Asalaam Aleiykum,
Unakijua chombo cha Wanasayansi au Mapolisi kinachoitwa(Heat Seeking Equipment)Chombo hichi kina uwezo wa kukujulisha wewe mwanaadamu iwapo utakua umejificha popote pale Ulimwenguni, hicho ndio chombo wanachoringia wanasayansi wa kidunia kuhusu ugunduzi wao wakuijua hiyo (Energy)inayotoka kwenye Maumbile ya Binaadamu au kwenye chombo chochote kinachotoa (Heat). Na wanasayansi wa Ulimwengu ulojificha(Mystical)Ulimwengu ambao wewe huuoni mpaka fadhila zikushukie au upate mafunzo Maalum yalombatana na Taqwa, katika Ulimwengu huu wa (Mysticism) wao pia wamegundua kuna (Energy)Maalum inatokea iwapo Mja atajifunga na vitendo vya Ibadah, Na kwanini isiwe hivyo wakati leo Jambazi likikimbia usiku wa manane likajificha linaonekana lipo wapi, nini habari yako wewe unayenyanyua hatua kujifunga kwa nia kuelekea Msikitini kwenda kufanya Ibadah, nani anayekuona wewe?.
Itupie macho kwa makini habari hii tunayozungumza ili upate faida ya kwenda kuzisali Sala zako Msikitini, Usije ukaanza kusoma halafu kuja na tafsiri zako, itakupita maana ya Darsa hii, Sababu kila mtu ana tafsiri yake anavosoma au kuona mambo, na ukitaka kujua vipi tafsiri zinavoondoa maana kihudhurie kisa hichi cha Fundi wa Kibaniani, Baba na Mtoto wake,halafu uone vipi kila Mtu anavo fahamu atakavyo yeye, "Kuna siku kati ya masiku Zama hizo za zamani katika Mji wa Unguja""Mzee Fulani alikua anadaiwa na Fundi wa Kibaniani kwa ajili ya utengenezaji viatu""Mara akapiga hodi yule fundi viatu, Baba aliposikia Mlango unagongwa akamwita Mtoto wake(Itizame tafsiri ya kuona, kusema, na kusikia inavobadilika) na kumwambia kama fundi viatu basi mwambie Baba katoka""Yule Mtoto akatoka mbio mpaka Mlangoni akamwambia fundi viatu, Baba anasema Katoka""Baniani akatizama chini kizingitini akaviona vile viatu alivotengeneza""Na yeye akajibu""Mwambilishe Bana Kuba, kama siku pili tatoka sisahau Guu yake"Naam hivi ndivo kila mtu akisoma darsa zangu anatia tafsiri yake, namie nakwambieni Msisahau kwamba hizo ni tafsiri zenu sio zangu, na ukija namna hivyo utakosa faida, inabidi ukiondoka (Sisahau Guu yako)maana si (Tafsiri)yangu mie, njoo (Open) wacha Darsa iingie ilete (Transformation) upate badiliko fulani, ukiona haifai niachie mwenyewe.
Naam sasa turudi nyuma tupate kuijua hii (Energy) inatokea wapi? na nini dhumuni lake?.Kwanza inabidi ukumbuke unapotaka kubeba kitu kizito au kufanya kazi ngumu inabidi vipatikane vitu vinne Muhimu vifatavyo ili uweze kutekeleza hilo tendo (Chakula, Afya, Nguvu, na Akili Timamu) ili upate kubeba Begi moja la kilo hamsini tu, vikikosekana viwili katika hivo kazi haifanyiki, unajua Kwanini? Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment