Asalaam Aleiykum,
Sasa (Energy) hii inapatikana vipi? Tizama ndani ya Quraan upate jawabu la kuridhisha kabla hujenda Msikitini, Inapatikana Nguvu hii kwa dalili hizi ndani ya Quraan, Kwanza kabisa kuhusu hicho chakula, Abbasa aya ya 24 " فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَـٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦۤ""Hebu Mwanaadamu na atizame chakula chake", vipi kinavokupa nguvu kikajenga Mwili wako ukawa uko tayari kuhimili kazi zako(Yeye Mollah ni Mwenye kukileta hicho chakula na yeye ndie mwenye kukupa hizo Nguvu). Tunajua Akili ni yenye kuchukua 75% ya vitamin ya hicho chakula, sasa tunaelewa Akili inafanya kazi za ziada, kutwa nzima unaandika na kufikiri ndani ya kichwa chako, mara wazo hili, mara wazo lile, hupumziki hata sekunde tano ila wazo lishaingia na lile linatoka, na kwa hivyo inatakiwa Akili yako iwe timamu kupata utulivu wa hiyo (Energy).
Aya ya Mwanzo sura ya Qalam "نٓۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ""Naapa kwa (Akili)Kalamu, Na yale Wayaandikayo kwa (Akili)kalamu hizo""(Lazima uwe na dhamana ya Akili yako ili Uwe Muumin wa kweli).
Ama kuhusu hiyo Afya Al-Shuara aya ya 80" وَإِذَا مَرِضۡتُ فَهُوَ يَشۡفِينِ""
Ninaposhikwa na Maradhi, Yeye ndie anayeniponesha"Hiyo ndio afya, yote ipo kwenye ufalme wake(Yeye Mollah ndie anaekudumisha katika Afya, na ukiwa na Afya unasahau kila kitu, lakini wacha Ukucha tu ukiuma watu wote hawalali kwenye Nyumba, kwa hiyo unaona vipi vitu vyote vimezungukwa na Ufalme wa Mwenye enzi Mungu), na kuhusu nguvu itizame sura ya Ghafir aya ya 2"تَنزِيلُ ٱلۡكِتَـٰبِ مِنَ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡعَلِيمِ" Kuteremshwa kwa kitabu(hiki)kumetokana kwa Mwenye enzi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye kujua".
Ukiangalia aya zote hizo Nne nilizo zitaja maelezo yake yanaashiria Uweza wa Mollah na vyote hivo vinavyoilete hiyo (Energy) vinatokea kwake Mollah wetu, kuanzia Chakula, Akili, Afya, na hiyo nguvu, ndio wewe ukapata uwezo wa kulibeba (Bag moja la nguo) Na ukilinyanua Bag hilo unakua ushapunguza hizo nguvu, mpaka uzitafute tena, Sasa hili la Ibadah inakuaje? Unaambiwa kila Ukinyanyua Mguu unaandikiwa(Thawabu na kuongezewa hizo Nguvu) na ikiwa Nia yako na vitendo vyako vimefungana na dhumuni la Ibadah, basi kila nguvu zinazopungua unapata (Recycle)yake mara (Saba) Sitoweza kuifundisha hadharani siri hii ya kukufanya usichoke, hii ndio walonayo wacha Mungu ukawa unawaona hawachoki kufanya Ibadah, sio kama mimi na wewe tukisali usiku siku tatu tu tunaanza kukumbuka kipenzi chetu usingizi.
Nguvu zenyewe za kunyanyua hatua kwenda msikitini hazitakiwi ziwe zimechanganyika na mambo ya kipuuzi, unapotaka kwenda Msikitini kwa ajili ya Ibadah lazima mawazo yako yote yawe (Intune)Na Ibadah. (Mfano)unakwenda Msikitini uanze kwa Mawazo ya kumsabahi Mollah wako, au kusoma Quraan hapo ndio utakua unatengeneza hiyo (Energy), Lakini kama utaanza safari yako kuelekea Msikitini huku una (Magazine)nzima ya (Love Story) au unakwenda Msikitini na mawazo ya miadi, atakuja saa ngapi, au unapanga vipi utamfanyia fulani Ujambazi, hapo unakua si mwenye kuipata hiyo (Energy)wala Thawabu. Na elewa kila kitu katika Ulimwengu huu kinatengeneza (Energy) ukiwemo na wewe na (Energy) za Ibadah ni zenye kubakia. Endelea part 3
No comments:
Post a Comment