Sunday, November 24, 2013

MAJINA YA MWENYE ENZI MUNGU(RAZAQ)PART 1

Asalaam Aleiykum,

Mwenye Kuruzuku(Mtoa Riziki) Wanaadamu tumo katika kiza kikubwa hata akitokea Mtu akakushika mkono na kukufahamisha twende upande huu kuna muangaza utatoka kwenye giza basi hutokubali kumfata, Mwenzangu wee mimi nimeshaona alama ya taa waweza kuipata njia na ukatoka kizani basi utatia wasiwasi na hutokubali kumfata abadan. Hiyo ndio desturi ya Imani dhaifu inavokuamrisha ubakie kwenye kiza, Imani hiyo inatufahamisha kuwa kipato kinapatikana kutokana na nguvu zako mwenyewe.
Napenda uelewe hakuna nguvu zako mwenyewe ila yupo alokupangia ikisha akakuonesha na njia za kupita, halafu akakufundisha mipango ya kufanya mpaka ukaipata hiyo (Riziki).
Yeye ndiye ambaye mwenye kusababisha kila kitu katika Ardhi hii, basi kwanza "Na atizame mwanaadamu chakula chake"Abasa 24"فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَـٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِ"
Ukitizama chakula kinaweza kukupeleka safari kubwa ya kufika kwenye ukamilifu wa Imani yako katika jambo la kumjua(Razaq) Kakuwekeeni kila kitu kuanzia chakula chenu mpaka Mali ghafi zenu mnazipata kutoka katika Ardhi yake, kama Petrol,Dhahabu,Shaba,Vyuma,Almasi Maji na kila kinachohitajika katika Uchumi wenu, sasa Jiulize nani Tajiri, Nani mwenye kutoa, Nani anopanga huyu apate kile na huyu apate hiki, ukimjua Mwenye kupanga hayo basi Yeye ndiye (Razaq) Ambaye baada ya hapo akawa Mwenye kuwaonyesha waja wake njia za kuvipata vitu hivyo, Huyu akampa elimu na kumpangia wewe itakua kazi yako Ofisini, wewe utakua mfanya biashara, akawapa maguvu nyinyi mtakua mnatumika kwa njia nyengine kuipata Riziki yenu.
Ikisha baada ya yote hayo akatoa mtihani kuwaangalia waja wake alowapa kwa radhi na mapenzi yake kama jee akiwataka watoe vile alivowapa watamtii, Jee watafanya hivyo kwa ajili ya Imani ya kumpenda Mollah wao na kuvitoa kwa mapenzi? lakini wapi hapo ndipo anasahaulika kabisa Mwenye kuruzuku na mnageuka kuwa wenye"

وَتُحِبُّونَ ٱلۡمَالَ حُبًّ۬ا جَمًّ۬ا
(Kuipenda)Mnapenda Mali pendo la kupita kiasi.
Unasema kabisa hapa hakitoki kitu, unapata maradhi ukimuona maskini unaanza kupanga uongo wa kujikinga kabla hata hujakutana nae,(Kumbe maskini mkipishana anakutolea salamu tu) Na akitokea Mtu kukumbusha jamani mnatakiwa mtowe mtaanza kumwita husda huyoo wa mali za watu, Na kuna wengi wanasahau kama katika maombi yao chungu nzima kabla ya kupewa hiyo Mali walikua kwenye Sijda au sehemu ya siri katikati ya usiku wanaomba na kusema," وَمِنۡہُم مَّنۡ عَـٰهَدَ ٱللَّهَ لَٮِٕنۡ ءَاتَٮٰنَا مِن فَضۡلِهِۦ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ"(Tawba 75)
Na miongoni mwao wako waliomuahidi Mwenye enzi Mungu kuwa,(Kama)akitupa katika fadhila zake tutatoa Sadaka na tutakuwa miongoni mwa wanaotenda mema.
Nenda ukaombe sasa hivi uone cha mtemakuni, Pengine utamkuta mtu kaweka (Bodyguard) hao kwa madhumuni ya kuwazuia maskini tu wasimkurubie, Basi kumbuka huyo ndio (Razaq)mwenye kumiliki Uchumi wote katika Ulimwengu huu.
Endelea part 2


MAJINA YA MWENYE ENZI MUNGU(RAZAQ)PART 2

Asalaam Aleiykum,

Yeye ndiye ambaye akileta msukosuko wa Mvua au Kimbunga Biashara zote husimama, akikutieni mtihani wa vita nchi nzima inafilisika, akikuondosheeni amani kidogo tu Petrol inapanda, mara haiwezi kusafirishwa, vyakula bei juu hichi hakendi kile hakirudi sasa jiulize nani Mwenye kuruzuku.
Ukiyajua hayo basi utagundua hata huko kupewa kwako Mali ni mwenenedo wa kuruzukiwa, Hiyo njia ya kutafuta Riziki pia ni kuruzukiwa, huo Uhai pia ni kuruzukiwa, kakutia yeye fahamu na kukuonesha mipango ya kufanya mpaka ukaweza kuipata hiyo Mali ulonayo. Yeye ndiye anayempa anayemtaka na kumnyima anayemtaka, Na katika viwili hivyo kuna sababu ya undani ikiwa utakua mjuzi wa kutizama, Kwa hiyo ikiwa ushahangaika sana na unaona Utajiri haupatikani basi pumzika jua Mwenyewe mwenye Kuruzuku hataki utajirike, Na ana sababu za kufanya hivyo na hiyo pia ni baraka itokayo kwake ili utumikie mambo mengine, lakini wapi wewe umeshikilia lazima upate utajiri na hayo ndio makosa yako.
Basi litumie Jina hili la Razaq kwa ajili ya kumuomba Mollah wako, Na usije kudhani mapesa yataporomoka kutoka mbinguni ila atakufungulia njia ili uweze kupata hiyo Riziki, Na hata ukinyimwa furahi kwani kuna mengi Mollah wako anayo kuruzuku hayana hesabu, Na kama hujapewa kabisa Furahi jua Mollah wako kakusikia na anakupenda na uko karibu nae na kila ukimuomba hakupi,basi kwa kutamka jina hili litakujulisha kitu kwamba Mollah kakupa mengine yenye thamani kuliko huo utajiri, Na kwa kukunyima huo utajiri anakupenda na kukuepusha na shari yake,
Tunakuomba Mollah, Yaa Razaq, tupe ulotupangia ya kheri na utujaalie kuridhika.

Sunday, November 17, 2013

MAJINA YA MWENYE ENZI MUNGU(HAAFIZ)PART 1

Asalaam Aleiykum,

(Mwenye Kuhifadhi) Vipi utamjua anayehifadhi, Itabidi kwanza uchunguze mwenendo mzima wa kuwepo kwako kwenye Ulimwengu huu, Nani kakuumba na imekuaje akakuleta kwenye dunia hii na kukupa zawadi ya Uhai, Ukisha kulijua hilo ndipo jiulize vipi atashindwa kukuhifadhi.
Halafu fanya maulizo tena kwanini unafikia uamuzi wa kwenda kwa Mganga kutafuta hifadhi, lazima upate Hirizi au akupe kichupa ukaweke ndani ya nyumba au kazini eti iwe Hifadhi yako, ukisha elewa kama huo ni upuuzi mtupu basi achana na kuamini kuwa yupo mwengine atakae kuhifadhi zaidi ya Mollah wako, na ukikubali kuwa Mollah wako pekee ndie mwenye kukuhifadhi basi hiyo ndio Imani na wewe Muumin wa kweli.
Lakini najua tabia za Binaadamu vigumu kuacha Imani walizo zizoea, vipi leo utakubali kinga isiyokua ya Hirizi la Shaba au Pete la Fedha, au kikaratasi uweke chini ya mto, Basi kwa kukidhi haja yako hiyo Mimi leo nitakupa Hirizi langu ambalo hutakiwi kulivaa shingoni, Hirizi hii unatakiwa uivae Akilini, Na ukisha kuivaa utakua huna wasiwasi na chochote, woga wote utaondoka, Hirizi hii itakufahamisha kumbe kwenye Ulimwengu huu hakuna cha kukudhuru, na utajua kwamba mimi nimehifadhiwa kila upande na yoyote yule atotaka kunidhuru lazima apate idhini au Amri ya yule Mwenye kunihifadhi.
Sina haja mimi ya kulindwa na fulani wala fulani, Hakika hifadhi ya (Haafiz)imeenea kila sehemu na kila pahala Hifadhi hii inaendelea kuwapo, Yeye huyo ndio Mwenye kuhifadhi vidogo na hivyo vikubwa vyenye maguvu, Na hata kama haja kuhifadhi ukahisi mbona yamenikuta basi elewa kukufika huko kwa hilo jambo ni kwa sababu maalumu, Na kutokana na yeye kuruhusu hilo jambo likufike, Na kila likufikalo elewa ni kwa Amri yake yeye, Na lile lenye kukuepuka basi pia kaa ukijua yeye ni (Haafiz).
Kamata Hirizi hii ili uiweke moyoni mwako, Ikisha ingia sawasawa utajua kwa yakini liloandikwa likukute litakukuta hali ya kuwa hakuna mlinzi wa kukuhifahi.
Endelea part 2

MAJINA YA MWENYE ENZI MUNGU(HAAFIZ)PART 2

Asalaam Aleiykum,

Ipokee Hirizi yenyewe ikuvae kwenye mawazo yako uwe unaikumbuka mara kwa mara, Ishibishe ndani ya Akili itakupelekea Aya hii ya ayat (Kursiyu)kumjua nani huyo (Haafiz)kwa upeo mwengine kabisa, itakapo kuingia aya hii basi utakua hutaki tena Mlinzi yoyote isipokua Yeye Yaa (Haafiz).
Nisiseme hivi ukadhani kuwa kumbe kama ni hivyo naweza kulala na begi la Pesa mlango wazi kwenye jiji la dar es salaam yatakayo kukuta mimi simo, kuna kisa katika Injili(Biblia)kinafaa nikitaje ili upate ufahamu mzuri, Nabii Issa a.s (Jesus)"Alichukuliwa na Shetani kwa ajili ya majaribio(Mtihani)kwa muda wa siku arobaini, baada ya kupasi majaribio yote Shetani akamchukua katika jaribio la mwisho, Akampeleka kwenye Mlima mrefu, ikisha akamwambia kama uyasemayo ni kweli basi chupa nikuone, chupa nithibitishe, Nabii Issa a.s(Yesu)akamjibu (Baba Hachezewi),"Kwa hiyo na wewe ukitaka kufanya majaribio ya kulala na godoro lako la pesa kumbuka (Baba Hachezewi).
Sasa tunaingia kwenye aya yenyewe tuichungulie (Sifat ul Haafiz)Baqara 255
ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَىُّ ٱلۡقَيُّومُ‌ۚ 
"Mwenye Enzi Mungu ni mmoja hakuna Mollah(Mwengine)na ndiye Mwenye Uhai wa Maisha na Mwenye kusimamia kila jambo"
Wapi unataka hifadhi kwengine hali ushajua Yeye ndie aliyekupa Uhai na Yeye ndie wa Kudumu, hata hao wakikudhur elewa yeye atakupa Uhai tena, ondoa wasiwasi".
 لَا تَأۡخُذُهُ ۥ سِنَةٌ۬ وَلَا نَوۡمٌ۬‌ۚ
"Hakumshiki kusinzia (Kusahau)wala kulala"
Vipi atashindwa kukuhifadhi hali yakua wakati wote ni mwenye kuwaangalia na kuwajua viumbe vyake.
لَّهُ ۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَمَا فِى ٱلۡأَرۡضِ‌ۗ 
Ni vyake (Vyote) viliyomo Mbinguni na vilivyomo katika Ardhi.
Sasa itatokeaje kuwa awe Mlinzi wako asiyekua Yeye Mollah wako, ikiwa kavimiliki vyote vya mbinguni na ardhini atashindwa kukuhifadhi wewe.
مَن ذَا ٱلَّذِى يَشۡفَعُ عِندَهُ ۥۤ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦ‌ۚ
"Nani huyo awezaye kuombea mbele yake(Mollah)Bila ya Idhini yake". Hakuna yoyote anayeweza kukudhuru wala ukidhurika hakuna awezaye kukuponya isipokua lazima ipatikane Idhini yake Yeye aliye (Hafiz)Bure kuhangaika na mizimu, Upuuzi mtupu eti mpaka utambike, mizimu imehamaki, Mganga akichukia utaangamia, yote hayo porojo, Jua wewe Umehifadhiwa Na Yeye Mollah wako alokuleta katika Ulimwengu huu, na akitaka jambo likufike litakufika hakuna wa kuzuia, Na akitaka upone utapona bila ya Mganga, hujiulizi mbona Ndege na wanyama wanapona bila ya (Doctor).
يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡ‌ۖ 
"Anayajua yaliyo Mbele yao (Viumbe)na Yaliyo(Nyuma)yao"
Mwenye kuyajua ya mbeleni kabla ya kutokea hayo msoyajua, Na pia anayajua yale mlokwisha kuyasahau ambayo yashatokea vipi leo ashindwe kukuhifadhi."
وَلَا يُحِيطُونَ بِشَىۡءٍ۬ مِّنۡ عِلۡمِهِۦۤ إِلَّا بِمَا شَآءَ‌ۚ
"Na wala(Viumbe)hawalijui lolote katika Ilimu yake(Mwenye enzi Mungu)ila kwa alipendalo(Analolitaka)"
Hakuna kupiga Bao(Ramli)wala kujua utibabu huu na ule, au chochote katika Ulimwengu huu mpaka ujulishwe kutoka kwake Mwenyewe mwenye kuhifadhi.
وَسِعَ كُرۡسِيُّهُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ‌ۖ وَلَا يَـُٔودُهُ ۥ حِفۡظُهُمَا‌ۚ وَهُوَ ٱلۡعَلِىُّ ٱلۡعَظِيمُ
"Enzi yake Imeenea Mbingu na Ardhi, wala hakumshindi kuvilinda, Na yeye Ndiye aliye juu na ndiye aliye Mkuu"
Huo ndio Ufalme wa Mwenye enzi Mungu, umekimiliki kila kitu, Na hiyo ndio hifadhi unotakiwa kuijua, Na hivi ndivo unavotakiwa fikra hii ikuingie katika mawazo yako yende (deep)kuwa kila ukiona Binaadamu, Vinyama, Miti, Mbingu,Nyota,Mwezi,Jua Uwe unakumbuka kuwa vyote hivi ni Enzi ya Mwenye enzi Mungu, Na kwamba yeye ndiye aliyeviumba na yeye ndiye Mwangalizi wake, Na pia ndiye (Hafiz)Mwenye kuvihifadhi, Aliye juu ya kila alichokiumba na ni Mkuu wa kila Jambo, basi litumie Jina hili la (Haafiz)uipate kinga itokayo kwa Mollah wako.






Sunday, November 10, 2013

MAJINA YA MWENYE ENZI MUNGU (ALIIM) PART 1

Asalaam Aleiykum,

Hakika yeye ni Mwenye kujua kila kitu kwenye Ulimwengu huu,(Aliim) Nini Kujua? Kujua ni Elimu yenye kuhusiana na (Roho), Ndio maana utaona kujua siku zote kunatokea ndani na wala sio nje.
Na mifano ipo chungu nzima ikiwa unataka kuelewa nini kujua, basi hebu jiulize inakua vipi mtoto akizaliwa anajua kutafuta ziwa la mama na kulinyonya, nini kinachomjulisha sasa aanze kutambaa,(Lazima kuna kitu kinamjulisha), Nani anomjulisha mnyama akizaliwa tu anze kusimama na kutembea,,Nani Mwenye kukujulisha wewe sasa hivi uhai na mzima, Nani Mwenye kukujulisha wakati Umelala amka sasa ushamaliza usingizi, Yeye huyo ndie ajuae fulani siku gani ataumwa na lini atakufa, Nani atazaliwa na nchi gani atakayozaliwa, Yeye huyo Mtukufu ndie aliye kienea kila kitu kwa Ujuzi(Muhittun)Kila kitu kimo katika Ufalme wake wa Kujua.
Yeye ambaye kakipanga kila kitu kufata amri za ujuzi wake bila ya upinzani wowote, Na akaufunza ujuzi huo kwa kila kilicho Hai chenye kuishi. Kwanini nikaita ujuzi na nisiite elimu, Sababu elimu ina kikomo lakini ujuzi hauna kikomo, elimu ukijua kidogo wenzio wanajua zaidi, lakini ujuzi au kujua hakuna tafauti wewe unajua hili ua na mwenzio analijua hivyo hivyo hili ua, hakuna tafauti, kujua kama kuona au kusikia hakuna mwenye kuzidi, ukisha kujua ndio ushajua hakuna mbadala, kujua kunatokana na hiyo elimu ya (Ghayib)au siri kama alivosema Mwenye huo Ufalme wa kujua kwenye sura ya (Hashir 22)
هُوَ ٱللَّهُ ٱلَّذِى لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ‌ۖ عَـٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ‌ۖ
"Yeye ndiye Mwenye enzi Mungu ambaye, Anayajua yalofichikana na yaliyo dhahiri"
Mafundisho yote yanatokea kwake kwenye enzi ya siri na kufundishwa viumbe vyote, Na kila kiumbe kimefunikwa na ujuzi huu usiokua na mwisho, Jiulize swali la rahisi kwanini kila kiumbe kina dasturi ya kufanya maskani ya kukaa, Nani alomfundisha Ndege kujenga Nyumba yake na kutafuta Riziki, Na ana juaje wapi ataipata. Yeye huyo ndie Mollah Mjuzi mwenye kumfundisha huo ujuzi wake kila kiumbe, Akateremshiwa huyu akawa mwenye kuvumbua kutengeneza Ndege, Na mwengine akaunda Meli, Yule akavumbua kile na huyu akavumbua hichi, Na wote ukiwauliza wapi mumepata (Idea)hizi, imekuaje mpaka mkajua, ilikua vipi hata ukatengeneza gari, atakujibu mimi imenijia tu katika Akili yangu, Ikisha nikaandika kwenye karatasi ndio nikaanza kuifanayia kazi.
Nini Elimu?
Endelea part 2

MAJINA YA MWENYE ENZI MUNGU (ALIIM) PART 2

Asalaam Aleiykum,

Naam nini  Elimu? Elimu ni (Gathering of Information) unakusanya huku na kule ikisha una hifadhi kichwani mwako, Na mwanzo wake imetokea kwenye hiyo (Source) na kutiwa katika Roho yako, Halafu tena wewe mwenyewe unafanya (Transfer)  kuipeleka kwenye akili, Na hapo ndio unaanza Ku(Shared) na watu wengine.
Lakini Ujuzi unaweza kubakia peke yako kama hutakai kuugeuza elimu, ikawa unajua mambo hayo ya siri pekee. Na anokupa Ukarim huo wa kujua hakuna Mwengine isipokua Yeye Mwenyewe (Yaa Aliim)Mjuzi wa kila kitu. Yeye ndie anaejua kila kitu kitokeacho Ardhini na Mbinguni, Kifanyike Baharini au Nchi kavu hakitokei bila ya Idhini yake au yeye kukijua.
Basi ikiwa hali yenyewe ndio iko hivyo ajijue kiumbe huko kufichaficha kwake na kufanya siri anajidanganya mwenyewe kwa mambo anayaofanya hali ya kuwa anajua fika Mollah wake anafahamu kila kitu.
Basi Niombeni kwa ajili ya Jina hili la (Aliim) ili mpate ujuzi zaidi wa kumfahamu Mollah wenu na Ulimwengu huu mnaoishi kwa Jumla, Ikiwa kwa Ukarimu wake kakufunzeni bila ya kumuomba, Nini Habari yenu nyinyi kama mtamuomba kwa dhati ya nafsi zenu, Basi kuanzia leo ikiwa mwenye kutaka kujua jambo la kheri utumie jina hili la Yaa Aliim kwa idadi nyingi kabisa huku unataja hilo kusudio lake uone faida zake. Na ulikumbuke jina hili kabla ya kulala, kuwa ukilala na jina hili, kuna mambo mawili yatatokezea ima utaamka ushapata jawabu au ufumbuzi, au utapewa habari kwa njia ya ndoto, Tunamuomba Mollah wetu atuzidishie ujuzi wa kumjua yeye na kumuabudu pasi na makosa, na huku tukitii amri zake.

Sunday, November 3, 2013

MAJINA YA MWENYE ENZI MUNGU(BASIRA) PART 1

Asalaam Aleiykum,

(Basiran) Mwenye kuona, Kabla ya kuendelea na jina hili wacha tujue tafauti ya kuona na kutizama, kutizama ni kitendo cha kuwepo mbali ukawa unaangalia, Kuona ni kitendo cha kuwepo karibu na ukawa unashuhudia, Na shahada ni jambo la yakini halina wasiwasi, kutizama inaweza kuwa yule ndie au siye huna uhakika, lakini kuona unasema moja kwa moja huyu ndie, hiyo ndio tafauti yake, Sasa hii sifa ya kuona imekusanya kila jambo linaonekana (in detail)kuona huku hakuna pazia wala kikomo, tunapo zungumza kuona huku si kule kuona kwa kawaida unavofahamu mimi na wewe, kuona huku kwenye kutajawa hapa kuna muhusu yule ambaye amejaalia huku kuona, kwa hiyo isije kukutuma akili yako ukadhani anaona kama unavoona wewe, hizo zako ni (tashbiha)umeletewa ili upate kutumia hilo jina la kuona kwa ajili ya maombi yako.
Usije ukazuka nakuanza kufikiri anaona kwa macho gani, usifananishe kabisa na kitu chochote, (Basira)Mwenye kuona, Kumekua kuona huko ni alama ya kuwepo na kukienea kila kitu, huna wakati au sehemu ikawa huonekani, ikiwa upo peke yako yeye wapili wako(Na kuna Method ya kulijua hilo ukifikia upeo fulani wa kufahamu utafahamishwa)Yeye ni Mwenye kukiona kila kila kitu kwa undani wake, hakuna chochote kiwezacho kuepuka kutoonekana na Mollah wako.
Yeye ndiye aliyekupa Roho na anakuona ndani ya hiyo Roho, Vipi linakua tukio lenyewe, Napenda ieleweke kuwa kitendo cha kuona ni (Temprory)katika matumizi ya macho, lakini ni cha kuendelea kwenye matumizi ya kiroho ndio maana ukilala unaendelea kuona ndoto zako, kwa hiyo inayoona ni hiyo Roho. Kwa hiyo hilo tendo limeitwa Jaala kwa sababu mara nyingi unaondoshewa hata katika hiyo Roho huoni kitu(Ndio unaamka na kusema leo nimelala fofofo, Kwa hiyo yeye ni mwenye kumiliki huko kuona, ndio maana akakwambia kwenye surat(Mulk 3-4)
مَّا تَرَىٰ فِى خَلۡقِ ٱلرَّحۡمَـٰنِ مِن تَفَـٰوُتٍ۬‌ۖ فَٱرۡجِعِ ٱلۡبَصَرَ هَلۡ تَرَىٰ مِن فُطُورٍ۬ 
"Tizama katika Uumbaji wa Rahmani huoni tafauti (Yoyote)Rejesha macho (Yako utizame)jee unaona kosa"
ثُمَّ ٱرۡجِعِ ٱلۡبَصَرَ كَرَّتَيۡنِ يَنقَلِبۡ إِلَيۡكَ ٱلۡبَصَرُ خَاسِئً۬ا وَهُوَ حَسِيرٌ۬ 
"Tena rejesha macho(yako)mara nyingi zaidi, jicho lako litarudi hali ya kuwa limehasirika na umechoka"
Tizama, sababu Mbinguni  mbali, kwa hiyo nyanyua jicho utizame kama utaona tafauti yoyote, halafu ukaambiwa tazama tena na hali utarejesha jicho lako ukiwa hasarani, kwa sababu huko kuona kakupa yeye Mwenyewe uwezo huo , Na hizo mbingu saba kazitengeneza yeye, Basi kama unazitafuta.Endelea Part 2


MAJINA YA MWENYE ENZI MUNGU(BASIRA)PART 2

Asalaam Aleiykum,

Kwanini kila ukitizama Mbinguni huoni tafauti na wala hizo Mbingu saba , Kwa sababu kuona kwetu viumbe kuna daraja au kikomo, ndio maana ndege ana kiasi chake, kuku ana kiasi chake, samaki ana upeo wake wa kuona, na yote hayo yamemilikiwa na mwenyewe mwenye huo Ufalme wa kuona, Lakini wewe Mwanaadamu kiumbe chake alokufanya Khalifa kwenye Ulimwengu huu kakupa zawadi ya kutizama isiyokua na kikomo.
Na ndio maana kwenye hiyo aya imetajwa tizama na wala sio angalia, Basi kafanye majaribio hayo ya kutizama ukimaliza kusoma, Nenda Nje angalia Mbingu au upande wowote usokua na kizuizi cha Miti au Majumba utajua siri hiyo ya upeo wako usokua na mwisho.
Picha au (Telescope)zinachukua (Still Image) kutokana na mafundisho yako, wewe unaona na kuweka kumbukumbu kutokana na uwezo na mafundisho ya Mollah wako, Yeye pekee ndio Mwenye huo uwezo na Ufalme wa Kuona, Na katika kuona huku kupo kwa aina mbili unaweza kuona Nje na ukipata mafundisho ya kuondoa pazia basi utaona na ndani(au mambo ya siri),  hivi sasa unaona lakini bado pazia limekufunika, labda mpaka siku ya kufa kwako ndio huondoshwa hilo pazia ukawa unaona pasi shaka na hicho unacho kiona, Kwa hiyo fanya hima katika kuona kwako ili utumie jina hili la Basira likuondoshee pazia na uyaone mambo makubwa makubwa yaliyo mazuri katika Ulimwengu huu.