Wednesday, February 1, 2017

KIFO CHA MAPENZI PART 1

Asalaam Aleiykum

Wanauliza wenye kuuliza nini siri ya Ndoa yenye kudumu muda mrefu?. tupe habari hizi ili nasi tufanikiwe, Waulizaji wa swali hili wanaonesha ushupavu mkubwa wa kuuliza, si wengi wenye ushujaa huu wa kuweza kuuliza swali kama hili, kwenye chumba cha Mtihani kila mtu anakaa kimya, na hivi ndivo lilivo kwa watu wengi wenye matatizo ya ndoa.
Leo mmenitoa kwenye (Darsa zangu)Menileta kwenye uwanja wa mapambano ili nipate kuchangia habari hii ya (Kifo cha Mapenzi)kwenye ndoa zetu, ndani ya majumba yetu, ukiulizwa swali una njia mbili za kujibu, moja ya kukinga ujinga wako unafanya unajua, na njia ya pili kutoka kwenye werevu wako ulojaa hisia za hekima zisokua na hatia. Isikilize habari hii iwe na faida na wewe ili upate muongozo fulani wa kukaribisha furaha kwenye maisha yako.
Jawabu:
Nini Kinatokea chenye kwenda kinyume na aya iliyomo katika sura ya (Al-Rum 21)?
"وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦۤ أَنۡ خَلَقَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٲجً۬ا لِّتَسۡكُنُوٓاْ إِلَيۡهَا وَجَعَلَ بَيۡنَڪُم مَّوَدَّةً۬ وَرَحۡمَةً‌ۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ "
Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, Naye Amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya zimo ishara kwa wenye kujua(Wenye kufahamu).
Umezitizama wewe Alama? Umeshakaa ukajiuliza vipi umekutana na huyo uliyenaye hivi sasa?, na kwanini ikawa huyo?, nani alokukutanisha.?"Na kwa Alama zake amekuumbieni wake zenu" Mbona wewe umeacha wote umekwenda kumuoa huyo ulonae? ushawahi kujiuliza swali hilo, umejiuliza mbona tabia zimelingana?, mbona tumezoeana?, kwanini tunaishi pamoja?, imekuaje tumepata Watoto hawa?, kuna Hikma gani kwa Mollah wetu kutufanya sisi kuwa(Family)?.
Umepata kukaa kujiuliza maswali hayo, au unakwenda huku umefunga macho, basi kama umeyafunga nakuomba ufungue, kwani juu yako kuna siri kubwa ya wewe kupewa baraka hizo za kuishi na mwenzio(au kukutanishwa na huyo ulo naye mkeo), huyo Mwenzio umepangiwa wewe na yule ambaye humuoni wala humsikii, na katika Ishara zake "Amekuumbieni wake zenu" katika jinsi zenu, basi Picha hujui kutizama, basi huoni mkeo kuna mambo kafanana na wewe, basi hata ishara huzioni?."Utulivu"ulokua nao umepotelea wapi"?,mbona hutulii (What Happen).
Kumbuka nikizungumza Jaala nazungumza kitu chenye kuja na kuondoka, kama ilivyo huruma ni mfano huo huo, Mlipoambiwa Mmejaaliwa mapenzi na huruma baina yenu hiyo ni zawadi jee mliipokea zawadi hii au hamjui kama mmeletewa, basi nakwambieni zawadi hiyo ipo kinachotakiwa ni kurekebisha fahamu zenu ili na nyinyi muingie katika kundi la watu wenye kujua akama walivotajwa mwisho wa hiyo aya. Mapenzi yapo kwenye Ulimwengu huu kama yalivo Maua.
Sasa swali la kujiuliza mbona hatuyaoni mapenzi, mbona hatuoneani huruma, mbona tunatesana, Naam sababu kubwa Meshughulika kuyatafuta Nje, Mmekazana lazima muyaone yanavoteremka kutoka Mbinguni na hilo ndio tatizo kubwa la wana ndoa wa siku hizi.
Nini Ndoa?, Kwa Tafsiri ya haraka Ndoa ni Ndoana, Kama huijui ndoana ni kifaa cha Mvuvi ambacho anatia chakula kumvutia Samaki, yule samaki akiona hukifata na kukila chakula kile na hapo tena huwa kanasa, Hapo ndio inaitwa ndoana,  na humfanya atakavyo huyo samaki. Sasa iwapo wewe itakua mume mvuvi itakua una anaanzisha matatizo kwenye ndoa yako.Na Samaki ukishampata huna shughuli tena, ukiwa na mawazo kama hayo ndugu yangu umo hasarani.
Vipi Matatizo yanaanza?, Matatizo yanakuja pale nyie nyote wawili kusahau kuwa mapenzi na huruma mnajaaliwa, Mnasahau jambo hilo na kusikiliza Familia inasemaje, Wakwanza kabisa kuyaua mapenzi ni hao Ndugu zako, unasikiliza watu wenyewe wana matatizo makubwa, nini wanafanya?, Wana Itikadi zao sijui zimetokea wapi, utaona anaambiwa sio kampende Mkeo au Mumeo ila anafundishwa, ukenda kumshika kichwa mkanyage mguu asije akakutawala, nuia awe chini yako, maskin sio kapendaneni ila kagombaneni, (Massage)waloipata maharusi hawa ni hiyo, kwa hiyo kila mmoja anakwenda kajiandaa kivita, wasia huo unakwenda(very deep). Tahadharini mafunzo hayo yanapelekea kuharibu maisha ya wanandoa hao.
Sasa kwa kuwa washapewa  mafunzo ya kupandiana vichwani, penzi halina nafasi tena ya kushuka kwenye moyo, linabakia akilini, kazi kutazamana, mara fikira hizi mara fikira zile, harusi mwezi wa kwanza mtu kashika kulinda simu,tayari ana hasira na wivu. Mbona imekua hivi, mbona tabia zake namna hii, mbona kanenepa, kwanini anakoroma, Baada ya hapo sasa kwa kuwa umetoa mahari linaingia lile kubwa la (possession)Utawala, unamfanya sasa ni mali yako, unahisi umemnunua huyo Mwanamke, kumbuka hiyo ni zawadi ulompa huyo Mwanamke hayo (Mahar).
Endelea part 2


No comments:

Post a Comment