Sunday, August 18, 2013

DINI HAINA MWANZO HAINA MWISHO PART 1

Asalaam Aleiykum,

Tunaendelea na Darsa zetu kama kawaida, leo hii kwa kuwa mwezi wa Ibadah umekwisha, miskiti mitupu, safu mbili zinapatikana kwa shida  tena hazitimii, na yule anosali nyumbani anakusanya zote ili asali kwa pamoja umuondoke udhia, kwa kuwa wengi wetu hatujui nini Dini?.
Dini ni haya Maisha yenyewe, kwani nikisema mfumo ntaipunguzia hadhi Dini, Na mfumo una tabia ya kubadilika, lakini dini haibadiliki na wala haina kikomo, maisha hayana mwisho (Life) inaendelea, ndio maana ukaambiwa utafufuliwa siku ya (Qiyama)lakini wewe Binaadamu unao mwisho, ndio utaona mara unaingia mara unatoka katika maisha haya ya Dini, Na unapotoka katika maisha haya ya dini unakua ushachupa katika maisha ya Matatizo wewe mwenyewe, Kwa sababu maisha ya Dini ni Maisha ya (Gurantee) ndani yake hukuti matatizo ila unakuta Mitihani.
Nini Matatizo? Matatizo ni jambo la kujitakia (Mfano) huna pesa, hujui Biashara, ikisha unakopa kufanya Biashara na huku unaweka Nyumba yako Rehani, Biashara ikianguka ushaingia kwenye matatizo, unatafuta pesa za kulipa, njia za kuinusuru nyumba yako, na kubwa zaidi la kuilisha (family) yako, matatizo yanaanzia hapo, na kutoka kwenye matatizo inakua shida kubwa. Lakini kwenye Dini unapata Mtihani, Nini Mtihani? Mtihani ni jambo linalokuja (From Unknown) kutoka kwa mwenyewe Subhanna, na Mtihani una hakika wa kumalizika,(Mfano) Maradhi, unaumwa halafu unapona, umeshikwa na njaa unapewa njia ya kupata chakula, na mengi ambayo ukitulia na kuangalia kwa makini unajua hili mtihani na hili nimejitakia mwenyewe, Kumbuka Mtihani kutoka kwa Mwenye enzi Mungu, Matatizo kutoka kwako mwenyewe.
Sasa nini Dini? Dini ni kitu unachozaliwa nacho, halafu mwenyewe unaamua kutoka katika Dini kwa kuonja tunda la Elimu, tunda la kufahamu, lakini kufahamu huku kwa njia ya (Innocent) kunakupeleka kufanya uchunguzi wa kila kitu, kama alivo mtoto hichi nini, kile nini, ikisha unakwenda katika daraja nyengine ya (Ignorance) unafanya mambo katika Ujana ukiwa hujali matokeo yake wala madhara yake,Maasi kwako inakua jambo la kawaida, Unazama kwenye bahari ya dhuluma na kufanya Unyanganyi, Uongo kwako kawaida, Zinaa na fujo zote unazikabili kifua mbele, na hivyo vyote ni nje ya Maisha ya Kidini, Halafu tena kila mmoja wetu anapata (Chance) Nyengine ya kurejea kwenye hayo Maisha ya Kidini, unapata nafasi ya kurejea kwenye Maisha ulokua nayo mwanzo ya kidini, lakini wakati huu inakushukia hiyo (Wisdom)Hekima, Ujumbe unakufikia unakukuta uko (Choppy)kwa magunia ya Dhanmbi na mashaka na madhila ya Ulimwengu, unafahamishwa Rejea kwenye Maisha anayoridhia yule alokuumba, toka kwenye matatizo, ondoka kwenye moto wa ulimwengu, rejea kwenye bustani(Nyumbani)ulikokimbia.
Inateremka Nusura hii ya Hekima kukujulisha kwamba sasa jua lishakuchwa, acha kuzama kwenye shughuli za watu, usitumie Umri wako mpaka ukataka kukopa umri wa watoto wako, sasa wewe basi, na kutaka kujua kama umefika kikomo utaona dalili mwenyewe mbona wenzangu wamebadilika, mbona wote wanavaa hijab, inakuaje sasa wanahudhuria darsa, mbona disco hawaji tena, mbona harusini hawachezi tena, mbona wamecharuka kushiriki mambo ya kheri, sio kwa kujionesha, kwa sababu ukifanya kwa kujionesha basi jua (Hekima) au hiyo Nusura haijakufika, mabadiliko yapo mengi ya kukujulisha kwamba sasa ushapata taarifa ubadilike, urudi nyumbani ulipotokea, uwe mtu unaeishi maisha ya Kidini, na vipi utajua umesharejea kwenye maisha ya kidini?
Endelea Part 2


No comments:

Post a Comment