakini wewe huna huzuni na wala haukugusi, Msiba unatokea lakini haukugusi, Mali imeibiwa wewe haikugusi, mtu kakutukana wewe hujali tena unaona anatukana jina lakini mimi halinigusi, mateso yanakuja wewe hayakugusi, Raha zinakuja wewe hazikushughulishi uko umetulia kwenye Ufalme wa Qadara.
Sasa ufanye nini kuupata muujiza huu wa Qadara?
Utashangaa vipi unapatikana muujiza huu, utashangaa urahisi wake,na pia utastaajabu ugumu wake wa jambo hilo, hakuna jengine ila neno moja unalolisema bila ya mazingatio, huku neno hilo likiwa limebeba muujiza huu mkubwa wa kukupa raha na starehe ya kuishi maisha yako bila ya dhiki, bila ya huzuni, bila ya shida,bila ya lawama.
Hakuna jengine isipokua neno la Shukurani, neno hilo (Alhamdulillah) unatakiwa neno hili litoke moyoni mwako (Deep)kwenye hazina yako ya kusubiri, iwe kila kinachokufika unashukuru, maradhi yakija jua Mollah kanikumbuka, furaha ikija jua pia umekumbukwa,shida zikikuzonga jua Mwenye Qadara anataka iwe hivyo, kumbuka kila kitu kinaletwa na Mollah wako, kama kula yako, kulala kwako, kuamka kwako, kusema kwako, kuhema kwako, jitahidi kujiweka katika hali hiyo kwa miezi sita uwe bila ya kusita unakumbuka jambo hilo la shukurani kwa kila kinacho tokea katika maisha yako, baada ya miezi sita, shida itakuja utaiangalia, maradhi yatakuja utakua unayaangalia yana udhuru mwili wako lakini wewe hayakugusi, Umasikini upo lakini unaungalia haukugusi,kwa sababu shukurani inakutenganisha wewe na Mwili wako, wewe na mambo yako, na unabakia Roho ilo shahidi wa hayo yote, na huo ndio muujiza kama ulivokuja huna dhara yoyote iliyokugusa, na hivyo ndio utakavo ondoka huna chochote kitacho kugusa katika Ulimwengu huu. Hakuna cha kukumbusha isipokua Kumshukru yule alokupa Uhai na uka (surrender) kwake na kuwa Muislam kamili. (Just be thanks full and Surrender) uishi katika muujiza wa Qadara.