Wednesday, June 20, 2012

SIRI YA MAUTI-(VIPI UNAKUFA)PART 1

ASALAAM-ALEIKUM. Hakuna kitu anacho chukia mwanaadamu na kukiogopa kama mauti au (Kifo)ndio maana mada kama hizi hazipendwi kuzungumzwa kabisa, hakuna anopendelea kuizungumza kwa undani na ufanisi japo kuwa tukio hili sote litatukabili au kuna wenzetu lishawakabili lakini tunaendelea kujifanya kama halipo au sisi halitotugusa.Ewe mwanaadamu hivo ushapata kujiuliza nini kitatokea Mauti yatakapo kuhudhuria? Wanaadamu jambo hili linavyowatisha ndio utaona hata makaburi basi yamewekwa nje ya mji sababu watu wapate kusahau tukio hili la mauti.Watu wanaweza kupata nafasi ya kuizungumzia Roho lakini hawataki kabisa kuzungumza kutoka kwa Roho, Jee basi inakuwaje pale Malaika wamehudhuria kuja kumtoa Roho Mwanaadamu, "Ewe jumba la makosa"nakuomba piga moyo konde usafiri na mimi katika maudhui hii ili upate kujua japo kwa ufupi nini hasa kinakufika wakati Roho inapotolewa kutoka katika mwili wako.Hebu acha kuizungumzia siku ya kuzaliwa peke yake pata anagalau kidogo mvinyo wa Mauti ujue ladha yake inakuaje na nini kinatokea wakati huo. Sikusema mimi maneno haya amesema yule alotumwa kwa haki kutuletea ujumbe huu, sasa yeye kasema nini? Anasimulia "(Abdulla Ibn Umar r.a Bwana Mtume s.a.w kasema)"Moyo unaingiwa na kutu kama vile chuma kinavoingiwa na kutu kikiingiwa na maji,Alipoulizwa nini tufanye ewe Bwana Mtume s.a.w ili tuusafishe,"akasema fanyeni jitihada kubwa za kukumbuka Mauti na kusoma Quraan". Tumo katika kuyafata maagizo ya Bwana Mtume s.a.w tumeingia katika bahari hii ya Mauti ili iwe mazingatio ya ukumbusho kwetu sote. Sasa kwanini jambo hili likawa linatuhuzunisha na kutudhoofisha, kipi hasa tunachokipoteza katika haya mauti hata ikawa hatutaki kusikia habari hii, mbona chungu sana kadhia hii, inakuaje inatisha hivi ikawa mtu akitajiwa hana raha tena ya ulimwengu huu, Tupia macho aya ya 1-2 sura (MULK-Tabarak)تَبَـٰرَكَ ٱلَّذِى بِيَدِهِ ٱلۡمُلۡكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَىۡءٍ۬ قَدِيرٌ (١) ٱلَّذِى خَلَقَ ٱلۡمَوۡتَ وَٱلۡحَيَوٰةَ لِيَبۡلُوَكُمۡ أَيُّكُمۡ أَحۡسَنُ عَمَلاً۬‌ۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡغَفُورُ (٢) "Ametukuka yule ambaye katika mkono(uweza wake)upo ufalme na ni mueza wa kila kitu" Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukufanyieni mtihani (nani)atakaye fanya mema,na yeye ni mwenye nguvu na mwenye kusamehe.Ameumba mauti na uhai kwanini yameanzwa kutajwa mauti mwanzo,ukenda katika elimu ya Tawhid ndio utagundua asili yetu lazima tupitie katika mauti ndio tuzaliwe,tizama mfano wa mbengu lazima ifukiwe ardhini halafu ndio itoe mti au ichipue kuwa mmea n.k, kwa hiyo ukiangalia kwa njia ya Tawhid Mauti na Uhai ni kitu kimoja ambacho kinapita katika sehemu inayoitwa maisha, ndio maana aya ikasema tumeumba mauti na uhai ili tukufanyieni mtihani,Kutokana na sababu hii ya kukikosa kitu hichi kinachoitwa maisha ndio Binaadamu akawa anajuta,tunalia,tunahuzunika kuikosa zawadi hii njema ya Mollah wetu alotupa yakuweza kuishi, ukipewa habari tu kuwa una maradhi na yanaweza kusababisha mauti, basi jitizame vita utakayopigana hapo madawa ya kila aina dua za ajabu ili mauti yasikufike. Mollah wetu katupangia njia ya kuja katika ulimwengu huu pale wanapokutana waja wawili katika tendo la ndoa, ndani ya mkutano huu imewekwa njia ya uhai kuanza safari hii ya kuonja ladha ya Maisha. Halafu tumewekewa njia nyengine ya kuondka katika ulimwengu huu na kuicha ladha ya maisha nayo ni hichi kifo, Mwanaadamu kama ulivokuja mwanzo peke yako na kwenye njia hii ya mauti unaondoka peke yako, lakini kuna tafauti ulipoanza safari hii mwanzo ulikua huna fahamu na sasa unaondoka na fahamu zako kamili, ulikuja katika ulimwengu huu mweupe huna doa, huelewi chochote,lakini leo unaondoka umekua mjuzi wa kila kitu, basi jee katika hayo ulosomea kwenye hii University ya maisha yapo uliyoyafanyia kazi za wema, jee ule mtihani umefaulu vizuri, Na kama umefeli ulifanya jitihada za kufanya marekebisho. Basi leo unaaga dunia unayaacha maisha tunakufungulia daftari yako ili tupate kukujulisha uliyoyatenda katika ufalme huu wa Mollah wako wa haya maisha. Mauti yanaendelea kuwa maajabu juu yetu, yanaendelea kututisha kutokana hatuko tayari kuyakabili kama walivoyakabili watendao mema. Na sababu kubwa ni ile ya kusahau kama sisi katika ulimwengu ni wageni na kuna siku tutarejea tulikotoka, sasa nini tunafanya, tunakuwa wabinafsi,mtu pengine anaabudu mali yake,au jumba lake,au mapenzi yote kayamimina kwa familia yake na kamsahau Mollah wake,hakumbuki kabisa yale maneno aloambiwa haitokufaa leo mali wala watoto wako. Mauti yanatutisha sababu kwa mara ya mwanzo inakukutanisha na hicho kitu kiitwacho Roho au kwa usemi mwengine (Your true self)Mauti yanakufanya upotee kabisa katika ulimwengu huu ndio maana khofu inakua kubwa sana, halafu napenda uwe na yakini katika safari hii ya mauti hakuna chochote kitacho kwenda na wewe isipokua amali zako, na pia jua kwa ukamilifu safari hii ni peke yako kama ulivokuja mara ya mwanzo huna jina huna nguo na mara hii unaondoka peke yako, na lengine la zaidi ni ile siri uliyoifutika ya kujiuliza hivo nitakua hai mie baada ya mauti yangu, jee vipi yale mambo ninayoambiwa kweli yapo huko niendako,basi leo ni siku ya kukutanisha na kile kilochotokea mbinguni kinachoishi ndani ya mwili wako, wengine wanapata bahati kukishuhudia wakati wapo hai kama vile ukiamka ndani ya ndoto ukawa unashuhudia kisa kinachotokea katika ndoto hiyo, ukipata nafasi ukatanabahi kujua na kuiona ndoto yako basi huyo aloona inabidi ajiulize nani huyu mwenye kushuhudia. Ewe mwenye kuamini kwamba Mauti nikumalizika kwa kila kitu basi acha tukujulishe yakua kila chenye mwanzo elewa kina mwisho na kila chenye mwisho basi kina mwanzo wake, Jee imekufikia habari hii ya hijja yako ya akhera, basi kama huna habari au unapuuza hebu tega macho katika sehemu ya pili ya maudhui hii ujue nini kinatokea wakati Malaika wamehudhuria kuja kukuchukua, usije ukaogopa siku hii itakufika kama sio leo pengine kesho au umebakisha mwezi au mwaka lakini lazima utakutana na kadhia hii nzito isoepukika hivi karibuni.SASA VIPI MWANAADAMU UNATOLEWA ROHO,ENDELEA SEHEMU YA PILI IKIWA UNA MOYO WA KISHUPAVU. A.BAJA

No comments:

Post a Comment