Asalaam Aleiykum
Mwaka mpya mambo mepya, Katika jambo la dini Mja ni haki yako ya kimsingi kukijua kila kitu kwenye Ulimwengu huu, Sasa ikiwa ni haki yako ya kimsingi kuyajua hayo jiulize kwanini haya ya (Kichawi) yamefichwa na hayajulikani.
Sababu kubwa ya kufichwa kwa mambo hayo ni Madhara ambayo kama yangeachiwa huru kila mtu kuyajua basi tungemalizana kama kuku. Mwenye enzi Mungu Kaificha Elimu hii kwa maelezo yaliyomo kwenye Quraan aya ya 102 (Baqarah)
"وَٱتَّبَعُواْ مَا تَتۡلُواْ ٱلشَّيَـٰطِينُ عَلَىٰ مُلۡكِ سُلَيۡمَـٰنَۖ وَمَا ڪَفَرَ سُلَيۡمَـٰنُ وَلَـٰكِنَّ ٱلشَّيَـٰطِينَ كَفَرُواْ يُعَلِّمُونَ ٱلنَّاسَ ٱلسِّحۡرَ وَمَآ أُنزِلَ عَلَى ٱلۡمَلَڪَيۡنِ بِبَابِلَ هَـٰرُوتَ وَمَـٰرُوتَۚ وَمَا يُعَلِّمَانِ مِنۡ أَحَدٍ حَتَّىٰ يَقُولَآ إِنَّمَا نَحۡنُ فِتۡنَةٌ۬ فَلَا تَكۡفُرۡۖ فَيَتَعَلَّمُونَ مِنۡهُمَا مَا يُفَرِّقُونَ بِهِۦ بَيۡنَ ٱلۡمَرۡءِ وَزَوۡجِهِۦۚ وَمَا هُم بِضَآرِّينَ بِهِۦ مِنۡ أَحَدٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَيَتَعَلَّمُونَ مَا يَضُرُّهُمۡ وَلَا يَنفَعُهُمۡۚ وَلَقَدۡ عَلِمُواْ لَمَنِ ٱشۡتَرَٮٰهُ مَا لَهُ ۥ فِى ٱلۡأَخِرَةِ مِنۡ خَلَـٰقٍ۬ۚ وَلَبِئۡسَ مَا شَرَوۡاْ بِهِۦۤ أَنفُسَهُمۡۚ لَوۡ ڪَانُواْ يَعۡلَمُونَ "
"Wakafata yale waliyofata Mashetani(Wakadai yalikua)Katika Ufalme wa (Nabii)Suleiman, Na Suleiman Hakukufuru, Bali Mashetani ndio walokufuru, wakiwafundisha watu uchawi,(Ambao wakiujua toka zamani)Ulioteremshwa kwa Malaika wawili, Haruta na Maruta katika Mji wa Babil, Wala (Malaika hao) hawakumfundisha yoyote mpaka wamwambie, "Hakika sisi ni Mtihani" (Wa kutizamwa utiifu wenu)basi usikufuru. Wakajifunza kwao ambayo kwa mambo hayo waliweza kumfarikisha mtu na mkewe (Na mengineyo chungu nzima). Wala hawakua wenye kumdhuru yoyote ila kwa idhini ya Mwenye enzi Mungu. Na wanajifunza ambayo yatawadhuru wala hayatawafaa. Na kwa Yakini wanajua kwamba aliyekhiyari(kuridhia)haya hatakuwa na sehemu yoyote katika Akhera. Na Bila shaka ni kibaya kabisa walichouzia(Starehe za)Nafsi zao(Kwa ajili ya kuikosa Akhera)laiti wangelijua(wasingelifanya hivyo).
Naam, Baada ya kutufukuzisha Peponi wameamua kutufata huku huku Ardhini ili kutupoteza, huu Uchawi ulikuja kama mtihani unapewa elimu halafu unatizamwa utaitumia vipi elimu hiyo, Ni elimu iliyofichikana ino khusu (Physiology) ya Mwanaadamu ndio maana hapo ikatajwa moja katika hayo ni kule (Kumfarakisha mtu na mumewe au mkewe).
Utakapo niuliza mimi nini (Uchawi) Nitakujibu ni (Medium) ni chombo cha siri chenye kutumwa kuwasiliana na jambo au kitu kwa ajili ya utendaji wa kazi yake.
"Leo hapa nazungumza tawi moja la uchawi katika matawi chungu nzima ya kichawi", Ni muhimu kulizungumza tawi hili kwa sababu linagusa moja kwa moja kwenye hiyo furaha yako, Nini Furaha?, Furaha ni Afya na Uchawi unaharibu au kudhulumu afya yako, na afya ikiguswa Binaadamu umemalizika.
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment