Wednesday, February 1, 2017

KIFO CHA MAPENZI PART 3

Asalaam Aleiykum

Kama pamezaliwa watoto hapo tena magonvi yanaanza kuwadhuru na watoto, mama anakuwa mgonjwa na baba pia wote wanaumwa, Wanaumwa maradhi ya mapenzi, na ukiumwa maradhi haya unakuwa huna furaha, na ubaya wake unakuwa hujijui, kwa sababu umekikataa kitu adhim kutoka kwa Mollah wako. Unawadhuru mpaka watoto wako katika maisha yao ya ujanani na uzeeni hawawezi tena na wao kupenda.
sasa yote haya yanatokea wapi?. Sana kwa Wanaume na tatizo kubwa ni woga, itakuwaje watu wakisikia mimi (Mume Maridhia). hapa itabidi nikupeni hadith moja ya Mfalme wa India aliyekua Shujaa, (Very Powerful) siku moja"alibishana na mkewe pale alipomwambia Wanaume wote (Ni Maridhia), Mfalme huyo akiitwa Akbar, hakukubali maneno ya Mkewe akaamua kufanya uchunguzi akamwita mmoja katika washauri wake wakubwa aitwaye abiral, ""Akamwambia jana usiku mimi na mke wangu tulikua tunabishana akanambia wanaume wote ni maridhia"Abiral akamwambia kwanini usimpige kibao, Mfalme Akbar akajibu Mke wangu nampenda itakua ugonvi namie nitakua sina raha, akauliza Akbar kwani wewe Abiral vipi sio Maridhia, Abiral akasema msema ukweli mpenzi wa Mwenye enzi Mungu, hata mimi nyumbani ni Maridhia, basi Mfalme Akbar akamwambia hebu nenda ukafanye uchunguzi katika Mji huu tujue kama yupo mume ambaye sie Maridhia, chukua zawadi ya Farasi wawili ukimkuta mume asiyekua Maridhia basi mzawadie farasi, Akatoka Abiral na Farasi wawili mweusi na mweupe na kupita nchi nzima, kila anomkabili anamwambia hata mie Maridhia, akiwa katika hali ya kuchoka na kukata tamaa akamkuta kipande cha baba wa miraba sita, ananyanyua gari la farasi kwa mkono mmoja, kumbuka siku hizo farasi ndio kama ndege siku hizi, akamfata akamuuliza hebu nambie hivyo wewe una mke, akasema ninaye, mkeo ana kauli yoyote juu yako, akimaanisha kuwa wewe ni Maridhia, akasema wee unanitania, nani atonifanyia upuuzi huo mie, pembeni kuna mwanamke mfupi ikisha mwembamba anapika anasikiliza yale mazungumzo, basi Abiral akamwambia yule mtu kweli wewe umeshinda, sio Maridhia, sasa kuna zawadi Farasi hawa wawili mweusi na mweupe chagua unamtaka yupi?. Kabla ya kuchagua yule Mwanamke akaruka pembeni chagua Mweupe ukichagua mweusi utanitambua""Abiral akamwambia basi hakuna zawadi na wala hakuna Mwanamme asiyekua Maridhia.
Kwa hiyo usione haya kuwa Maridhia, ni kawaida sisi sote Maridhia, ndani ya Maridhia ndiko linapokaa Paenzi. Vipi utalifufua penzi lako lilokufa.(Fanya First aid)unaweza kuliwahi, penzi kama usiku na mchana, linaingia na kutoka, na huruma hivyo hivyo, unachotakiwa tafuta mbolea lima tena(practice love)halafu (True Love)inafatia yenyewe.
Anza kupanga mambo yenu pamoja, anza kumfanya mkeo au mumeo Rafiki, kumbuka mpaka mekutanishwa kwenye Ulimwengu huu basi Mollah wako kakukutanisha na (Your other Half)sasa umekamilika, Anzeni kupanga mambo yenu kwa pamoja, ombaneni msamaha, mpigie simu au mfate kazini akikuuliza umekuja kufanya nini mwambie nimekuja kusema(I love you)hakuna makosa yoyote kufanya hivyo, muachie kibarua kwenye mto kuwa unampenda, acha kwenda nje ili utumie wakati na mkeo, Fanyeni wakati wenu mahsusi wa maongezi bila ya simu au nyimbo, saidianeni kazi za nyumbani, mwanamme usikhisi vibaya kukosha vyombo(Mbona hotel unakosha), nendeni matembezi ya pamoja, pangeni wiki hii zamu yako kunikanda, hapana aibu, peaneni zawadi, kuwa mwepesi mtu akitamka kitu wewe uwe wa mwanzo kumfanyia, nendeni kwa wazee au ndugu wa pande zote mbili kwa pamoja, safirini pamoja, usione haya kununua maua, unajua kwanini maua, kwa sababu Mollah wetu katupa zawadi katika Ulimwengu huu wa maua, litizame ua linavokuja, nani alolipamba, nani alolitia harufu na rangi zake, ukimpelekea mtu zawadi unamwambia, huko yalokotokea maua haya na penzi langu pia limetokea huko nakupa(something of beyond)Ngoja nikukumbushe wapi yalipotokea Maua.
(Al-Aaraf 19)وَيَـٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ فَكُلَا مِنۡ حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَـٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّـٰلِمِينَ .
Ewe Adam Kaa peponi pamoja na mkeo, na kuleni mnapopenda, lakini msiukaribie mti huu msije kuwa miongoni mwa waliodhulumu(Nafsi zao).
Huko ndiko yalipotokea maua, japokua tumefukuzwa huko lakini tumepewa nafasi ya kustarehe hapa Ulimwenguni kama ilivotajwa katika aya ya (24)kwenye sura hiyo hiyo.
Kwa hiyo huna haja ya kudhulumu nafsi yako na yamwenzako, jifanyie (Garden)yako hujakatazwa, Umeambiwa kuleni, pikeni vyakula vizuri, tokeni kama mna uwezo mkale nje, hamna uwezo furahia chakula kilopikwa na mkeo, mpaka utahisi unakula mkono wake kwa utamu, kwani chakula ni (Part of your body), Kumbuka (Body)nafasi yake (Sex) lakini Mapenzi sehemu yake ni kwenye Roho, na chochote chenye kugusa Roho ni (Bliss),basi ghafla utafunikwa na kitu kitokeacho Mbinguni, ghafla utakua umegubikwa na mapenzi, ghafla kuna kitu kitakaa moyoni, ghafla machozi yatakudondoka na ukilijua penzi basi utakua unajua na siri ya maua na harufu inapotokea, utajua nini kitu kiitwacho(Bliss)(Then)yakiondoka huruma inabaki, huruma ikiondoka mapenzi yanarejea, viwili hivyo vinapshana kama usiku na mchana, na hapo utakua na uwezo kuwapenda wanao, kupenda wazee wako, kupenda viumbe vyengine, utaanza kuupenda Ulimwengu na hatimaye kumpenda Mollah wako kwa Baraka alizokupa, utapata fahamu kuwa ipo (Power behind you)ambayo inakumiminia Mapenzi hayo, na wewe huna la kufanya ila Kusema Alhamdulillah. hiyo ndio Afya, hiyo ndio furaha, na huo ndio Uhai, kinyume cha hayo weye ushakufa ungali hai.

No comments:

Post a Comment