Asalaam Aleiykum,
Ukiishi Maisha ya Dini unakua usharejea Nyumbani kwa Mollah wako, Na ukirejea Nyumbani unarejeshewa jina lako la asilia, lipi hilo jina lako la Asili ? Al Furqan 63.
"
"وَعِبَادُ ٱلرَّحۡمَـٰنِ ٱلَّذِينَ يَمۡشُونَ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ هَوۡنً۬ا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ ٱلۡجَـٰهِلُونَ قَالُواْ سَلَـٰمً۬ا"
Na Waja wa Mwenye enzi Mungu, Ni Wale wanokwenda Ulimwenguni kwa unyenyekevu, Na wajinga wakisema nao huwajibu Salama.
Naam, Yametajwa maneno makubwa hapo kama utayazingatia unaweza kupata faida itakayokua taa yako ya muongozo katika kurejea kwako katika dini. Hakiki sisi sote ni Viumbe wa Mwenye enzi Mungu, lakini kuwa Mja ni daraja nyengine, Nani Mja?
Mja ni yule ambaye Imemjia Hekima(Wisdom) akaikubali na kugundua kwamba mimi niko Ngambo ya Pili, natakiwa nirudi katika Dini nifate Amri zote, Akagundua kwamba mimi Mwenyewe nimeumbwa kutokana na Utiifu wa Billion za (Cells)kila moja inafanya kazi yake kutokana na Maamrisho ya dini ili kunifanya mimi niwe Hai.Na Amri hii ikikatika mimi baada ya nusu saa naanza kunuka, nakera wenzangu, hao wanakwenda kunifukia futi 6 chini ya ardhi, wanaweka na ubao hata nikiamka nisiweze kuja juu, Mwenye kugundua hayo, anaelewa sasa kila kitu katika Ulimwengu huu ni Dini, Kinafata Amri za yule aliyekiumba, anakuaje huyo alopata Hekima hii(Wisdom).
Anatembea kwenye Ardhi hii kwa Unyenyekevu(Simple) anajua umuhimu wa kuishi kwa muongozo wa Dini, Dira na Ramani inakua ni Dini yake, anajijua yeye yuko hapa kwa muda mchache, anajua dini ni yenye kudumu kwa hiyo anaamua kuwa na hizi sifa nne (4), anakua Muangalizi wa Wanyonge(1) mambo yote ya Maskini ni mwenye kuyashughulikia bila ya Kiburi wala kutaka sifa,(2)Anakua msafi wa Moyo, na Mtu wa Salama kila mmoja anaweza kumkabili na kumwambia shida zake, (3) Anakua Mnyenyekevu kwa Binaadmu wenzake, (4) Na Mwenye kukihurumia kila kiumbe na kukitakia Salama kwenye Ulimwengu huu, akipata Mja sifa hizo anaipata hiyo(Simplicity) na moja kwa moja anarejea Nyumbani na kuwa Mja wa Mwenye Enzi Mungu, Zinamuondoka Hamaki au hasira, unamteremkia Upole, na hata akikutana na (Ignorance) wakawa wanamkejeli na kumcheka yeye anakua kashapata kitu adhimu sana Moyoni mwake, yote wanayoyasema anawajibu kwa Usalama, anawaombea (Peace upon you) Salama iwe juu yenu, mpate kama niloyapata mimi ya kurejea kwa Mollah wangu, na huku tu ndio kwenye hiyo Salama. Hiyo ndio Dini kila kitu kimo ndani ya Dini, kimezungukwa na Dini, mwanzo dini mwisho dini, kutokana na hiyo Dini ndio ikapatikana Ibadah, kwa hiyo Waja wa Mwenye enzi Mungu wameruhusiwa kufanya Shughuli zao kama zilivopangwa na utaratibu wa Dini, Ikisha wakimaliza hizo Shughuli, basi wanatakiwa hapo hapo kurudi Nyumbani, nenda ofisini, nenda kafanye biashara, toka ukalime, katembelee watu nk, lakini ukimaliza unasubiriwa na aya hii Ash Sharh aya ya 7
"فَإِذَا فَرَغۡتَ فَٱنصَبۡ" Basi ukishamaliza(Yalokushughulisha)Shughulika (Na Ibadah) Na kama utakutana na Mja wa Mwenye enzi Mungu utaona mabadiliko fulani, kula kwake Ibadah, mpaka kulala kwake Ibadah, kusema kwake Ibadah, na hizo Ibadah ziko unazozifanya kwa hiyari na zengine zinatendwa kwa Mpangilio wa Dini Inavotaka kutokana na Amri ya Mollah wako, (Mfano)kama vile kuvuta pumzi, kusaga chakula na mengi mengineyo hayo yote yanafanywa kwa ajili ya Amri ya Mollah wako na hiyo ndio dini ilokizunguka kila kilichomo kwenye Ulimwengu huu, usije ukakerwa na Akili yako ukadhani Dini ni Ibadah, Ibadah ni tendo ndani ya Dini, Dini ni kila kitu kilichomo Ulimwenguni ukivipenda na kuvitunza na kuvithamini, basi utakua umo ndani ya dini, Siasa, dini, Uchumi dini, ndio maana utaona nchi hii inapewa mafuta, huku kunagunduliwa gas, kule kuna madini, hapa kuna hichi na kile mambo yote yanasimamiwa na mfumo wa Dini, chochote kile ukitendacho kimo ndani ya dini, ila anakuja Shetani kukutoa katika Uangalizi wa Dini, ndio maana Waumin mnakumbushwa katika sura ya Baqarah aya ya 208
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱدۡخُلُواْ فِى ٱلسِّلۡمِ ڪَآفَّةً۬ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٲتِ ٱلشَّيۡطَـٰنِۚ إِنَّهُ ۥ لَڪُمۡ عَدُوٌّ۬ مُّبِينٌ۬
"Enyi Mloamini ingieni katika Uislam (Kwa)Ukamilifu, Wala msifate nyayo za Shetani, kwa hakika yeye kwenu ni adui (aliye wazi)Dhahir"
Msikubali kutoka katika dini, kubalini kwa ukamilifu yote alokupangieni Mollah wenu, furahini na kila kilichomo katika Ulimwengu, Msikubali kutoka Nyumbani na kufata nyayo za Shetani hakika yeye nia yake ni kukupotezeni, ili msahau kuwa nyinyi metokea Nyumba ya Dini na mnatakiwa mrejee muishi maisha ya salama ndani ya Dini, na hapo ndipo hapana mwanzo wala hapana mwisho, ila maisha ya milele yenye kheri na neema.Ambayo tunamuomba Mollah atujaalie sote kwa uwezo wake.
No comments:
Post a Comment