Sunday, November 24, 2013

MAJINA YA MWENYE ENZI MUNGU(RAZAQ)PART 2

Asalaam Aleiykum,

Yeye ndiye ambaye akileta msukosuko wa Mvua au Kimbunga Biashara zote husimama, akikutieni mtihani wa vita nchi nzima inafilisika, akikuondosheeni amani kidogo tu Petrol inapanda, mara haiwezi kusafirishwa, vyakula bei juu hichi hakendi kile hakirudi sasa jiulize nani Mwenye kuruzuku.
Ukiyajua hayo basi utagundua hata huko kupewa kwako Mali ni mwenenedo wa kuruzukiwa, Hiyo njia ya kutafuta Riziki pia ni kuruzukiwa, huo Uhai pia ni kuruzukiwa, kakutia yeye fahamu na kukuonesha mipango ya kufanya mpaka ukaweza kuipata hiyo Mali ulonayo. Yeye ndiye anayempa anayemtaka na kumnyima anayemtaka, Na katika viwili hivyo kuna sababu ya undani ikiwa utakua mjuzi wa kutizama, Kwa hiyo ikiwa ushahangaika sana na unaona Utajiri haupatikani basi pumzika jua Mwenyewe mwenye Kuruzuku hataki utajirike, Na ana sababu za kufanya hivyo na hiyo pia ni baraka itokayo kwake ili utumikie mambo mengine, lakini wapi wewe umeshikilia lazima upate utajiri na hayo ndio makosa yako.
Basi litumie Jina hili la Razaq kwa ajili ya kumuomba Mollah wako, Na usije kudhani mapesa yataporomoka kutoka mbinguni ila atakufungulia njia ili uweze kupata hiyo Riziki, Na hata ukinyimwa furahi kwani kuna mengi Mollah wako anayo kuruzuku hayana hesabu, Na kama hujapewa kabisa Furahi jua Mollah wako kakusikia na anakupenda na uko karibu nae na kila ukimuomba hakupi,basi kwa kutamka jina hili litakujulisha kitu kwamba Mollah kakupa mengine yenye thamani kuliko huo utajiri, Na kwa kukunyima huo utajiri anakupenda na kukuepusha na shari yake,
Tunakuomba Mollah, Yaa Razaq, tupe ulotupangia ya kheri na utujaalie kuridhika.

No comments:

Post a Comment