Sunday, November 10, 2013

MAJINA YA MWENYE ENZI MUNGU (ALIIM) PART 1

Asalaam Aleiykum,

Hakika yeye ni Mwenye kujua kila kitu kwenye Ulimwengu huu,(Aliim) Nini Kujua? Kujua ni Elimu yenye kuhusiana na (Roho), Ndio maana utaona kujua siku zote kunatokea ndani na wala sio nje.
Na mifano ipo chungu nzima ikiwa unataka kuelewa nini kujua, basi hebu jiulize inakua vipi mtoto akizaliwa anajua kutafuta ziwa la mama na kulinyonya, nini kinachomjulisha sasa aanze kutambaa,(Lazima kuna kitu kinamjulisha), Nani anomjulisha mnyama akizaliwa tu anze kusimama na kutembea,,Nani Mwenye kukujulisha wewe sasa hivi uhai na mzima, Nani Mwenye kukujulisha wakati Umelala amka sasa ushamaliza usingizi, Yeye huyo ndie ajuae fulani siku gani ataumwa na lini atakufa, Nani atazaliwa na nchi gani atakayozaliwa, Yeye huyo Mtukufu ndie aliye kienea kila kitu kwa Ujuzi(Muhittun)Kila kitu kimo katika Ufalme wake wa Kujua.
Yeye ambaye kakipanga kila kitu kufata amri za ujuzi wake bila ya upinzani wowote, Na akaufunza ujuzi huo kwa kila kilicho Hai chenye kuishi. Kwanini nikaita ujuzi na nisiite elimu, Sababu elimu ina kikomo lakini ujuzi hauna kikomo, elimu ukijua kidogo wenzio wanajua zaidi, lakini ujuzi au kujua hakuna tafauti wewe unajua hili ua na mwenzio analijua hivyo hivyo hili ua, hakuna tafauti, kujua kama kuona au kusikia hakuna mwenye kuzidi, ukisha kujua ndio ushajua hakuna mbadala, kujua kunatokana na hiyo elimu ya (Ghayib)au siri kama alivosema Mwenye huo Ufalme wa kujua kwenye sura ya (Hashir 22)
هُوَ ٱللَّهُ ٱلَّذِى لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ‌ۖ عَـٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ‌ۖ
"Yeye ndiye Mwenye enzi Mungu ambaye, Anayajua yalofichikana na yaliyo dhahiri"
Mafundisho yote yanatokea kwake kwenye enzi ya siri na kufundishwa viumbe vyote, Na kila kiumbe kimefunikwa na ujuzi huu usiokua na mwisho, Jiulize swali la rahisi kwanini kila kiumbe kina dasturi ya kufanya maskani ya kukaa, Nani alomfundisha Ndege kujenga Nyumba yake na kutafuta Riziki, Na ana juaje wapi ataipata. Yeye huyo ndie Mollah Mjuzi mwenye kumfundisha huo ujuzi wake kila kiumbe, Akateremshiwa huyu akawa mwenye kuvumbua kutengeneza Ndege, Na mwengine akaunda Meli, Yule akavumbua kile na huyu akavumbua hichi, Na wote ukiwauliza wapi mumepata (Idea)hizi, imekuaje mpaka mkajua, ilikua vipi hata ukatengeneza gari, atakujibu mimi imenijia tu katika Akili yangu, Ikisha nikaandika kwenye karatasi ndio nikaanza kuifanayia kazi.
Nini Elimu?
Endelea part 2

No comments:

Post a Comment