Sunday, November 17, 2013

MAJINA YA MWENYE ENZI MUNGU(HAAFIZ)PART 2

Asalaam Aleiykum,

Ipokee Hirizi yenyewe ikuvae kwenye mawazo yako uwe unaikumbuka mara kwa mara, Ishibishe ndani ya Akili itakupelekea Aya hii ya ayat (Kursiyu)kumjua nani huyo (Haafiz)kwa upeo mwengine kabisa, itakapo kuingia aya hii basi utakua hutaki tena Mlinzi yoyote isipokua Yeye Yaa (Haafiz).
Nisiseme hivi ukadhani kuwa kumbe kama ni hivyo naweza kulala na begi la Pesa mlango wazi kwenye jiji la dar es salaam yatakayo kukuta mimi simo, kuna kisa katika Injili(Biblia)kinafaa nikitaje ili upate ufahamu mzuri, Nabii Issa a.s (Jesus)"Alichukuliwa na Shetani kwa ajili ya majaribio(Mtihani)kwa muda wa siku arobaini, baada ya kupasi majaribio yote Shetani akamchukua katika jaribio la mwisho, Akampeleka kwenye Mlima mrefu, ikisha akamwambia kama uyasemayo ni kweli basi chupa nikuone, chupa nithibitishe, Nabii Issa a.s(Yesu)akamjibu (Baba Hachezewi),"Kwa hiyo na wewe ukitaka kufanya majaribio ya kulala na godoro lako la pesa kumbuka (Baba Hachezewi).
Sasa tunaingia kwenye aya yenyewe tuichungulie (Sifat ul Haafiz)Baqara 255
ٱللَّهُ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَىُّ ٱلۡقَيُّومُ‌ۚ 
"Mwenye Enzi Mungu ni mmoja hakuna Mollah(Mwengine)na ndiye Mwenye Uhai wa Maisha na Mwenye kusimamia kila jambo"
Wapi unataka hifadhi kwengine hali ushajua Yeye ndie aliyekupa Uhai na Yeye ndie wa Kudumu, hata hao wakikudhur elewa yeye atakupa Uhai tena, ondoa wasiwasi".
 لَا تَأۡخُذُهُ ۥ سِنَةٌ۬ وَلَا نَوۡمٌ۬‌ۚ
"Hakumshiki kusinzia (Kusahau)wala kulala"
Vipi atashindwa kukuhifadhi hali yakua wakati wote ni mwenye kuwaangalia na kuwajua viumbe vyake.
لَّهُ ۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَمَا فِى ٱلۡأَرۡضِ‌ۗ 
Ni vyake (Vyote) viliyomo Mbinguni na vilivyomo katika Ardhi.
Sasa itatokeaje kuwa awe Mlinzi wako asiyekua Yeye Mollah wako, ikiwa kavimiliki vyote vya mbinguni na ardhini atashindwa kukuhifadhi wewe.
مَن ذَا ٱلَّذِى يَشۡفَعُ عِندَهُ ۥۤ إِلَّا بِإِذۡنِهِۦ‌ۚ
"Nani huyo awezaye kuombea mbele yake(Mollah)Bila ya Idhini yake". Hakuna yoyote anayeweza kukudhuru wala ukidhurika hakuna awezaye kukuponya isipokua lazima ipatikane Idhini yake Yeye aliye (Hafiz)Bure kuhangaika na mizimu, Upuuzi mtupu eti mpaka utambike, mizimu imehamaki, Mganga akichukia utaangamia, yote hayo porojo, Jua wewe Umehifadhiwa Na Yeye Mollah wako alokuleta katika Ulimwengu huu, na akitaka jambo likufike litakufika hakuna wa kuzuia, Na akitaka upone utapona bila ya Mganga, hujiulizi mbona Ndege na wanyama wanapona bila ya (Doctor).
يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡ‌ۖ 
"Anayajua yaliyo Mbele yao (Viumbe)na Yaliyo(Nyuma)yao"
Mwenye kuyajua ya mbeleni kabla ya kutokea hayo msoyajua, Na pia anayajua yale mlokwisha kuyasahau ambayo yashatokea vipi leo ashindwe kukuhifadhi."
وَلَا يُحِيطُونَ بِشَىۡءٍ۬ مِّنۡ عِلۡمِهِۦۤ إِلَّا بِمَا شَآءَ‌ۚ
"Na wala(Viumbe)hawalijui lolote katika Ilimu yake(Mwenye enzi Mungu)ila kwa alipendalo(Analolitaka)"
Hakuna kupiga Bao(Ramli)wala kujua utibabu huu na ule, au chochote katika Ulimwengu huu mpaka ujulishwe kutoka kwake Mwenyewe mwenye kuhifadhi.
وَسِعَ كُرۡسِيُّهُ ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضَ‌ۖ وَلَا يَـُٔودُهُ ۥ حِفۡظُهُمَا‌ۚ وَهُوَ ٱلۡعَلِىُّ ٱلۡعَظِيمُ
"Enzi yake Imeenea Mbingu na Ardhi, wala hakumshindi kuvilinda, Na yeye Ndiye aliye juu na ndiye aliye Mkuu"
Huo ndio Ufalme wa Mwenye enzi Mungu, umekimiliki kila kitu, Na hiyo ndio hifadhi unotakiwa kuijua, Na hivi ndivo unavotakiwa fikra hii ikuingie katika mawazo yako yende (deep)kuwa kila ukiona Binaadamu, Vinyama, Miti, Mbingu,Nyota,Mwezi,Jua Uwe unakumbuka kuwa vyote hivi ni Enzi ya Mwenye enzi Mungu, Na kwamba yeye ndiye aliyeviumba na yeye ndiye Mwangalizi wake, Na pia ndiye (Hafiz)Mwenye kuvihifadhi, Aliye juu ya kila alichokiumba na ni Mkuu wa kila Jambo, basi litumie Jina hili la (Haafiz)uipate kinga itokayo kwa Mollah wako.






No comments:

Post a Comment