Wednesday, May 1, 2024

Innalillah wainna illahi Raajiun

 HAKUNA KAULI YENYE KUCHUKULIWA KWA WEPESI KAMA HII YA INOSEMA SISI NI (AU TUMETOKEA KWA MWENYE ENZI MUNGU NA KWAKE TUNAREJEA, KILA MSEMAJI ANASEMA NI KAMA (LIP SERVICE) IPO MDOMONI LAKINI MOYONI HAINA MAANA YOYOTE ILE, SASA LEO UNAPATA NAFASI YA KUZAMA NA KUTAFITI UBORA WA MBEGU YA MANENO HAYA AMBAYO UKIYAFAHAMU KWA UNDANI NA KUYAJUA MAANA YAKE INAWEZEKANA IKAZAA KITU KIPYA CHENYE MUONO MWENGINE KATIKA NAFSI YAKO NA KIKAKUBADILISHA KABISA UWELEWA WA MAISHA YAKO. KUMBUKA NABII AU MFALME SULEIMAN ALIPOWASIKIA (SISIMIZI)(Ants)WAKIONGEA ALICHEKA , HATA MIMI NILIPOJUA KUWA MTI(TREE)UNA MKE NILISHANGAA, NA ZOTE HIZO NI (REACTION) ZA ROHO, SASA SIJUI WEWE MWENZANGU UKIJIGUNDUA WEWE NI ROHO UTAFANYA NINI?.

LEO TUNAINGIA KWENYE DARSA NDANI YAKE KUNA MAMBO MAWILI LA KWANZA DAWA YA (USINGIZI) NA LA PILI UVUMBUZI WA KUJIJUA KUWA WEWE NI ROHO. AMA KUHUSU DAWA USIJE UKASEMA SIKUPEWA, UKIENDELEA KUUMWA BASI UNAYAPENDA MARADHI, NAAM WACHA TUINGIE KWENYE KAULI YETU KAMA INAVOSEMA KWENYE KICHWA CHA DARSA YENYEWE, ITABIDI MNIWIE RADHI LEO NIANZE NA (HAPPY BIRTHDAY)KWA SABABU MNAPENDA KUSHEHEREKEA JAPO HAMTII NYIMBO LAKINI MNAFURAHI NA KUPONGEZANA, NA UKIAMBIWA KHERI YA SIKU YAKO YA KUZALIWA BASI MOYO UNAJAA FURAHA KWA WINGI. NAPENDA UELEWE MWANAADAMU UNA SIKU ZAKO MBILI MUHIMU MOJA UNASHEHEREKEA NA WATU UNAOWAKUTA DUNIANI NA NYENGINE UNA SHEREKEA NA VIUMBE UTAKAVO VIKUTA (AKHERA) AU UPANDE WA PILI, KWA HIYO NAKUTAKA UFAHAMU WEWE UNA (BIRTHDAY NA DEATH DAY)KWENYE UANDISHI MOJA INAUNGANA NA NYENGINE INATENGANISHA, NINI HABARI YETU SISI KWENYE HIYO YENYE KUTENGANISHA?.

3 comments:

  1. Asalam aleikum warahmatullah wabarakatuh shehe kwanza kwa dhati kabisa ya moyo wangu naomba utukufu wa nuru ya muumba ikifunike napata uelewa mkubwa Sana kupitia darasa zako

    Pili natamani kufaham wakati najituliza kwenye tafakuri au meditation Kuna hali bado sijaielewa hasa maana yake kiroho au kwenye mujtadha wa elimu hizi za kujitafuta kiroho

    Kuna wakati mwili unakuwa Kama wapigwa shoti kubwa Sana kiasi ambacho siwezi vumila hiyo Hali na kutamani kurudi kwenye Hali ya kawaida naomba unipe Siri ya Jambo hili kiundani

    ReplyDelete
  2. By the way tumepoteana pia kwa MDA kwa Sabab ya simu yangu kushindwa kusapot mfumo wa watsap niombee Dua nimefurahi Sana leo kukusoma Tena

    ReplyDelete
  3. Ninakualika kutembelea blogu yangu! 🌿✨
    Katika https://herbalteaman.blogspot.com/ ninashiriki maudhui yanayohusiana na dunia ya mimea, chai za mitishamba na mengine mengi.
    Ikiwa unapenda kugundua mapishi, vidokezo na mambo ya kuvutia kuhusu asili, itakuwa furaha kubwa kukukaribisha huko!

    Ninakungoja!

    ReplyDelete