Sunday, November 17, 2013

MAJINA YA MWENYE ENZI MUNGU(HAAFIZ)PART 1

Asalaam Aleiykum,

(Mwenye Kuhifadhi) Vipi utamjua anayehifadhi, Itabidi kwanza uchunguze mwenendo mzima wa kuwepo kwako kwenye Ulimwengu huu, Nani kakuumba na imekuaje akakuleta kwenye dunia hii na kukupa zawadi ya Uhai, Ukisha kulijua hilo ndipo jiulize vipi atashindwa kukuhifadhi.
Halafu fanya maulizo tena kwanini unafikia uamuzi wa kwenda kwa Mganga kutafuta hifadhi, lazima upate Hirizi au akupe kichupa ukaweke ndani ya nyumba au kazini eti iwe Hifadhi yako, ukisha elewa kama huo ni upuuzi mtupu basi achana na kuamini kuwa yupo mwengine atakae kuhifadhi zaidi ya Mollah wako, na ukikubali kuwa Mollah wako pekee ndie mwenye kukuhifadhi basi hiyo ndio Imani na wewe Muumin wa kweli.
Lakini najua tabia za Binaadamu vigumu kuacha Imani walizo zizoea, vipi leo utakubali kinga isiyokua ya Hirizi la Shaba au Pete la Fedha, au kikaratasi uweke chini ya mto, Basi kwa kukidhi haja yako hiyo Mimi leo nitakupa Hirizi langu ambalo hutakiwi kulivaa shingoni, Hirizi hii unatakiwa uivae Akilini, Na ukisha kuivaa utakua huna wasiwasi na chochote, woga wote utaondoka, Hirizi hii itakufahamisha kumbe kwenye Ulimwengu huu hakuna cha kukudhuru, na utajua kwamba mimi nimehifadhiwa kila upande na yoyote yule atotaka kunidhuru lazima apate idhini au Amri ya yule Mwenye kunihifadhi.
Sina haja mimi ya kulindwa na fulani wala fulani, Hakika hifadhi ya (Haafiz)imeenea kila sehemu na kila pahala Hifadhi hii inaendelea kuwapo, Yeye huyo ndio Mwenye kuhifadhi vidogo na hivyo vikubwa vyenye maguvu, Na hata kama haja kuhifadhi ukahisi mbona yamenikuta basi elewa kukufika huko kwa hilo jambo ni kwa sababu maalumu, Na kutokana na yeye kuruhusu hilo jambo likufike, Na kila likufikalo elewa ni kwa Amri yake yeye, Na lile lenye kukuepuka basi pia kaa ukijua yeye ni (Haafiz).
Kamata Hirizi hii ili uiweke moyoni mwako, Ikisha ingia sawasawa utajua kwa yakini liloandikwa likukute litakukuta hali ya kuwa hakuna mlinzi wa kukuhifahi.
Endelea part 2

No comments:

Post a Comment