Sunday, August 4, 2013

KWAHERI RAMADHAN KARIBU UCHA MUNGU PART 2


Asalaam Aleiykum,

Hebu sasa mtupie macho khalifa anapotoka nyumbani na huku Ramadhan ishakwisha anakuaje kiumbe huyu, vipi inakua hali yake, jambo la mwanzo, anavua kilemba anavua hijab kisa Ramadhan imekwisha na sasa anageuka (Toto Nunda)anatoroka Nyumbani, anatoka Mwenyewe Peponi, hasubiri kufukuzwa, kwani kuishi kwenye Taqwa, ni kuwa kwenye pepo ya Ulimwengu huu, na ukitoka kwenye Taqwa inakua ushachupa mwenyewe kwenye matatizo, umejitia mwenyewe kwenye majanga, tizama vipi ukitoka kwenye Taqwa na kurejea kwenye mambo yako unavokuwa.
Al-Rum 41.
"ظَهَرَ ٱلۡفَسَادُ فِى ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ بِمَا كَسَبَتۡ أَيۡدِى ٱلنَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعۡضَ ٱلَّذِى عَمِلُواْ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ"
Uharibifu umedhihiri Bara na baharini kwa sababu ya yale iliyofanya mikono ya watu, ili awaonjeshe (Adhabu kwa) Baadhi ya mambo waliyoyafanya, huwenda wakarudi.
Kila mwaka unapewa nafasi ya kurudi lakini wapi kila ukirudi unatoroka tena, na kila ukitoroka unazidisha kupita yale ulofanya mwaka jana, Eti sasa ndio umefika wakati wa kuandaa(Picnic on the Boat)yanafanyika haya katika bahari na nchi kavu, kuna wengine kidogo wanaogopa labda (Boat)itazama wao wanaamua kufanya ufukweni mwa Bahari(Beach Party) tunapokea habari mambo makubwa yanatokea huko, yanotokea huko kama watafufuliwa watu wa (Sondoma na Gomora)watatoka machozi waseme sisi hatukufanya kiasi hiki, kipi? Naam tunasikia bwana kuna (Kanga Party) eti anokwenda huko hana ruhusa ya kuvaa chengine chochote mwilini mwake, isipokua hiyo kanga, hebu sasa fikiria katoka mwanao au rafiki yako au jirani yako na kanga moja tu, jee imenyesha mvua au kimekuja kimbunga mtu huyo anarejea na hali gani iwe nyumbani au kwa Mollah wake, wewe ndie mwenye kufikiri, itizame hali hiyo iwe mvua ya mafuriko au kimbunga cha kuangamiza (Usiwaze mambo machafu umo kwenye Ramadhan-alaa) nini habari yetu sisi tunao kaa kimya tukafurahia mambo kama hayo, huku tunashuhudia ufisadi unavozidi, vipi itakua Akitumwa Sayyid Jibril a.s atapokuja utamwambia mimi nilikua naogopa kusema, basi ikiwa ushachoka kusema, au uvivu umekushika kumbuka Nabii Nuhu a.s alikumbusha takriban miaka 850 na wala hakuchoka, mpaka akaambiwa sasa tengeneza jahazi ukimbie, duh imekua hivi, na wewe sema mpaka jahazi lako la mauti likifika upate kukimbia, ukiona mtu anafanya maasi usikae kimya kamzindue, nenda kamkumbushe, usimlazimishe anataka kukumbushwa, ukiona mtu anapokea rushwa nenda kamkumbushe hataki waambie askari hufanyi kosa unamnusuru na moto, huwezi kumchongea piga kelele huyu ananidai rushwa na mimi sina, nenda kwa mkubwa wake ukaangushe kilio umwambie nyote mnanidhulumu, usichoke hiyo ndio iwe kazi yako, na unayajua malipo yake, kila ukimuonya na wewe unaandikiwa thawabu za kukataza maovu na huku unasamehewa, nenda kachukue zawadi za bure za kukataza maovu uende peponi.
Ewe ndugu yangu kama umefaidika na hayo sasa nakutaka uzame kwenye maneno yangu ili nitie mbegu Adhimu kwenye moyo wako, na kama utafanikiwa kuiotesha kwenye moyo wako itakua umefanikiwa mafanikio makubwa sana, na wala hutotaka kukimbia kwenye Taqwa, utajiuliza mwenyewe kwanini unakimbia maisha ya Taqwa wakati ndio (Nature) yako. Endelea part 3

No comments:

Post a Comment