Asalaam Aleiykum
Nianze kwa kusema kwa anayejua atacheka sana akisikia eti (Taqwa)ina mafundisho, Lakini inabidi tuseme hivyo kwa ajili ya wale wasoijua, Kwa wale wenye kujua wanaelewa Taqwa haina haja ya mafundisho, Kwa sababu hakuna yoyote Mwenye kufundishwa Mapenzi. Lakini huruma ziwafikie wale ambao hawajawahi kupenda, au kufikia daraja hiyo ya Mapenzi ya Taqwa, hawa wanahitaji muongozo, wanataka kujua wakifika kwenye hilo daraja wafanye nini?. wana wasiwasi labda itakuaje, huwezi kuwalaumu kutokana na wasiwasi huo kwa sababu katika hali ya kawaida wanaogopa kupenda, Nini habari yetu sisi wakiingia kwenye Mapenzi ya Mwenye Enzi mungu itakuaje, wengine wanaamua kujiua, wengine wanaihama dunia, wengine wanapoteza akili kwenye mapenzi haya.
Utaona kuna siri kubwa ya kuyakwepa Mapenzi haya kwa njia za kutafuta ulevi wowote ule, wengine wanasema hakuna chochote, lakini ndani ya nafsi kuna shaka inabakia ya kiu cha kutaka kujua Mapenzi haya ya aina gani?, jee haya maisha yana mwisho au yanaendelea?, Napenda ukumbuke (Kiu)Ulonayo na dhiki ya maisha haviondoki mpaka uyapate Mapenzi ya Mwenye enzi Mungu. Nataka pia uelewe sio hujayapata, unayo lakini bado huyajui.
Najua tunajiuliza siku zote haya mapenzi yanatokea wapi?. Jawabu itabidi ujitizame Mwenyewe, pale unapokua huna dhiki, huna magonjwa, uko safi utagundua kwamba wewe una vipande vipande vya mapenzi, mara unapenda Mwanamke au Mwanamme, mara unapenda gari, halafu huyo unapenda shamba lako, na mara unapenda watoto wako, Jee ushawahi kujiuliza yanatokea wapi mapenzi haya?, Umeshawahi kwanini unachukia kufa?, Jee huijui kama hiyo ndio (Nature) yako, Quraan inasemaje kuhusu jambo hili la mapenzi. (Aya ya 14 Al-Imran).
زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ ٱلشَّهَوَٲتِ مِنَ ٱلنِّسَآءِ وَٱلۡبَنِينَ وَٱلۡقَنَـٰطِيرِ ٱلۡمُقَنطَرَةِ مِنَ ٱلذَّهَبِ وَٱلۡفِضَّةِ وَٱلۡخَيۡلِ ٱلۡمُسَوَّمَةِ وَٱلۡأَنۡعَـٰمِ وَٱلۡحَرۡثِۗ ذَٲلِكَ مَتَـٰعُ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ وَٱللَّهُ عِندَهُ ۥ حُسۡنُ ٱلۡمَـَٔابِ
Watu wametiwa huba ya kupenda Wanawake na watoto na (wingi)mirundi ya dhahabu na fedha, na farasi wanotunzwa vizuri, na wanyama na mashamba, Na hayo ni matumizi ya maisha katika dunia, Na Kwa Mwenye enzi Mungu ndiko kwenye marejeo mazuri.
Sasa ukisha kulijua hilo nakurejesha kwenye aya ya (183)iliyomo ndani ya sura ya (Bakarah) inayosema Melazimishwa kufunga ili mpate kumcha Mungu, Hapo nakuomba uitizame aya kwa undani, usipite juu juu utakua huipati maana yake, na hapo ndipo wengi wetu tunashindwa kufafanua tafauti na kusudio la aya hii. Sasa pata nafasi ya kuijua maana yake halisi, ijue siri iliyopo hapo upate kuitumia kama utakavo ifahamu.
Nakukumbusha kwamba aya imesema ili upate kumcha Mollah wako, au kwa lugha nyengine yapate mapenzi kwa ukamilifu (Higher love)unakumbuka kule ulikua na vipande vipande huku kama utafunga kwa Imani na ukawa (Total)ume (Surrender) ndio unaipata hiyo Taqwa au (Mapenzi ya Mwenye enzi Mungu).
Napenda ukumbuke aya haikutaja ulishe mayatima, wala kutoa sadaka, hukuambiwa ufanye hisan kwa yoyote yule ila umeambiwa upate kumcha Mollah wako(seek the love of your god). Jee unaijua maana ya Kumcha Mungu?, Basi kama huijui tuliza fikra zako ili upate kuijua maana ya kumcha Mungu. Halina maana nyengine neno hili ila kulipa hadhi ya mapenzi, lakini kwa kuwa katika hali ya kawaida hatuyajui mapenzi ni nini, ni bora tuliache pembeni neno hili ili twende kuitafuta maana ndani ya mwezi huu wa Ramadhan.
Tunafundishwa maana halisi ya Mwezi huu wa Ramadhan ni kuufanya ni (Special)kwa ajili ya Mollah wetu, Ni kwa ajili ya kutafuta mapenzi ya Mollah wetu, kugundua utukufu wa yule alotuumba, kuzitafuta Radhi zake, Kuelekeza Fikra, mawazo, maswali yote kwa ajili ya kumjua Mollah wako, kuna msemo unasema (Gonga utafunguliwa), kumuomba atuwezeshe kuyapata mambo manne muhimu yaliyomo ndani ya hiyo Taqwa katika Mwezi huu wa Ramadhan, Mambo yenyewe yepi yaliyomo ndani ya mwezi huu?.
Endelea part 2
Monday, May 22, 2017
MAFUNDISHO YA TAQWA PART 2
Asalaam Aleiykum
Mambo hayo Manne yaliyomo ndani ya hiyo Taqwa ndio yatakusaidia kuyapata mapenzi ya Mwenye enzi Mungu, Na ukipata Mapenzi ya Allah hakika wewe umefanikiwa katika mafanikio yasio na mfano. Umo ndani ya ustaadh wa kulea Roho, jambo la mwanzo(1) kabisa ambalo ndio muhimu lenye kukutia au kukuletea hayo mapenzi ni hiyo "Shahada yako" Ya kumshuhudia Mollah wako ni Mmoja wala hana mshirika, Shahada hii daima unaitamka mdomoni(Lip sevice) inakua si lolote si chochote juu yako.
Sasa umo ndani ya Ustaadh wa kulea Roho na wewe unayataka mapenzi ya Mollah wako inabidi uende (Deep)ndio maana ya Ramadhan. Utakapoulizwa una shuhudia nini? ujue cha kujibu, usiwe unatoa macho huna cha kusema, sasa twende mimi na wewe tukatafute jawabu, vipi utalijibu swali hili ni lazima lihusiane na Roho yako na sio ulimi, vipi utaipata Shahada anza japo na Miti, anza kutafakari(Kwani maneno haya si yamesemwa ndani ya sura ya Ghashiyah 17-20)"Hawatazami jinsi ngamia walivoumbwa""Na Mbingu jinsi zilivyo inuliwa""Na Milima ilivyo thubutishwa""Na Ardhi Jinsi ilivyotandazwa", basi kama hivyo vitakua mbali ndio nimeanza na miti, tafakari kwa kujua kumbe hii miti inavuta pumzi kama ninavo vuta mimi, mimi natoa (Carbon dioxide) miti inaivuta ndani na kunitolea mimi (Oxygen)na mimi huyo navuta pumzi.
Pata kujua kwanini ukiona Rangi za kijani unajisikia (Fresh), jishughulishe uelewe kwanini kila ukenda Baharini unajisikia furaha, pata fahamu Jua lina mahusiano gani na mimi, Angalia wanyama mbona wana (System)kama mimi?, wanalala, wanakula, na ukifika muda wao wanakufa.
Fikiria pia kilichomo kwenye majani, na kwenye ardhi, na katika nyota pia kimo katika nafsi yangu, ukikaa ukafikiria japo muandamo wa mwezi na siku zake 28 basi kuna kitu ndani ya moyo wako kitakujulisha nini maana ya Mungu mmoja, au nini maana ya Shahada na wapi mapenzi yanapotokea, Na itakapotokea hali kama hiyo wewe Mwenyewe utagundua kumbe hii ndio taqwa, na hii ndio hiyo Rehma ninayo ambiwa, hapo ndio utapata nafasi ya kuliendea jambo la pili (2).
Nini hilo jambo la Pili ?.
Baada ya kuujuwa Uwezo wa Mwenye enzi Mungu na Ufalme wake, hapo tena kwa mapenzi ya hali ya juu unaanza kuomba (Mghfira)ita upendavyo(Kumi la pili)au Msamaha, unaomba msamaha huo kwa mara zisizo na idadi, usije ukadhani samahani yenye kutoka katika hali ya Taqwa ni kama ile yako ya kawaida ilojaa kiburi, unajiona ushaacha madhanbi na uko msikitini, au unafanya mema, Msamaha wa Taqwa ni ule wa (Realization)Msamaha wa kujua kwa yakini kumbe mimi nilokua na mkosea yupo, naye ndiye aliyeniumba akanipa uhai huu, Namuasi yule ambaye katika Ufalme wake kakidhibiti kila kitu pasi kuwa na mshirika, Huyu ndie Mollah wangu anayeniruzuku kila siku hata wakati ule nafanya maasi, Yeye ndie Mwenye kunipa Furaha kila niipatapo dhiki, Ananipa usingizi na Kuniamsha kila siku ya uhai wangu. Basi Mimi Mollah wangu sina cha kuomba mbele yako, na wala sistahiki chengine chochote isipokua Faraja ya Msamaha wako, na hakuna Msamaha utakao nipa mimi ila niyapate mapenzi yako ndani ya Mwezi huu wa na daima katika uhai wangu.
endelea part 3.

MAFUNDISHO YA TAQWA PART 3
Asalaam Aleiykum
Hapo utakua tayari kuliingia jambo la tatu(3) ambalo ni kumuomba Mollah wako (Pepo yake). Unapotajiwa pepo akili yako mbio inakimbilia kwenye jumba la ghorofa na mto(River)inapita mbele, basi umemaliza. Lakini Jambo unalo ahidiwa na Mwenye enzi Mungu elewa halina mfano, ikiwa haya maisha ya dunia katika huu (Uhai)ulopewa unaupenda hali hii, ukiambiwa sasa wakati wako ushafika wa kurudi Akhera unakua na huzuni kubwa, hutaki kwenda, unapigana kwa kila hali, mara dawa hii mara ile, iteni (doctor)huyu au yule, Sasa hebu fikiria nini habari yetu sisi hiyo Pepo, (Jicho halijawahi kuona, sikio halijapatapo kusikia) ina hali gani Pepo ya Mollah wetu.
Nyinyi Mmeonewa huruma ndio maana hesabu zenu zikazidishwa, kwa sababu wengine wana Maringo wanadhani vijithawabu vyao katika miezi ya kawaida vinaweza kununu pepo. Basi thamani ya hiyo Pepo imetajwa kama unataka kuinunua itazame fadhila iliyomo ndani ya mwezi huu, umeambiwa nini?.
Ukifanya au ukitujia na jambo moja la kheri katika mwezi huu wa Ramadhan malipo yake ni sawa sawa na mambo sabini (70)ya Fardh, Pia unaambiwa "Ewe Mcha Mungu" huu ni mwezi wa subira, Na kwa ajili hiyo ya kujizuia kwako na mambo yote, basi imekua zawadi ya subira yako ni hiyo Pepo.
Nini (Sabr)? Subira ni (Eternity) ni sehemu ambayo haina mwisho, subira haina saa wala dakika, haina usiku wala mchana, haina miezi wala miaka, ndio maana ukiingia ndani ya tendo la subira mara moja linatoweka, yatizame mambo yote mazuri yanakwisha haraka sana, kwa sababu umeonja subira, umeonja mapenzi, umeonja Taqwa, lakini zitizame dhiki unavoziona zinadumu milele, ndio maana ukilala hujui masaa mangapi mpaka uamke, lakini ukiwa macho (Unasema Mwenyewe Funga ya leo kali haimaliziki).
Basi kwa ajili ya Mollah wako umefanya subira na kukubali amri yake, kwa hiyo malipo yako ndio hiyo Pepo.
Hiyo ndio maana ya ukitujia na jema moja tunakulipa mara sabini, kwa sababu hilo moja lako limo ndani ya hiyo (sabr)Subira, Jee unaijua Sabini ya Mwenye enzi Mungu ikoje?. (Wallahi)ungeijua ilivyo basi ungeifata kwa Magoti na unyenyekevu ukawalisha watu japo kokwa ya tende, ukawafutarisha watu japo maji, ukawapa japo maziwa, Nini habari yako Mja wewe ulokushika Ucha Mungu Mwaka huu Ukaamua Kuwafutarisha Masikini Mwezi Mzima malipo yake yatakuaje?.
Enyi Mliopo Arabuni na Ulaya na Kwengineko zikimbilieni Thawabu hizi zitakuja kukusaidieni siku ya kufunga macho ya dunia, siku ambayo utashangaa unatolewa Roho yako na huku mbele unaoneshwa malipo yako kwa ajili tu ya kumfutarisha mwenzio alofunga. Fanyeni bidii kuipata hiyo Taqwa kwa kuwalisha watu futari, Hayo ndio mapenzi ya Mwenye enzi Mungu juu yenu. Anataka na nyie muyapate ndio maana anakuhimizeni na kukuulizeni vile tulokupeni mmevitoa, Angalia kawaida ya Mwanaadamu jee anayo Tabia ya kutoa, hutokuta ila wachache sana, na hiyo ndio dalili ya mapenzi, ukiona huwezi kutoa basi na mapenzi au hiyo Taqwa itakua ngumu sana kuipata.
Mwenye enzi Mungu kakupa uhai hapa duniani na kesho Akhera, Ukiijua Rehma hiyo ndani ya Mwezi huu wa Ramadhan basi utafanya bidii kubwa kuyaendea mapenzi ya Mwenye enzi Mungu.
Utabadilika kuwa Mtu wa aina nyengine, hutomuasi Mollah wako, hutopindukia mipaka uliyowekewa, Ndani ya Mwezi huu Mollah wako kakukumbusha kuwa wewe ni (Special)Kakupa (Gurantee)ya Msamaha kwa ajili ya hiyo (Taqwa)yako, kwa kuwa huu ni Mwezi wake (Special) kakupa hilo jambo la (4) la kukunusuru na adhabu ya Moto wa Jahannam. Hiyo ndio (Taqwa) ndani ya mwezi huu wa Ramadhan.

Monday, May 1, 2017
IJUWE RAMADHAN PART 1
Asalaam Aleiykum
Mwanzo napenda kufahamisha ili unielewe kwanini darsa hii ikaanza na sentensi (Ijuwe Ramadhan), kumbuka kuna tafauti nyingi ambazo zinatokea katika maisha na wewe bado huzifahamu, mfano kama (Kusikia na Kusikiliza)vitu viwili hivi tafauti lakini kuvifahamu lazima upate muongozo. Kawaida ya kusikia ni ile ya uhuru wa masikio kusikia kila kitu, Lakini kusikiliza inatakiwa umuhimu wa (Roho)yako ihudhurie pasi na kushughulishwa na chochote ili kukipa nafasi ya pekee hicho ambacho (Unaambiwa au kukisikia), kusikiliza unatakiwa usiingize chochote kati yake,kwa maana hiyo hata Akili yako isiingie kati katika hilo tendo la kusikiliza, Isiwe Mtu anakwambia kitu, wewe ndani ya Akili yako unatafisiri vyengine kabisa.
Hali kadhalika juhudi hiyo pia unatakiwa uifanye wakati wa kujifunza jambo, au ukiwa katika harakati za kujua. Kwa wale ambao bado hawajanifahamu wacha nifupishe misemo na kuwatolea mfano rahisi wa kujua, ni kama vile unafundishwa kuogelea ukaambiwa sasa jiregeze, usigombane na maji, peleka mkono huu taratibu mbele, mara huyo ukajiona umeelea, uko juu ya maji hapo inakua ushajua kuogelea na hiyo inaitwa (Experience),na hiyo ndio maana ya kujua.
Sasa vipi imehusiana na kuijua Ramadhan, Kwa sababu siku zote ""(Unasikia)"wanasema Masheikh Funga mwezi umefika, Na wewe huyo unaamua kukaa na njaa,Kwanini nikasema kukaa na njaa?, kwa sababu huipati Taqwa, pengine miaka yote hali kama hiyo inakukuta, sio makosa kwa sababu pengine ulikua hujui, lakini ukishamaliza kuisoma darsa hii ukaendelea kama ulivokua unafunga mwanzo, hapo utakua unatenda makosa kwa sababu umeshajua ila wewe sasa hutaki.
Nakuchukua katika (Deep sea) ili funga yako mwaka huu iwe vyengine kabisa, ili upate kujua kusudio la Mwezi huu na wewe ufunge kama mawalii, ufunge kama (Mystic). Siku zote nasema kama utaona mafunzo yangu (batil)huyafahamu, sio kama alivosema (Sheikh wako)basi niachie mwenyewe, mie ndio dhamana wa hili somo, na wewe baki na mwenendo wako, huna haja yakuchuma dhanmbi au kunitupia maneno yasofaa.
Kumbuka darsa zangu naziandaa ili nikufanyie (Shock)hakuna kitu kipya ila yale yale yalosemwa nyuma ila mimi nayaleta kwa njia nyengine tu. Kwa hiyo wakati mwengine utaona mbona mambo mepya haya, na hilo ndio kusudio langu, usibakie na mambo ya zamani, pata kujua mambo mepya, Ulimwengu huu una mambo mepya kila siku yanavumbuliwa, Kwanini unaogopa upya?. Naamsha moyo wako , Masheikh wanapiga kigoma cha daku kila mwaka na wewe bado umelala, sasa mimi nakuja na Tarumbeta(Saxphone)ili nipate kukushitua.
Nini Ramadhani?
Ramadhan ni kama ilivyo (Hajj)ila tafauti yake (Hijja)ni mara moja tena kwa mwenye uwezo, lakini Ramadhan ni kila mwaka unatakiwa ukahijji wapi?. Tuliza Akili upate kunifahamu vizuri na hii itakufanya uione Ramadhan kwa muonekano mpya kabisa, na kama darsa hii itafika moyoni mwako itakubadilisha milele kama ilivo nibadilisha mimi.
enedelea part 2

IJUWE RAMADHAN PART 2
Asalaam Aleiykum
Kwanini Nikasema kama (Hajj)?.
Kumbuka haya ni maneno yangu, au ufahamu wangu, na nitakuonesha kwa mifano ipi hata nikaita Ramadhan ni kama (Hijja)ya kila mwaka kwa Muumin, Yamekua Mapenzi ya Allah makubwa juu yetu kwa kutuletea Mwezi huu Mtukufu wenye Baraka kila mwaka.
Ili upate kunifahamu vizuri itabidi nikujulishe mambo mawili ambayo ndio msingi wa darsa yetu, Ama jambo la kwanza ni ile desturi ya "Bwana Mtume s.a.w alipokua kila akilizungumza jambo la Taqwa akionesha kifuani kuashiria ndani""Alikua akiashiria kitu kilichomo ndani akisema Taqwa imo ndani, Taqwa imo Ndani", Wengi hawalijui na wanadhani alikua akionesha kifua chake, au kuashiria moyo, lakini kusudio lake ilikua kutufahamisha kuna kitu ndani ya mwili wetu, hicho ndio chenye uwezo wa kutenda Taqwa, mkiweza kukijua, mkifanikiwa kukigundua, basi moja kwa moja unakua Mcha Mungu, na usidhani Ucha Mungu unapatikana bila ya kitu hicho, unaweza kujidanganya, nje ukawa Mcha Mungu, lakini ndani kutwa ukawa unazini, unadhulumu,unafisidi hapo bado hujawa Mcha Mungu, Ucha Mungu lazima uwe na (Control)ya ndani na nje, lakini ukiona bado ndani unateseka basi fanya jitihada, zidisha safari ya (Umrah) ya ndani mpaka ukijue hicho kinachoweza kutenda (Taqwa).
Ama Jambo la Pili nalopenda kukufahamisha ni zile (Ngazi)tatu za kukufanya wewe ufikie huo Ucha Mungu au kuwa Muislam kamili, Wengi katika sisi tumepata baraka(Blessing)za kuzaliwa ndani ya Uislam, tumeinukia kwenye Uislam, kwa hilo tunapaswa kumshukuru Mollah kwa hisan hiyo, kwanini nikasema hisan, kwa sababu wewe hukuchagua uzaliwe na wazazi wa dini gani, kakuchagulia Mollah wako ndio na wewe ukajikuta Muislam, pengine ungezaliwa na wazee wenye dini nyengine usingekua Muislam, ndio maana nikaita (Ihsan).
Sasa jambo la mwanzo katika hizo (step 3)kuwa wengine Uislam kwao unakuja (Automatic)kama kwa kuzaliwa, na wengine wanaingia kwa kupewa (dawa)au mawaidha wakubali kuwa waislam. Sasa Uislam ni ngazi ya kwanza, ni kama kitambulisho, ndio maana unakua Muislam lakini unatenda mambo yote yenye kukatazwa na Mollah wako, huna tafauti na asiyekua Muislam, halafu jambo la pili katika hayo matatu niliyo yataja ni lile la wewe kuwa Muumin, Nini Muumin?.
Ni yule aliyeanza kuzitii Amri, akaanza kuzifata kidogo kidogo, mara anateleza anaanguka, ikisha anainuka na kuendelea na safari ya kujitahidi kuwa Muumin, Halafu jambo la tatu kukutana na (Truth)kufungukiwa na fahamu, kukutana (Face to Face)na yakini ya mambo yalofichwa kwa uwazi.kupata uhakika kwa njia ya (Ilham)Na ukipata au kujua uhakika hapo unakua Mbarikiwa, na wala si kwa njia ya kusoma sana ukakusanya (Information), Ni njia ya ku (Experience)kwenye moyo wako, hapo ndio inatokea hiyo (Surrender),unakua (Total)umewasili kwenye kisiwa cha (Taqwa)sasa wewe unaweza kuvaa taji la (Ucha Mungu).
Hapo ulipo visa vyote vinapotea, huna haja ya chochote, umeshagundua utajiri wa Mwenye enzi Mungu, humtegemei tena Binaadamu mwenzako, unakaa kimya kuangalia Ulimwengu, Raha za hali kama hiyo sio tena za Ulimwengu huu (Full of bliss). Hapo huna tamaa, huna chuki, huna ufisadi, huna hamaki, hutaki maasi, vyote vinatoweka katika nafsi yako, Na hiyo ndio funga ya Ramadhan ambayo na wewe unatakiwa uionje kila mwaka, pengine ukiigusa au kuionja hali kama hiyo unaweza kuamua kudumu nayo, ndio maana nikaita kama (Hijja),nenda kahudhurie uipate kila mwaka. Na hayo ndio mashiko yenye kutufungulia darsa yetu ya leo.
Endelea part 3

IJUWE RAMADHAN PART 3
Asalaam Aleiykum
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡڪُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِڪُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ
(Bakarah 183)
"Enyi Mloamini Mmelazimishwa kufunga(Saumu)kama walivyolazimishwa waliokua kabla yenu ili mpate kumcha Mungu"
Kwanini aya ikaanza na enyi Mloamini melazimishwa, kwa sababu mngeambiwa mmeamrishwa bado mngebakia kama waislam wengine wanaendelea kutenda dhanmbi, wanabakia na kitambulisho tu cha majina, lakini kumbuka hiyo lazima ya hapo ni lazima ya mapenzi, sio lazima ya mtutu wa bunduki kama hufanyi utakufa, ila Mollah wako anataka uonje ladha ya kumtii yeye inakuaje, hali inayo kutokezea ukiwa karibu naye, anakutaka japo mara moja kwa mwaka uka (Hijj)ndani ya nafsi yako ujijue (How bless are you).
Sasa kwanza tuitizame funga yenyewe ina siri gani?, sitaki kwenda kwenye faida zake katika darsa hii nikawa kama nafanya biashara, kwani wengine wanasubiri wasikie funga inaponesha maradhi, ndio wanafunga ili wapate kupona, inafanya hivyo sikatai, lakini ukifunga kwa ajili hiyo utakua umeikosa Taqwa, unatakiwa ufunge kwa ajili ya mapenzi ya Mollah wako ili ukutane na hicho chenye kutenda taqwa.
Nini funga inafanya juu yako, na kwanini nikasema (Hijja)ya kila mwaka, siku zote unafunga hujui mambo haya, sasa kuanzia leo nataka funga yako iwe ya aina nyengine isiwe kama za miaka ya nyuma, ndio maana nikakwambia kwanza (Ijue Ramadhan)halafu ndio utaifunga kwa vizuri, ikisha ndio utaipata hiyo Taqwa.
Kitu cha mwanzo kabisa nataka ukumbuke tu, ndipo utaipata hiyo (Hijja)ya kuhudhuria (Body)Mwili wako, ili upate kujua vipi inakua, vipi unakumbuka, Jambo la kwanza kabisa au saumu yako ya mwanzo unapata jambo la kuwa (Alert)(Awareness) au Dhahir, unapata fahamu kuwa hujala, sasa itabidi ujiulize huyu nani mwenye kujijua sijala, na kuwa nimefunga, ukishagundua hilo litaanza kukupeleka kwenye mambo mengine moja baada ya jengine katika nafsi yako na hiyo ndio (Hijja)yenyewe nilokusudia.
Utaona vipi Akili inavo hangaika na kuhaha kutaka chakula, kwa kuwa (Body)yako yote ni (Intelligence)tupu inatambua kuwa (Boss)leo kagoma kuleta chakula, hakuna huduma kutoka nje, kwa hiyo inaanza kwenda ndani kwenye (Store) na kutoa akiba hapo (Body)inajilisha yenyewe(Cannibal)unajila mwenyewe, na hapo unapata hiyo (separation)baina ya Mwili wako na hicho chenye kutenda Taqwa ukiweza kulijua hilo unakua wewe ni Mwenye kufuzu.
Mara unaona njaa hiyo imepotea , kumbuka huyu mwenye kuona ni nani?, Ikipotea njaa mara unakuja usingizi, na usingizi upo wa aina mbili uko ule wa kulala umezidiwa au ule wa kujizubaisha ambapo Akili sasa imehamaki inakwambia rudi kwenye desturi yetu ya Miezi 11, ya nini unataka kugundua au kufanya jambo la Taqwa, wewe shika simu, au angalia TV, au twende tukajiliwaze senema, hee basi safari hii hata barazani hupiti, Akili inakuvuta kwenye mazoea yako ya kumuasi Mollah wako, inakurudisha katika yale mambo yote unayofanya miezi 11 ilopita, mimi nakwambia safari hii pigana na akili, Yaache mambo yote ya Mwezi wa kula mchana, nenda kinyume na maamrisho yake, vipi utafanya? usije ukashindana na akili, huwezi kushinda, ila nakupa (Trick)mawazo yote yakija (Just watch inside you)ukiweza kuangalia Akili yako mara baada ya sekunde chache wazo la karata, barazani,sokoni, kutizama wanawake au wanaume litatoweka, kidogo kidogo utaanza kuishinda Akili.
Kawaida unakuwa ni mwenye kushinda vita ya ndani, Njaa pale inapokuja unaipuuza, usingizi unapokuja unaushinda, lakini Ramadhan zote vita vya nje vinakushinda na hilo ndilo lenye kukukosesha hiyo Taqwa, Basi kama ulivoamrishwa na Mollah wako kumbuka Taqwa haitakiwi iwe nusu, inatakiwa (Total)Taqwa ni ncha mbili ndani na nje ndio uweze kuifikia, uweze kuigundua, uweze kuifanya, Kumbuka ndani unaishinda njaa, sex,usingizi, lakini nje mambo yote yanaendelea kama kawaida, haitakiwi hivyo, kuipata Taqwa unatakiwa hiyo (Surrender total)Itakubidi mwaka huu ubadilike, funga yako iwe ya aina nyengine, jiandae na mambo ya nje yote uyaache, kumbuka ni siku chache tu lakini manufaa yake ni ya kudumu, ikiwa unaweza kujizuia Bia na sigara na mirungi, maji, chakula na vyengine vyote unaweza kuviepuka, basi mwaka huu ongeza mambo ya nje, kimbia mambo ya kipuuzi, iepuke simu, achana na facebook, acha kukimbilia mazungumzo ya kipuuzi,gomea mipira,ichukie Tv,usitizame machafu,usende karibu na mambo machafu, acha kudhulumu, usiseme seme sana, acha uongo, jiepushe na matamanio, acha kuwa muandishi wa habari kuwa kila kitu ushuhudie, acha kukaa kuanza kufikiria mafutari, ukiweza kubakia (Empty) au kufanikiwa kuyashinda mengi katika hayo japo kwa siku tatu za mwanzo, hapo utaanza kupata (Glimpse)ya hiyo Taqwa, utaanza kui (Experience) wewe mwenyewe, nitakua sina haja ya kukuhadithia.
Taqwa itaanza kuzaliwa kwenye Roho yako, Utakua Mwenye(Bliss)umewasili nyumbani, (You are Blessed) Taqwa itakuchukua pale ambapo wanafika Mawalii, wanapofika (Mystic)utafika hapo kwenye kujibiwa duwa, utafika hapo kwenye (Makarama)yote wanapofika wacha Mungu, hutotaka tena Mtu akuombee dua, Hapo ndipo iliposemwa kumi la Mwanzo ni (Rehma)hiyo ndio taqwa ambayo ukiipata wewe ndio utakua shahid wa hilo, kumbuka darsa hii ni kuijua na darsa ijayo ukishakua katika hali ya hiyo Taqwa nini kinatokezea?kwanini nikasema kinatokezea kwa sababu hiyo ndio (Nature)ya Taqwa, na kama haitokezei basi unakaa na njaa, na wakati wa kukaa na njaa sasa ushakwisha unatakiwa ufunge huku umeshiba, na hiyo ndio Taqwa, na kumbuka ukishiba chakula lazima ukigawe, na hilo tutalikuta katika mada ya (Mafundisho ya Taqwa)Tukijaaliwa na Mollah wetu kabla ya kuingia katika mfungo wa Ramadhan.

Subscribe to:
Posts (Atom)