Sunday, August 4, 2013

KWAHERI RAMADHAN KARIBU UCHA MUNGU PART 1

Asalaam Aleiykum,

Pata habari ya kitoto kichanga kinapozaliwa na wewe ukajua kwamba kinyanginya chako au kitukuu chako kimekuja kwenye Ulimwengu huu kikiwa safi, na vimacho vyake vyeupe, chakula chake cheupe, ambacho ni maziwa hayana doa wala dosari, kitoto hicho kinakua kinategemea kila kitu kufanyiwa na wazee wake mpaka kitapofikia umri wa kujiweza au kupata fahamu na kuanza kupinga yale yote anoamrishwa na wazee wake, hiyo ndio kawaida yetu sote, hiyo ndio njia tunayopita kila mmoja wetu. Kumbuka na wewe umepita katika hali kama hiyo katika mwezi huu wa Ramadhan, Tafauti yako na hicho kitoto ni kuwa yeye kinatii amri zote hakijui kwanini,  mpaka pale  kipate fahamu, Lakini wewe umetii Amri hii unajua kwanini na faida zake zipi, Na miongoni mwa faida kubwa uliyoijua katika mwezi huu ni huo Ucha Mungu.
Ucha Mungu sio (Temprorary) kama tunavodhani, Ramadhan ni mtego wa kuonjeshwa hiyo Taqwa, na kama utaipenda basi utadumu nayo milele na kama utaiwacha hilo litakua shauri lako, siku ya kukutana na Mollah wako. Tunamzungumzia mtoto ili tupate mfano wa wewe kuweza kujilinganisha na kujijua nini msimamo wako kuhusiana na hii Taqwa. Mtoto anapokua mkubwa lazima atoke nje akutane na mambo haya na yale, vishawishi hivi na vile, hutoka akaivuruga dunia  mpaka itakapomaliza kumfunza mambo ya kilimwengu na kupata akili, hapo hurejea nyumbani kwa wazee jamani nimetubu, sasa nisameheni, ni utundu sitofanya tena, sasa narejea sitokua nunda tena, mimi nitakua mtoto mzuri, na wewe hali kama hiyo, mwezi huu umerejea nyumbani, Umekaa vizuri katika himaya ya Mollah wako, mwezi huu wewe umepata mafunzo mazuri ya Ucha Mungu. Mwenye enzi Mungu anakupa vitu viwili kwa pamoja katika Mwezi huu, cha kwanza ni hiyo Swaum(Awareness) unakua unasikia njaa, unajijua umefunga, hunywi maji, unajizuia na machafu na mengi mengineyo, na ya pili anakupa huo Ucha Mungu (Taqwa-Love)Unapata Rehma, unakua mpole, unafanya Ibadah, unasaidia wasojiweza, unaonea huruma wenzio, unatoa sadaka na zaka, hivyo ndio kurejea nyumbani, Sasa jiulize kwanini unataka kutoka nyumbani, nini unakifata duniani?unataka kufunzwa na ulimwengu tena, kwanini hubakii kwa Mollah wako ukajiunga na Wacha Mungu. 
Vipi Utajiunga? Hakitakiwi kitambulisho wala kadi ya ukaazi, hautakiwi Uraia, cheo wala tamaa ya kitu, Kiburi hakikubaliwi, wala mapenzi ya Mali, hutakiwi kujionesha wala kujificha, kinachotakiwa ni (natural)yako na Utiifu wa kukubali kwa njia ya Imani ya kwamba yupo aloniumba na yeye ndie muangalizi wa kila jambo langu.Vipi niingie kwenye (Taqwa)? Naungalia mfano wa Kuamini kwa ushahidi kuwa  Mwenye enzi Mungu ndie aliyemuumba Ndege ikisha akampa fahamu kujenga Makaazi yake  kwenye Mti, Akamfahamisha taratibu na njia za kujipatia Riziki, Na anaposhikwa na maradhi basi yeye Mollah wako ndie mwenye kumponesha, na akimpa vitoto huvitizama kwa mapenzi vitoto vyake wala havikimbii kama ufanyavo wewe, basi ikiwa kampa fahamu zote hizo nakuomba uelewe na pia kampa na fahamu za kuweza kumsabahi na anatii ndege huyo na kuishi kwenye Taqwa ambayo wewe unasubiri uikimbie pale mwezi tu unapoandama,
Ikumbuke sura ya Nur aya ya 41 inasema nini,

"أَلَمۡ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ يُسَبِّحُ لَهُ ۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٲتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱلطَّيۡرُ صَـٰٓفَّـٰتٍ۬‌ۖ كُلٌّ۬ قَدۡ عَلِمَ صَلَاتَهُ ۥ وَتَسۡبِيحَهُ ۥ‌ۗ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِمَا يَفۡعَلُونَ"
"Je huoni kwamba Mwenye enzi Mungu vinamtukuza vilivyomo mbinguni na ardhini, na ndege wakikunja mbawa zao, Kila(mmoja)amekwisha kujua sala yake na namna ya kumtukuza kwake, Na Mwenye enzi Mungu ni mjuzi wa wanayaofanya"
Hukuti ndege anadhulumu au ana zini, au kugombana na Rafiki zake, Lakini sasa twende tukamhudhurie Khalifa mwenyewe uone visa vyake, Mtizame vipi ukimalizika mwezi huu anavotupa vilemba na kofia, anavochana hijab na majuba. Endelea part 2

No comments:

Post a Comment