Asalaam Aleiykum
Mwanamke ni Mwenye kuja katika maisha ya ndoa akiwa na moyo wenye kuamini, anajitolea maisha yake kuishi na wewe akiwa na yakini ndoto zake zote zitakua kweli, kwanini nikazitaja kuwa ndoto, kwa sababu kwenye ndoto ukiamka hamna chochote, majumba yote na magari, na maua yote unayaacha usingizini.
Sasa kwa kuonesha Shukrani zako kwa huyo Mwanamke ndio unaambiwa mpe zawadi ya kukubali kwake, Lakini wapi ukisha kukubaliwa mipango yako yote unafanya upate kumtawala huyo mwanamke(Umekua kama Mvuvi). Na Mwanamke akiona kuna vita vya kutawaliwa na yeye anajiunga, japokua anajiunga kwa ustadi mkubwa na wanaume wengi hawalijui hilo, Na yeye anataka atawale.
Ndio utaona hapo (Kifo cha mapenzi)kinatokezea, Nyumba hiyo utakuta yanabaki mazoea, Rohoni kila mmoja anasema tukiachana wazee watasemaje, Majirani watazua nini, kila kitu kinawahusu watu wa nje, (What about you)?. Utaona katika maisha hayo ya ndoa kila mmoja anaota kucha zake, Mume anaona kanunua kitu, anamgeuza Mkewe (as Thing)anasahau kabisa kama harusi ni muungano wa (Two Beings)Waja wawili waloamua kuishi pamoja, na katika maisha hayo hakuna mtawala, kwa sababu nafsi yoyote haichukui madhila ya kutawaliwa, kuna siku itatafuta uhuru wake.
Kwa hiyo Ndoa ikiwa ya hali hiyo ule Mlingoti wa Bendera ya mapenzi unageuka na kuelekea upande wa chuki.
Mwanamke daima anakuja kwenye ndoa akiwa na mbegu ya Mapenzi, anakuja hana chengine cha ku(Offer) ila ana moyo ulojaa (Trust)kwa Mumewe, atakuta hichi na kile, atafanyiwa hivi na vile, Ndio maana utaona maharusi wote wamo furahani, ni kazi ya Mume kulipalilia shamba hilo la mapenzi, ni kazi ya mume kulitilia maji na linapokuja kuchanua basi Maua yake ni mapenzi matupu.
Vipi utaanza kazi hiyo ya Mkulima, jambo la kwanza kabisa lazima Mkeo awe Rafiki yako, lakini wapi, angalia Tabia zako, Marafiki wa nje ndio wanakua washauri wako, wao ndio wanakua wanapewa safu ya mwanzo katika maisha yako. Kutokana na sababu hiyo ndio utamuona Mwanamme anapigana vita ya nje asionekane yeye (Mume Maridhia)anaogopa watu wasiseme mbona haji mpirani, mbona hatumuoni barazani, Marafiki na watu watasemaje, Na akirudi nyumbani anapigana vita vya ndani, mimi mumeo, ndio nishasema, ukitoka nje talaka yako,(Kifo cha Mapenzi)kinatokezea, hapo tena na yeye Mwanamke anatafuta mashoga vinaanza visa vya kusemana kwa marafiki na kwenye familia.
Tayari inakua mizizi ya fitna ishapandwa, baada ya kuota penzi linaota tunda la chuki, Mambo yanaanza kubadilika, hata kauli zinakua hichi changu, Na changu ni cha peke yangu, kwa kuwa (Nature)yako tayari ina mapenzi unaanza kupenda vyengine, Maskini na Mwanamke kwa kuwa yuko ndani anaanza kuteseka, anaanza kufanya kazi ya kuondosha mapenzi juu yako, mapenzi yanamtesa moyoni, hana uwezo, haviwezi vita vya Mwanamme, ndani mapenzi hakuna ila kuna jeraha.
Ndugu wanaingia kati, usidai talaka, stahamili, ishi kama maiti hamna neno sote tunaishi kama (Mazombie)ndani ya majumba, zitizame ndoa nyingi majumbani kwetu utaona wawili hao wanaishi kama (Maiti mbili zilokufa kifo cha mapenzi). Ndani ya Kaburi hilo hakuna masikilizano, hakuna mapenzi, na Rehma ishaondoka siku nyingi sana, Yamebaki mazoea, pengine mtu anaogopa asije akaumwa au kufa peke yake, umebaki wajibu ulotawaliwa na chuki na mashambulizi, masimango hayeshi, maneno ya ajabu yanatoka vinywani mwao(Matusi)ikifikia hali hiyo utamuona Mwanamme huyo anaenda kutafuta Mwanamke wa Nje(Kimada).
Na Mwanamke naye anageukia senema anaanza kwanza kumpenda Mwanamme wa senema(Govinder)mara (Sharukhan)hapo inakua hamkani si shuwari tena, Inapatika (Destruction of family life).
endelea part 3
No comments:
Post a Comment