Asalaam Aleiykum,
Unakijua chombo cha Wanasayansi au Mapolisi kinachoitwa(Heat Seeking Equipment)Chombo hichi kina uwezo wa kukujulisha wewe mwanaadamu iwapo utakua umejificha popote pale Ulimwenguni, hicho ndio chombo wanachoringia wanasayansi wa kidunia kuhusu ugunduzi wao wakuijua hiyo (Energy)inayotoka kwenye Maumbile ya Binaadamu au kwenye chombo chochote kinachotoa (Heat). Na wanasayansi wa Ulimwengu ulojificha(Mystical)Ulimwengu ambao wewe huuoni mpaka fadhila zikushukie au upate mafunzo Maalum yalombatana na Taqwa, katika Ulimwengu huu wa (Mysticism) wao pia wamegundua kuna (Energy)Maalum inatokea iwapo Mja atajifunga na vitendo vya Ibadah, Na kwanini isiwe hivyo wakati leo Jambazi likikimbia usiku wa manane likajificha linaonekana lipo wapi, nini habari yako wewe unayenyanyua hatua kujifunga kwa nia kuelekea Msikitini kwenda kufanya Ibadah, nani anayekuona wewe?.
Itupie macho kwa makini habari hii tunayozungumza ili upate faida ya kwenda kuzisali Sala zako Msikitini, Usije ukaanza kusoma halafu kuja na tafsiri zako, itakupita maana ya Darsa hii, Sababu kila mtu ana tafsiri yake anavosoma au kuona mambo, na ukitaka kujua vipi tafsiri zinavoondoa maana kihudhurie kisa hichi cha Fundi wa Kibaniani, Baba na Mtoto wake,halafu uone vipi kila Mtu anavo fahamu atakavyo yeye, "Kuna siku kati ya masiku Zama hizo za zamani katika Mji wa Unguja""Mzee Fulani alikua anadaiwa na Fundi wa Kibaniani kwa ajili ya utengenezaji viatu""Mara akapiga hodi yule fundi viatu, Baba aliposikia Mlango unagongwa akamwita Mtoto wake(Itizame tafsiri ya kuona, kusema, na kusikia inavobadilika) na kumwambia kama fundi viatu basi mwambie Baba katoka""Yule Mtoto akatoka mbio mpaka Mlangoni akamwambia fundi viatu, Baba anasema Katoka""Baniani akatizama chini kizingitini akaviona vile viatu alivotengeneza""Na yeye akajibu""Mwambilishe Bana Kuba, kama siku pili tatoka sisahau Guu yake"Naam hivi ndivo kila mtu akisoma darsa zangu anatia tafsiri yake, namie nakwambieni Msisahau kwamba hizo ni tafsiri zenu sio zangu, na ukija namna hivyo utakosa faida, inabidi ukiondoka (Sisahau Guu yako)maana si (Tafsiri)yangu mie, njoo (Open) wacha Darsa iingie ilete (Transformation) upate badiliko fulani, ukiona haifai niachie mwenyewe.
Naam sasa turudi nyuma tupate kuijua hii (Energy) inatokea wapi? na nini dhumuni lake?.Kwanza inabidi ukumbuke unapotaka kubeba kitu kizito au kufanya kazi ngumu inabidi vipatikane vitu vinne Muhimu vifatavyo ili uweze kutekeleza hilo tendo (Chakula, Afya, Nguvu, na Akili Timamu) ili upate kubeba Begi moja la kilo hamsini tu, vikikosekana viwili katika hivo kazi haifanyiki, unajua Kwanini? Endelea Part 2
Sunday, August 25, 2013
SALA YA MSIKITINI PART 2
Asalaam Aleiykum,
Sasa (Energy) hii inapatikana vipi? Tizama ndani ya Quraan upate jawabu la kuridhisha kabla hujenda Msikitini, Inapatikana Nguvu hii kwa dalili hizi ndani ya Quraan, Kwanza kabisa kuhusu hicho chakula, Abbasa aya ya 24 " فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَـٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦۤ""Hebu Mwanaadamu na atizame chakula chake", vipi kinavokupa nguvu kikajenga Mwili wako ukawa uko tayari kuhimili kazi zako(Yeye Mollah ni Mwenye kukileta hicho chakula na yeye ndie mwenye kukupa hizo Nguvu). Tunajua Akili ni yenye kuchukua 75% ya vitamin ya hicho chakula, sasa tunaelewa Akili inafanya kazi za ziada, kutwa nzima unaandika na kufikiri ndani ya kichwa chako, mara wazo hili, mara wazo lile, hupumziki hata sekunde tano ila wazo lishaingia na lile linatoka, na kwa hivyo inatakiwa Akili yako iwe timamu kupata utulivu wa hiyo (Energy).
Aya ya Mwanzo sura ya Qalam "نٓۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ""Naapa kwa (Akili)Kalamu, Na yale Wayaandikayo kwa (Akili)kalamu hizo""(Lazima uwe na dhamana ya Akili yako ili Uwe Muumin wa kweli).
Ama kuhusu hiyo Afya Al-Shuara aya ya 80" وَإِذَا مَرِضۡتُ فَهُوَ يَشۡفِينِ""
Ninaposhikwa na Maradhi, Yeye ndie anayeniponesha"Hiyo ndio afya, yote ipo kwenye ufalme wake(Yeye Mollah ndie anaekudumisha katika Afya, na ukiwa na Afya unasahau kila kitu, lakini wacha Ukucha tu ukiuma watu wote hawalali kwenye Nyumba, kwa hiyo unaona vipi vitu vyote vimezungukwa na Ufalme wa Mwenye enzi Mungu), na kuhusu nguvu itizame sura ya Ghafir aya ya 2"تَنزِيلُ ٱلۡكِتَـٰبِ مِنَ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡعَلِيمِ" Kuteremshwa kwa kitabu(hiki)kumetokana kwa Mwenye enzi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye kujua".
Ukiangalia aya zote hizo Nne nilizo zitaja maelezo yake yanaashiria Uweza wa Mollah na vyote hivo vinavyoilete hiyo (Energy) vinatokea kwake Mollah wetu, kuanzia Chakula, Akili, Afya, na hiyo nguvu, ndio wewe ukapata uwezo wa kulibeba (Bag moja la nguo) Na ukilinyanua Bag hilo unakua ushapunguza hizo nguvu, mpaka uzitafute tena, Sasa hili la Ibadah inakuaje? Unaambiwa kila Ukinyanyua Mguu unaandikiwa(Thawabu na kuongezewa hizo Nguvu) na ikiwa Nia yako na vitendo vyako vimefungana na dhumuni la Ibadah, basi kila nguvu zinazopungua unapata (Recycle)yake mara (Saba) Sitoweza kuifundisha hadharani siri hii ya kukufanya usichoke, hii ndio walonayo wacha Mungu ukawa unawaona hawachoki kufanya Ibadah, sio kama mimi na wewe tukisali usiku siku tatu tu tunaanza kukumbuka kipenzi chetu usingizi.
Nguvu zenyewe za kunyanyua hatua kwenda msikitini hazitakiwi ziwe zimechanganyika na mambo ya kipuuzi, unapotaka kwenda Msikitini kwa ajili ya Ibadah lazima mawazo yako yote yawe (Intune)Na Ibadah. (Mfano)unakwenda Msikitini uanze kwa Mawazo ya kumsabahi Mollah wako, au kusoma Quraan hapo ndio utakua unatengeneza hiyo (Energy), Lakini kama utaanza safari yako kuelekea Msikitini huku una (Magazine)nzima ya (Love Story) au unakwenda Msikitini na mawazo ya miadi, atakuja saa ngapi, au unapanga vipi utamfanyia fulani Ujambazi, hapo unakua si mwenye kuipata hiyo (Energy)wala Thawabu. Na elewa kila kitu katika Ulimwengu huu kinatengeneza (Energy) ukiwemo na wewe na (Energy) za Ibadah ni zenye kubakia. Endelea part 3

SALA YA MSIKITINI PART 3
Asalaam Aleiykum,
Anahadithia Sahaba Abdulla bin Omar r.a "Siku moja wakati Bwana Mtume s.a.w ameshakufa" Ilitokea kuna mtu ambae hakumuwahi Bwana Mtume s.a.w katika uhai wake, lakini alipopita Sahaba mmoja alokua pamoja na bwana Mtume s.a.w katika uhai wake, alinyanyuka bwana huyu na kuuvamia ule mkono wa Sahaba na kuubusu, alipoulizwa kwanini ulifanya vile, akajibu hamkijui kilichonivuta mimi kwenye ule mkono, lakini nitakwambieni kimoja tu mkono ule umewahi kushikana na mkono wa Bwana Mtume s.a.w. Hivo ndivo (Energy) Inavobakia katika Ulimwengu huu, hiyo ndio Maana ya kuambiwa Sala ya Msikiti wa Makka na Madina ni (Bora) kuliko Misikiti mengineyo, na hivi ndivo tunavo wajibu wale wanotuuliza kwanini kila ukenda Unguja lazima ukasali Msikiti (Gofu)Msikiti huo wamepita Mabwana wazito wazito, na (Energy)zao zimebaki kama tutavoona huko mbeleni.
Unakwenda hatua baada ya hatua mpaka unawasili Msikitini, Hatua na (Energy) ulotengeneza kwa ajili ya Ibadah zinabaki katika Ulimwengu huu kama inavobaki Sauti yako, Ukisema Uongo unabaki, ukipiga kelele zinabaki, ukisoma Quraan inabaki, hakuna kinachopotea, kwa hiyo tahadhari sana vipi unatumia (Energy) yako, iwe ya kazi, sauti, au Ibadah.
Unaingia Msikitini kila tendo lako linatengeneza (Energy) ambayo inabaki ndani ya Msikiti, ni matendo ya Ibadah, ni sauti za kusabahi, ni matendo ya kutukuza,kuomba Dua na kusujudu yanaobaki Ndani ya Misikiti, Sasa nini kinatokea, unaingia Muumin mja wa kheri, mnasimama kusali Jamaa kwa pamoja, na hapo ndio inapatikana (Symbol) ya Sala ya Kiislam ilokusanya Sala za dini zote za (Ahlil Kitaab) ukiwa wewe (Mkiristo au Myahudi)zote zimo, ikiwa unasali kwa kusimama basi kwenye Uislam utasimama, ikiwa unasali kwa kukaa kwenye Uislam pia imo kukaa, ikiwa unasali kwa kusujudu pia kwenye Uislam Utasujudu, kwa kuwa Dini ya haki imekusanya Dini zote na kuifanya ni Dini kuwa Moja.
Sasa Mtizame khalifa wa kwenye hii Ardhi vipi anawakilisha kila kilichomo katika Ulimwengu huu, Anasimama Mbele ya Mollah wake Kwa Heshima zote akiachia mikono au akifunga, akinyanyua au akiiwacha chini, basi yeye Mbele ya Mollah wake ni mwenye kuwajumuisha Ndege, Milima, na Miti na vyote vilivyomo, amesimama kwa unyenyekevu wa Kumsabahi Mollah wake na anapo (Rukuu) anajumuisha na kujirejesha kwenye hali ya (Mnyama) anakubali kuwakilisha jinsia ya ukaribu na Umbile lake na la Wanyama wote, na anapo (Sujjudu) hapo anarejea kwa kutii amri ya Mwenye enzi Mungu aliowaamrisha Malaika na Majini kuitenda, Amri ya kusujudu ni (Surrender) Unayayuka kwa utiifu, kwa kutii Amri ya kuanguka kwenye Ardhi na kumsabahi Mollah wako na Kumtukuza kwa sifa kubwa kubwa, hiyo ndio (Symbol)ya Sala ya Kiislam, na hapo ndipo inapobakia hiyo (Energy)ya Ibadah, na ndio unapatikana Utukufu wa Ibadah ya Msikitini, na hupatikana hiyo (Rest-Energy) au (E=Mc2)ya Ibadah, huo ndio Ubora wa Msikiti, na kila Pakisaliwa (Energy) inaongezeka na unapatikana uzuri wa dua za msikitini na Mambo ya kheri yanofanyika humo na usafi wa Nyumba hizo za Ibadah, na uzuri wa kuitwa (Baitul-Sujjud).Kwa hiyo fanya umuhimu wa kuipata Sala ya Msikitini na Fadhila zake ili na wewe uwe umewacha (Energy) ya Ibadah katika Misikiti hiyo.
Na kama Wanasali watu wa Kheri katika Misikiti hiyo na wewe ni Mwenye kuijua (Energy) hii basi ukiingia kwenye Msikiti utahisi (Positive Energy) Itakujaa Furaha ya wewe kuwapo Msikitini hapo, Na kama Wanasali Watu wa Shari, Wanaabudu watu wa Dhuluma, au Wala Rushwa, basi Utahisi (Nagative Energy) na utataka utoke mbio, mara utaona Mahirizi na vituko vya kila aina, Nyumba ya Mungu inageuzwa sehemu ya Mikasa na jukwaa la mazungumzo, hilo si dhumuni lake na kama unajua maana ya Msikiti basi toka mbio usije ukawa mwenye kushiriki katika (Nagative Energy). Tunamuomba Mollah atujaalie kuyajua hayo na kuyaepuka.

Sunday, August 18, 2013
DINI HAINA MWANZO HAINA MWISHO PART 1
Asalaam Aleiykum,
Tunaendelea na Darsa zetu kama kawaida, leo hii kwa kuwa mwezi wa Ibadah umekwisha, miskiti mitupu, safu mbili zinapatikana kwa shida tena hazitimii, na yule anosali nyumbani anakusanya zote ili asali kwa pamoja umuondoke udhia, kwa kuwa wengi wetu hatujui nini Dini?.
Dini ni haya Maisha yenyewe, kwani nikisema mfumo ntaipunguzia hadhi Dini, Na mfumo una tabia ya kubadilika, lakini dini haibadiliki na wala haina kikomo, maisha hayana mwisho (Life) inaendelea, ndio maana ukaambiwa utafufuliwa siku ya (Qiyama)lakini wewe Binaadamu unao mwisho, ndio utaona mara unaingia mara unatoka katika maisha haya ya Dini, Na unapotoka katika maisha haya ya dini unakua ushachupa katika maisha ya Matatizo wewe mwenyewe, Kwa sababu maisha ya Dini ni Maisha ya (Gurantee) ndani yake hukuti matatizo ila unakuta Mitihani.
Nini Matatizo? Matatizo ni jambo la kujitakia (Mfano) huna pesa, hujui Biashara, ikisha unakopa kufanya Biashara na huku unaweka Nyumba yako Rehani, Biashara ikianguka ushaingia kwenye matatizo, unatafuta pesa za kulipa, njia za kuinusuru nyumba yako, na kubwa zaidi la kuilisha (family) yako, matatizo yanaanzia hapo, na kutoka kwenye matatizo inakua shida kubwa. Lakini kwenye Dini unapata Mtihani, Nini Mtihani? Mtihani ni jambo linalokuja (From Unknown) kutoka kwa mwenyewe Subhanna, na Mtihani una hakika wa kumalizika,(Mfano) Maradhi, unaumwa halafu unapona, umeshikwa na njaa unapewa njia ya kupata chakula, na mengi ambayo ukitulia na kuangalia kwa makini unajua hili mtihani na hili nimejitakia mwenyewe, Kumbuka Mtihani kutoka kwa Mwenye enzi Mungu, Matatizo kutoka kwako mwenyewe.
Sasa nini Dini? Dini ni kitu unachozaliwa nacho, halafu mwenyewe unaamua kutoka katika Dini kwa kuonja tunda la Elimu, tunda la kufahamu, lakini kufahamu huku kwa njia ya (Innocent) kunakupeleka kufanya uchunguzi wa kila kitu, kama alivo mtoto hichi nini, kile nini, ikisha unakwenda katika daraja nyengine ya (Ignorance) unafanya mambo katika Ujana ukiwa hujali matokeo yake wala madhara yake,Maasi kwako inakua jambo la kawaida, Unazama kwenye bahari ya dhuluma na kufanya Unyanganyi, Uongo kwako kawaida, Zinaa na fujo zote unazikabili kifua mbele, na hivyo vyote ni nje ya Maisha ya Kidini, Halafu tena kila mmoja wetu anapata (Chance) Nyengine ya kurejea kwenye hayo Maisha ya Kidini, unapata nafasi ya kurejea kwenye Maisha ulokua nayo mwanzo ya kidini, lakini wakati huu inakushukia hiyo (Wisdom)Hekima, Ujumbe unakufikia unakukuta uko (Choppy)kwa magunia ya Dhanmbi na mashaka na madhila ya Ulimwengu, unafahamishwa Rejea kwenye Maisha anayoridhia yule alokuumba, toka kwenye matatizo, ondoka kwenye moto wa ulimwengu, rejea kwenye bustani(Nyumbani)ulikokimbia.
Inateremka Nusura hii ya Hekima kukujulisha kwamba sasa jua lishakuchwa, acha kuzama kwenye shughuli za watu, usitumie Umri wako mpaka ukataka kukopa umri wa watoto wako, sasa wewe basi, na kutaka kujua kama umefika kikomo utaona dalili mwenyewe mbona wenzangu wamebadilika, mbona wote wanavaa hijab, inakuaje sasa wanahudhuria darsa, mbona disco hawaji tena, mbona harusini hawachezi tena, mbona wamecharuka kushiriki mambo ya kheri, sio kwa kujionesha, kwa sababu ukifanya kwa kujionesha basi jua (Hekima) au hiyo Nusura haijakufika, mabadiliko yapo mengi ya kukujulisha kwamba sasa ushapata taarifa ubadilike, urudi nyumbani ulipotokea, uwe mtu unaeishi maisha ya Kidini, na vipi utajua umesharejea kwenye maisha ya kidini?
Endelea Part 2

DINI HAINA MWANZO HAINA MWISHO PART 2
Asalaam Aleiykum,
Ukiishi Maisha ya Dini unakua usharejea Nyumbani kwa Mollah wako, Na ukirejea Nyumbani unarejeshewa jina lako la asilia, lipi hilo jina lako la Asili ? Al Furqan 63.
"
"وَعِبَادُ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلَّذِينَ يَمۡشُونَ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ هَوۡنً۬ا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ ٱلۡجَـٰهِلُونَ قَالُواْ سَلَـٰمً۬ا"
Na Waja wa Mwenye enzi Mungu, Ni Wale wanokwenda Ulimwenguni kwa unyenyekevu, Na wajinga wakisema nao huwajibu Salama.
Naam, Yametajwa maneno makubwa hapo kama utayazingatia unaweza kupata faida itakayokua taa yako ya muongozo katika kurejea kwako katika dini. Hakiki sisi sote ni Viumbe wa Mwenye enzi Mungu, lakini kuwa Mja ni daraja nyengine, Nani Mja?
Mja ni yule ambaye Imemjia Hekima(Wisdom) akaikubali na kugundua kwamba mimi niko Ngambo ya Pili, natakiwa nirudi katika Dini nifate Amri zote, Akagundua kwamba mimi Mwenyewe nimeumbwa kutokana na Utiifu wa Billion za (Cells)kila moja inafanya kazi yake kutokana na Maamrisho ya dini ili kunifanya mimi niwe Hai.Na Amri hii ikikatika mimi baada ya nusu saa naanza kunuka, nakera wenzangu, hao wanakwenda kunifukia futi 6 chini ya ardhi, wanaweka na ubao hata nikiamka nisiweze kuja juu, Mwenye kugundua hayo, anaelewa sasa kila kitu katika Ulimwengu huu ni Dini, Kinafata Amri za yule aliyekiumba, anakuaje huyo alopata Hekima hii(Wisdom).
Anatembea kwenye Ardhi hii kwa Unyenyekevu(Simple) anajua umuhimu wa kuishi kwa muongozo wa Dini, Dira na Ramani inakua ni Dini yake, anajijua yeye yuko hapa kwa muda mchache, anajua dini ni yenye kudumu kwa hiyo anaamua kuwa na hizi sifa nne (4), anakua Muangalizi wa Wanyonge(1) mambo yote ya Maskini ni mwenye kuyashughulikia bila ya Kiburi wala kutaka sifa,(2)Anakua msafi wa Moyo, na Mtu wa Salama kila mmoja anaweza kumkabili na kumwambia shida zake, (3) Anakua Mnyenyekevu kwa Binaadmu wenzake, (4) Na Mwenye kukihurumia kila kiumbe na kukitakia Salama kwenye Ulimwengu huu, akipata Mja sifa hizo anaipata hiyo(Simplicity) na moja kwa moja anarejea Nyumbani na kuwa Mja wa Mwenye Enzi Mungu, Zinamuondoka Hamaki au hasira, unamteremkia Upole, na hata akikutana na (Ignorance) wakawa wanamkejeli na kumcheka yeye anakua kashapata kitu adhimu sana Moyoni mwake, yote wanayoyasema anawajibu kwa Usalama, anawaombea (Peace upon you) Salama iwe juu yenu, mpate kama niloyapata mimi ya kurejea kwa Mollah wangu, na huku tu ndio kwenye hiyo Salama. Hiyo ndio Dini kila kitu kimo ndani ya Dini, kimezungukwa na Dini, mwanzo dini mwisho dini, kutokana na hiyo Dini ndio ikapatikana Ibadah, kwa hiyo Waja wa Mwenye enzi Mungu wameruhusiwa kufanya Shughuli zao kama zilivopangwa na utaratibu wa Dini, Ikisha wakimaliza hizo Shughuli, basi wanatakiwa hapo hapo kurudi Nyumbani, nenda ofisini, nenda kafanye biashara, toka ukalime, katembelee watu nk, lakini ukimaliza unasubiriwa na aya hii Ash Sharh aya ya 7
"فَإِذَا فَرَغۡتَ فَٱنصَبۡ" Basi ukishamaliza(Yalokushughulisha)Shughulika (Na Ibadah) Na kama utakutana na Mja wa Mwenye enzi Mungu utaona mabadiliko fulani, kula kwake Ibadah, mpaka kulala kwake Ibadah, kusema kwake Ibadah, na hizo Ibadah ziko unazozifanya kwa hiyari na zengine zinatendwa kwa Mpangilio wa Dini Inavotaka kutokana na Amri ya Mollah wako, (Mfano)kama vile kuvuta pumzi, kusaga chakula na mengi mengineyo hayo yote yanafanywa kwa ajili ya Amri ya Mollah wako na hiyo ndio dini ilokizunguka kila kilichomo kwenye Ulimwengu huu, usije ukakerwa na Akili yako ukadhani Dini ni Ibadah, Ibadah ni tendo ndani ya Dini, Dini ni kila kitu kilichomo Ulimwenguni ukivipenda na kuvitunza na kuvithamini, basi utakua umo ndani ya dini, Siasa, dini, Uchumi dini, ndio maana utaona nchi hii inapewa mafuta, huku kunagunduliwa gas, kule kuna madini, hapa kuna hichi na kile mambo yote yanasimamiwa na mfumo wa Dini, chochote kile ukitendacho kimo ndani ya dini, ila anakuja Shetani kukutoa katika Uangalizi wa Dini, ndio maana Waumin mnakumbushwa katika sura ya Baqarah aya ya 208
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱدۡخُلُواْ فِى ٱلسِّلۡمِ ڪَآفَّةً۬ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٲتِ ٱلشَّيۡطَـٰنِۚ إِنَّهُ ۥ لَڪُمۡ عَدُوٌّ۬ مُّبِينٌ۬
"Enyi Mloamini ingieni katika Uislam (Kwa)Ukamilifu, Wala msifate nyayo za Shetani, kwa hakika yeye kwenu ni adui (aliye wazi)Dhahir"
Msikubali kutoka katika dini, kubalini kwa ukamilifu yote alokupangieni Mollah wenu, furahini na kila kilichomo katika Ulimwengu, Msikubali kutoka Nyumbani na kufata nyayo za Shetani hakika yeye nia yake ni kukupotezeni, ili msahau kuwa nyinyi metokea Nyumba ya Dini na mnatakiwa mrejee muishi maisha ya salama ndani ya Dini, na hapo ndipo hapana mwanzo wala hapana mwisho, ila maisha ya milele yenye kheri na neema.Ambayo tunamuomba Mollah atujaalie sote kwa uwezo wake.

Sunday, August 4, 2013
KWAHERI RAMADHAN KARIBU UCHA MUNGU PART 1
Asalaam Aleiykum,
Pata habari ya kitoto kichanga kinapozaliwa na wewe ukajua kwamba kinyanginya chako au kitukuu chako kimekuja kwenye Ulimwengu huu kikiwa safi, na vimacho vyake vyeupe, chakula chake cheupe, ambacho ni maziwa hayana doa wala dosari, kitoto hicho kinakua kinategemea kila kitu kufanyiwa na wazee wake mpaka kitapofikia umri wa kujiweza au kupata fahamu na kuanza kupinga yale yote anoamrishwa na wazee wake, hiyo ndio kawaida yetu sote, hiyo ndio njia tunayopita kila mmoja wetu. Kumbuka na wewe umepita katika hali kama hiyo katika mwezi huu wa Ramadhan, Tafauti yako na hicho kitoto ni kuwa yeye kinatii amri zote hakijui kwanini, mpaka pale kipate fahamu, Lakini wewe umetii Amri hii unajua kwanini na faida zake zipi, Na miongoni mwa faida kubwa uliyoijua katika mwezi huu ni huo Ucha Mungu.
Ucha Mungu sio (Temprorary) kama tunavodhani, Ramadhan ni mtego wa kuonjeshwa hiyo Taqwa, na kama utaipenda basi utadumu nayo milele na kama utaiwacha hilo litakua shauri lako, siku ya kukutana na Mollah wako. Tunamzungumzia mtoto ili tupate mfano wa wewe kuweza kujilinganisha na kujijua nini msimamo wako kuhusiana na hii Taqwa. Mtoto anapokua mkubwa lazima atoke nje akutane na mambo haya na yale, vishawishi hivi na vile, hutoka akaivuruga dunia mpaka itakapomaliza kumfunza mambo ya kilimwengu na kupata akili, hapo hurejea nyumbani kwa wazee jamani nimetubu, sasa nisameheni, ni utundu sitofanya tena, sasa narejea sitokua nunda tena, mimi nitakua mtoto mzuri, na wewe hali kama hiyo, mwezi huu umerejea nyumbani, Umekaa vizuri katika himaya ya Mollah wako, mwezi huu wewe umepata mafunzo mazuri ya Ucha Mungu. Mwenye enzi Mungu anakupa vitu viwili kwa pamoja katika Mwezi huu, cha kwanza ni hiyo Swaum(Awareness) unakua unasikia njaa, unajijua umefunga, hunywi maji, unajizuia na machafu na mengi mengineyo, na ya pili anakupa huo Ucha Mungu (Taqwa-Love)Unapata Rehma, unakua mpole, unafanya Ibadah, unasaidia wasojiweza, unaonea huruma wenzio, unatoa sadaka na zaka, hivyo ndio kurejea nyumbani, Sasa jiulize kwanini unataka kutoka nyumbani, nini unakifata duniani?unataka kufunzwa na ulimwengu tena, kwanini hubakii kwa Mollah wako ukajiunga na Wacha Mungu.
Vipi Utajiunga? Hakitakiwi kitambulisho wala kadi ya ukaazi, hautakiwi Uraia, cheo wala tamaa ya kitu, Kiburi hakikubaliwi, wala mapenzi ya Mali, hutakiwi kujionesha wala kujificha, kinachotakiwa ni (natural)yako na Utiifu wa kukubali kwa njia ya Imani ya kwamba yupo aloniumba na yeye ndie muangalizi wa kila jambo langu.Vipi niingie kwenye (Taqwa)? Naungalia mfano wa Kuamini kwa ushahidi kuwa Mwenye enzi Mungu ndie aliyemuumba Ndege ikisha akampa fahamu kujenga Makaazi yake kwenye Mti, Akamfahamisha taratibu na njia za kujipatia Riziki, Na anaposhikwa na maradhi basi yeye Mollah wako ndie mwenye kumponesha, na akimpa vitoto huvitizama kwa mapenzi vitoto vyake wala havikimbii kama ufanyavo wewe, basi ikiwa kampa fahamu zote hizo nakuomba uelewe na pia kampa na fahamu za kuweza kumsabahi na anatii ndege huyo na kuishi kwenye Taqwa ambayo wewe unasubiri uikimbie pale mwezi tu unapoandama,
Ikumbuke sura ya Nur aya ya 41 inasema nini,
"أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يُسَبِّحُ لَهُ ۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱلطَّيۡرُ صَـٰٓفَّـٰتٍ۬ۖ كُلٌّ۬ قَدۡ عَلِمَ صَلَاتَهُ ۥ وَتَسۡبِيحَهُ ۥۗ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِمَا يَفۡعَلُونَ"
"Je huoni kwamba Mwenye enzi Mungu vinamtukuza vilivyomo mbinguni na ardhini, na ndege wakikunja mbawa zao, Kila(mmoja)amekwisha kujua sala yake na namna ya kumtukuza kwake, Na Mwenye enzi Mungu ni mjuzi wa wanayaofanya"
Hukuti ndege anadhulumu au ana zini, au kugombana na Rafiki zake, Lakini sasa twende tukamhudhurie Khalifa mwenyewe uone visa vyake, Mtizame vipi ukimalizika mwezi huu anavotupa vilemba na kofia, anavochana hijab na majuba. Endelea part 2

KWAHERI RAMADHAN KARIBU UCHA MUNGU PART 2
Asalaam Aleiykum,
Hebu sasa mtupie macho khalifa anapotoka nyumbani na huku Ramadhan ishakwisha anakuaje kiumbe huyu, vipi inakua hali yake, jambo la mwanzo, anavua kilemba anavua hijab kisa Ramadhan imekwisha na sasa anageuka (Toto Nunda)anatoroka Nyumbani, anatoka Mwenyewe Peponi, hasubiri kufukuzwa, kwani kuishi kwenye Taqwa, ni kuwa kwenye pepo ya Ulimwengu huu, na ukitoka kwenye Taqwa inakua ushachupa mwenyewe kwenye matatizo, umejitia mwenyewe kwenye majanga, tizama vipi ukitoka kwenye Taqwa na kurejea kwenye mambo yako unavokuwa.
Al-Rum 41.
"ظَهَرَ ٱلۡفَسَادُ فِى ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ بِمَا كَسَبَتۡ أَيۡدِى ٱلنَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعۡضَ ٱلَّذِى عَمِلُواْ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ"
Uharibifu umedhihiri Bara na baharini kwa sababu ya yale iliyofanya mikono ya watu, ili awaonjeshe (Adhabu kwa) Baadhi ya mambo waliyoyafanya, huwenda wakarudi.
Kila mwaka unapewa nafasi ya kurudi lakini wapi kila ukirudi unatoroka tena, na kila ukitoroka unazidisha kupita yale ulofanya mwaka jana, Eti sasa ndio umefika wakati wa kuandaa(Picnic on the Boat)yanafanyika haya katika bahari na nchi kavu, kuna wengine kidogo wanaogopa labda (Boat)itazama wao wanaamua kufanya ufukweni mwa Bahari(Beach Party) tunapokea habari mambo makubwa yanatokea huko, yanotokea huko kama watafufuliwa watu wa (Sondoma na Gomora)watatoka machozi waseme sisi hatukufanya kiasi hiki, kipi? Naam tunasikia bwana kuna (Kanga Party) eti anokwenda huko hana ruhusa ya kuvaa chengine chochote mwilini mwake, isipokua hiyo kanga, hebu sasa fikiria katoka mwanao au rafiki yako au jirani yako na kanga moja tu, jee imenyesha mvua au kimekuja kimbunga mtu huyo anarejea na hali gani iwe nyumbani au kwa Mollah wake, wewe ndie mwenye kufikiri, itizame hali hiyo iwe mvua ya mafuriko au kimbunga cha kuangamiza (Usiwaze mambo machafu umo kwenye Ramadhan-alaa) nini habari yetu sisi tunao kaa kimya tukafurahia mambo kama hayo, huku tunashuhudia ufisadi unavozidi, vipi itakua Akitumwa Sayyid Jibril a.s atapokuja utamwambia mimi nilikua naogopa kusema, basi ikiwa ushachoka kusema, au uvivu umekushika kumbuka Nabii Nuhu a.s alikumbusha takriban miaka 850 na wala hakuchoka, mpaka akaambiwa sasa tengeneza jahazi ukimbie, duh imekua hivi, na wewe sema mpaka jahazi lako la mauti likifika upate kukimbia, ukiona mtu anafanya maasi usikae kimya kamzindue, nenda kamkumbushe, usimlazimishe anataka kukumbushwa, ukiona mtu anapokea rushwa nenda kamkumbushe hataki waambie askari hufanyi kosa unamnusuru na moto, huwezi kumchongea piga kelele huyu ananidai rushwa na mimi sina, nenda kwa mkubwa wake ukaangushe kilio umwambie nyote mnanidhulumu, usichoke hiyo ndio iwe kazi yako, na unayajua malipo yake, kila ukimuonya na wewe unaandikiwa thawabu za kukataza maovu na huku unasamehewa, nenda kachukue zawadi za bure za kukataza maovu uende peponi.
Ewe ndugu yangu kama umefaidika na hayo sasa nakutaka uzame kwenye maneno yangu ili nitie mbegu Adhimu kwenye moyo wako, na kama utafanikiwa kuiotesha kwenye moyo wako itakua umefanikiwa mafanikio makubwa sana, na wala hutotaka kukimbia kwenye Taqwa, utajiuliza mwenyewe kwanini unakimbia maisha ya Taqwa wakati ndio (Nature) yako. Endelea part 3
KWAHERI RAMADHAN KARIBU UCHA MUNGU PART 3
Asalaam Aleiykum,
tizama mapenzi ya Mwenye enzi Mungu yanavomiminika juu yako, kakupangia (Circle)Maalum, kama utaifata kwa utiifu utakua huna mashaka katika maisha yako, na hiyo ndio (Taqwa), Kwanza kabisa jiulize umetokea wapi?(Original)yako. Umetokea kwake yeye Mollah wako, Kwa mapenzi yake kakuumba mwanaadamu akakufanyia njia ya kuja katika Ulimwengu huu kupitia kwa wazee wako, Akakuweka kwenye Tumbo la mama yako miezi 9, ukawa (KKB)kula na kulala bure, (Al-mursalat 21)"فَجَعَلۡنَـٰهُ فِى قَرَارٍ۬ مَّكِينٍ" "Ikisha tukayaweka mahali pa utulivu"
Huna hofu mpaka siku ya kutoka tumboni na kuja duniani, hapo tena kwa mapenzi makubwa anakukabidhi kwa wazee wako wawili, anawatia mapenzi wanakulea kwa mapenzi makubwa na uangalifu, na unapofikia ujanani anakuongoza Mollah wako ukapata mwenzio wakupendana katika ndoa yenu, akakupeni kizazi ikisha ukiwa mtu mzima anawatia mapenzi kizazi chako cha kukupenda na kukutizama kwa mapenzi na huruma kubwa, Na wewe kama una Imani utajua toka mwanzo mpaka mwisho, umo kwenye (Taqwa)au mapenzi ya kuenziwa kiumbe wewe, kwanini leo Mwenye enzi Mungu kakurejesha katika hiyo Taqwa na wewe unajiandaa kutoka tena. Basi kabla ya kutoroka nyumbani izingatie aya ya 70 sura ya Bani Israel inakukumbusha nini?
وَلَقَدۡ كَرَّمۡنَا بَنِىٓ ءَادَمَ وَحَمَلۡنَـٰهُمۡ فِى ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ وَرَزَقۡنَـٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَـٰتِ وَفَضَّلۡنَـٰهُمۡ عَلَىٰ" ڪَثِيرٍ۬ مِّمَّنۡ خَلَقۡنَا تَفۡضِيلاً۬"
"Na hakika tumewatukuza wanaadamu na tumewapa vya kupanda barani na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewatukuza kuliko wengi katika wale tuliowaumba kwa utukufu ulio mkubwa"
Kwanza kabisa aya imeanza kwa kutukuzwa, wewe special lakini maskini hujijui, halafu ukapewa vya kupanda vya Bara na Baharini ili usihangaike, na tafauti ya kupewa na kuruzukiwa moja imefichikana na nyengine inaoneka kupewa ni (Form) Kuruzukiwa ni (Formless) Kupewa ni (Known) kuruzukiwa (Uknown) Kupewa ni (System)Maalum, Kuruzukiwa ni (Indivisual) hiyo ndio (Life) ilivyo, asizuke mtu na kusimama hichi haramu kile haramu, umeruzukiwa vitu vizuri tena vya kila aina, furahia wala usijikere ila usivuke mipaka, na wewe mwenye kuijua unajua hichi kibaya na hichi kizuri, umepewa utajiri shukuru ufurahi nao, utendee wema utajiri wako, umepewa uzuri furahi Mollah kanichagua mimi niwe zaidi basi ondosha kiburi, umepewa elimu furahi umechaguliwa wewe, sio unapita soda haramu, simu haramu , inakua Sheikh (Full of Haram) haijaja dini kukupiga marufuku kuishi, ishi lakini kama umo kwenye Swaum, Ishi ukiwa na Taqwa yako, hiyo ndio dini, sio kusema TV haramu ukiipata kwa siri unatizama (Programme)yote huo unafiki, napia napenda ujue hakuna makosa kuwa tajiri makosa kumsahau Mollah wako, na kwanini uyakanushe maneno hayo ya vitu vizuri, wakati wewe katika maisha yako ni vingi vizuri ulivokutana navyo kuliko vibaya, kwa sababu wewe malezi yako yote unalelewa kwenye hiyo Taqwa ya Mwenye enzi Mungu, sasa jichunguze maishani mwako yote ulosikia na kuona mengi yepi mazuri au mabaya? jee hivyo vya harufu ulivonusa vipi vingi vibaya au vizuri? ikisha kukujulisha zaidi kama unaishi ndani ya Taqwa Mollah wako kwa Mapenzi akakufundisha elimu ya kila aina mpaka ya kumjua yeye kwenye ulimwengu huu, ili akupe yakini ya kuwepo kwake, akakufanya uwe (Master), Mtukufu kila kilichomo kwenye Ulimwengu huu anakufungulia siri zake, kwa kukujulisha elimu zake kimoja baada ya chengine, na vyote hivo umevimiliki kwa ujuzi, vipi leo wewe unakimbia katika jumba la Taqwa.
Hayo kwa ufupi ndio mapenzi ya Muumba juu yako, hiyo ndio Taqwa ambayo umeshajiandaa kuikimbia siku itakapo malizika Ramadhan, Na Taqwa ishakwisha. Mollah wako hakutaka chochote kutoka kwako isipokua anakwambia nirejeshee mapenzi kwa kuniabudu na kufata amri zangu, kwani kama hunitii amri zangu na kufanya Ibadah na unaendelea kufanya maovu basi huwezi kunipenda mimi, sasa yaangalie majibu ya Kiumbe kilichofanyiwa hayo yote kinakuja na majibu yepi. Endelea part 4 uone manyago.

KWAHERI RAMADHAN KARIBU UCHA MUNGU PART 4
Asalaam Aleiykum,
Ananyanyuka Sheikh Mzima anakwenda kula futari iliyotaarishwa na Bank, nini habari ya Waumin, mnaitukanisha Taqwa ya Mwenye enzi Mungu ndani ya mwezi huu, hivyo kweli nyinyi Waumin wa Dini gani,(Na Ewe Sheikh) kwani hamfahamu Bank, Inakula Riba, Bank inadhulumu, Bank inanyanganya Mali na nyie mko ndani ya Mwezi wenu Mtukufu, basi kama hamjui hamjayasikia maneno ya (Yesu)(jesus) Nabii Isaa a.s katika (Gospel ya Matthew 21:12-13)
"Alipowaendea wabadilishaji pesa na Kuwaambia" Imeandikwa kwenye kitabu"Nyumba yangu itaitwa nyumba ya Ibadah""Lakini mumegeuza chaka la wizi". Na nyinyi ndani ya mwezi mtukufu mnakwenda kushirikiana na wezi, tunaweza kuwasamehe wanasiasa na wafanya Biashara sababu wamejaa unafiki, lakini na nyinyi Masheikh na Waumin hivyo mnaichafua Dini kiasi hichi, na huku umejivika cheo cha Usheikh, sasa ikiwa Sheikh ndio hali hiyo nini habari ya hao wanomfata Sheikh, maradhi makubwa yameingia katika jamii, dini inaondoka kabisa katika mioyo ya watu, na hivi ndivo tulivojitaarisha kutoka kwenye Taqwa pale tutakaposikia mwezi umeandama. Basi ikiwa unataka kubaki katika ucha Mungu kwanza kabisa yakumbuke mambo haya manne yanokufanya uukimbie Ucha Mungu.
Mambo yenyewe ni haya (Mali, Sex,Ulimi, na Tamaa) kama unataka uwe Mcha Mungu jikinge sana kuyashiriki mambo hayo, yasije yakakutoa katika zile siku za mwanzoni tu ukafukuzwa kwenye ufalme wa Mwenye enzi Mungu, Na kikubwa kinachofanya mambo haya ni kukusahaulisha njia ya Mollah wako nayo ni njia ya Taqwa.
Sasa Unajiuliza mimi nataka nibakie kwenye Taqwa nifanye nini?
Mollah wako kwa kuwapenda waja wake kawaletea vitu viwili ndani ya Ramadhan, lakini si watu wengi wenye kuvielewa, viwili hivyo ni (Swaum na Taqwa)Swaum ni yenye kukuweka kwenye (Awareness) ndio maana unaona njaa (siku zote njaa huijui ni nini)unajizuia kula na kunywa, unajikinga na matusi, na maasi yote hiyo ndio (Awareness) halafu ukishakua makini kwa hayo yote unateremshiwa (Love) Taqwa, Mapenzi, nimefunga kwa ajili ya Mollah wangu, mie namuheshimu na kumuogopa Mollah wangu, najizuia na kutii amri za Mollah wangu, hapo tena inakushukia upole na huruma, imani ya kuwasaidia wenzio na mengi mengineyo mazuri mazuri na hiyo ndio Taqwa na hayo ndio Mapenzi, sasa ikisha Ramadhan unatakiwa viwili hivyo ubakie navyo na ukishindwa viwili basi japo kimoja, ikiondoka (Awareness)bakia na (Love)ikiondoka Swaum bakia na Taqwa, Na najua tabu sana kubakia na Swaum (Awareness) lakini unaweza kubakia na Taqwa, na hapo yanatakiwa mabo haya manne ukiyaweza utaupata Ucha Mungu pasi na shaka yoyote, mambo hayo ni (Simplicity+Humility+Devotion Equal Remeberence)
Nini (Simplicity)?Sio kosa kumuomba Mollah wako chochote, lakini ukimwachia akupe mwenyewe hiyo ni (Simplicity). (Humility) ni kuwa kiongozi lakini ukawa mtiifu na kujihisi mtumishi sawa kwa wote hiyo ndio (Humility). (Devotion) kama vile unavosali wakati wa shida ndio iwe hali yako wakati wote kwa ajili ya Mollah wako, na hiyo (Rememberence) unakutana nayo kwenye Sura ya Aaraf aya 205,
"وَٱذۡكُر رَّبَّكَ فِى نَفۡسِكَ تَضَرُّعً۬ا وَخِيفَةً۬ وَدُونَ ٱلۡجَهۡرِ مِنَ ٱلۡقَوۡلِ بِٱلۡغُدُوِّ وَٱلۡأَصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡغَـٰفِلِينَ "
Na Mtaje Mollah wako moyoni mwako kwa unyenyekevu na khofu na bila ya kupiga makelele katika kauli, mkumbuke Mollah wako (Umtaje)asubuhi na jioni, wala usiwe miongoni mwa walioghafilika.
Hapo ndio kwenye Taqwa yenyewe, hiyo ndio ile mbegu nilokwambia kama itaota moyoni mwako wewe mcha Mungu, ukiwa jela, ukiwa mahabusu, ukiwa kazini, ukiwa nyumbani, ukiwa University ukiwa mpirani, ukiwa popote pale isikutoke fikra hii ya Mollah, Elewa wakati wote wewe upamoja na Mollah wako, kidogo kidogo utakua unaitwa Nyumbani na ukifika Nyumbani wewe umefuzu, ukiwa Mkutanoni upo na Mollah wako, Ukiwa Harusini upo na Mollah wako, Shetani akikukaribia anayayuka, na umkumbuke wakati wote wala huna haja ya kujijulisha mimi Mcha Mungu, mimi nina msimamo, mimi hivi, mimi vile laa kimya kimya wala hupigi kelele, wala usije ukaghafilika, kumbuka ukighafilika ina maana umesahau, na ukisahau shetani kafika anakupa jina lake, anakupa mambo yake, unajiunga na kabila lake. huko ndiko kubaki kwenye Taqwa. Namuomba Mollah wetu atudumishe daima katika Ucha Mungu, atukurubishe sisi na watu wema, atupe yalo mazuri ya duniani na akhera, atuondoshee tamaa ya haya maisha ya muda hapa duniani, Mollah wasamehe wazee wetu, uwasamehe Ndugu zetu, wasamehe viongozi wetu, wasamehe maadui zetu, wasamehe masheikh zetu, wasamehe walotukosea, wake na waume, walo hai na walokufa utupe sisi fadhila za mwezi huu mtukufu kama ulivo wapa Waumin wako walotangulia kabla yetu. Tuteremshie Amani ilojaa Rehma zako, utujaalie sote tuwe waja wa Peponi. Amin.

Subscribe to:
Posts (Atom)