Monday, January 1, 2018

SIRI YA UCHAWI PART 2

Asalaam Aleiykum

Pata habari hii ili utakapo tafuta dawa ujue unajitibia nini, upate kutambua vipi utaikata hiyo (Medium) isifanye kazi kwenye Mwili wako. Kumbuka nimetaja hiyo (Medium) ni kama (Transmiter) ya hayo yanofanyika kukuingia wewe kwenye (Body)Mwili wako.
Kumbuka tuko kwenye darsa ya Uchawi ambao wengi unakuteseni sana kutokana na Majini na Binaadamu kuitumia Elimu hii walonayo kukurogeni, leo hapa sitokwenda (Deep)lakini nitakufahamisha Vipi Unarogwa?, Tega macho uzuri huenda hili likawa na faida na wewe katika kuipata nafuu yako.
"Sura ya Naas na aya zote 6"
"قُلۡ أَعُوذُ بِرَبِّ ٱلنَّاسِ (1) مَلِكِ النَّاسِ (2) إِلَـٰهِ ٱلنَّاسِ (3) مِن شَرِّ ٱلۡوَسۡوَاسِ ٱلۡخَنَّاسِ (4) ٱلَّذِى يُوَسۡوِسُ فِى صُدُورِ ٱلنَّاسِ (5) مِنَ ٱلۡجِنَّةِ وَٱلنَّاسِ (6)"
Sema: Najikinga kwa Bwana Mwenye kuwalea(Viumbe)(1)Mfalme wa Watu(2)Mollah wa viumbe(3)Na Shari ya Mwenye kutia wasiwasi (Ikisha)Mwenye kurejea nyuma(4)Atiyae wasiwasi nyoyoni mwa watu(6)Ambaye ni katika majini na watu.
Naam hiyo ndio habari ambayo inayohusu mambo ya Uchawi, kwanini ikawa hivyo, kwa sababu hiyo ndio kusudio la hiyo sura, ndio maana hutumiwa sana kwenye mambo ya dhara ya Uchawi, Sasa wacha tuchambue kidogo kidogo ili tutoe ufafanuzi wa hayo maneno.
Na uzuri zaidi imekuja na aya sita kama ilivyo (Symbol) ya kichawi na (Number  6).
Najikinga kwa Bwana Mwenye kuwalea viumbe, Kumbuka wewe umo ndani ya Ufalme wa Mwenye enzi Mungu, Mollah wa viumbe vyote majini na Binaadamu Malaika na vyenginevyo ambavyo hatuvijui, (Tupia macho maneno ya tafsiri inayofata)"Na Shari ya Mwenye kutia Wasiwasi ikisha akarejea nyuma"Uchawi ni Shari kwa sababu hiyo anautia kwenye Nafsi au (Body) yako ikisha hakai anarejea nyuma, kwanini akarejea kwa sababu hakuna yoyote anayeweza kugusa Roho yako, ndio maana akisha fanya uharibifu kwenye Mwili wako anakaa nyuma kuangalia vipi unahangaika, afanyayo hayo iwe Jini au Binaadamu.
Naam Wanafanya nini Mafisadi hawa?. Wanachofanya ni kutia wasiwasi kwenye kifua cha Mwanaadamu, wapi wanatia wasiwasi huo?.
Endelea part 3


No comments:

Post a Comment