Sunday, November 24, 2013

MAJINA YA MWENYE ENZI MUNGU(RAZAQ)PART 1

Asalaam Aleiykum,

Mwenye Kuruzuku(Mtoa Riziki) Wanaadamu tumo katika kiza kikubwa hata akitokea Mtu akakushika mkono na kukufahamisha twende upande huu kuna muangaza utatoka kwenye giza basi hutokubali kumfata, Mwenzangu wee mimi nimeshaona alama ya taa waweza kuipata njia na ukatoka kizani basi utatia wasiwasi na hutokubali kumfata abadan. Hiyo ndio desturi ya Imani dhaifu inavokuamrisha ubakie kwenye kiza, Imani hiyo inatufahamisha kuwa kipato kinapatikana kutokana na nguvu zako mwenyewe.
Napenda uelewe hakuna nguvu zako mwenyewe ila yupo alokupangia ikisha akakuonesha na njia za kupita, halafu akakufundisha mipango ya kufanya mpaka ukaipata hiyo (Riziki).
Yeye ndiye ambaye mwenye kusababisha kila kitu katika Ardhi hii, basi kwanza "Na atizame mwanaadamu chakula chake"Abasa 24"فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَـٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِ"
Ukitizama chakula kinaweza kukupeleka safari kubwa ya kufika kwenye ukamilifu wa Imani yako katika jambo la kumjua(Razaq) Kakuwekeeni kila kitu kuanzia chakula chenu mpaka Mali ghafi zenu mnazipata kutoka katika Ardhi yake, kama Petrol,Dhahabu,Shaba,Vyuma,Almasi Maji na kila kinachohitajika katika Uchumi wenu, sasa Jiulize nani Tajiri, Nani mwenye kutoa, Nani anopanga huyu apate kile na huyu apate hiki, ukimjua Mwenye kupanga hayo basi Yeye ndiye (Razaq) Ambaye baada ya hapo akawa Mwenye kuwaonyesha waja wake njia za kuvipata vitu hivyo, Huyu akampa elimu na kumpangia wewe itakua kazi yako Ofisini, wewe utakua mfanya biashara, akawapa maguvu nyinyi mtakua mnatumika kwa njia nyengine kuipata Riziki yenu.
Ikisha baada ya yote hayo akatoa mtihani kuwaangalia waja wake alowapa kwa radhi na mapenzi yake kama jee akiwataka watoe vile alivowapa watamtii, Jee watafanya hivyo kwa ajili ya Imani ya kumpenda Mollah wao na kuvitoa kwa mapenzi? lakini wapi hapo ndipo anasahaulika kabisa Mwenye kuruzuku na mnageuka kuwa wenye"

وَتُحِبُّونَ ٱلۡمَالَ حُبًّ۬ا جَمًّ۬ا
(Kuipenda)Mnapenda Mali pendo la kupita kiasi.
Unasema kabisa hapa hakitoki kitu, unapata maradhi ukimuona maskini unaanza kupanga uongo wa kujikinga kabla hata hujakutana nae,(Kumbe maskini mkipishana anakutolea salamu tu) Na akitokea Mtu kukumbusha jamani mnatakiwa mtowe mtaanza kumwita husda huyoo wa mali za watu, Na kuna wengi wanasahau kama katika maombi yao chungu nzima kabla ya kupewa hiyo Mali walikua kwenye Sijda au sehemu ya siri katikati ya usiku wanaomba na kusema," وَمِنۡہُم مَّنۡ عَـٰهَدَ ٱللَّهَ لَٮِٕنۡ ءَاتَٮٰنَا مِن فَضۡلِهِۦ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ"(Tawba 75)
Na miongoni mwao wako waliomuahidi Mwenye enzi Mungu kuwa,(Kama)akitupa katika fadhila zake tutatoa Sadaka na tutakuwa miongoni mwa wanaotenda mema.
Nenda ukaombe sasa hivi uone cha mtemakuni, Pengine utamkuta mtu kaweka (Bodyguard) hao kwa madhumuni ya kuwazuia maskini tu wasimkurubie, Basi kumbuka huyo ndio (Razaq)mwenye kumiliki Uchumi wote katika Ulimwengu huu.
Endelea part 2


No comments:

Post a Comment