Sunday, August 4, 2013

KWAHERI RAMADHAN KARIBU UCHA MUNGU PART 4

Asalaam Aleiykum,

Ananyanyuka Sheikh Mzima anakwenda kula futari iliyotaarishwa na Bank, nini habari ya Waumin, mnaitukanisha Taqwa ya Mwenye enzi Mungu ndani ya mwezi huu, hivyo kweli nyinyi Waumin wa Dini gani,(Na Ewe Sheikh) kwani hamfahamu Bank, Inakula Riba, Bank inadhulumu, Bank inanyanganya Mali na nyie mko ndani ya Mwezi wenu Mtukufu, basi kama hamjui hamjayasikia maneno ya (Yesu)(jesus) Nabii Isaa a.s katika (Gospel ya Matthew 21:12-13)
"Alipowaendea wabadilishaji pesa na Kuwaambia" Imeandikwa kwenye kitabu"Nyumba yangu itaitwa nyumba ya Ibadah""Lakini mumegeuza chaka la wizi". Na nyinyi ndani ya mwezi mtukufu mnakwenda kushirikiana na wezi, tunaweza kuwasamehe wanasiasa na wafanya Biashara sababu wamejaa unafiki, lakini na nyinyi Masheikh na Waumin hivyo mnaichafua Dini kiasi hichi, na huku umejivika cheo cha Usheikh, sasa ikiwa Sheikh ndio hali hiyo nini habari ya hao wanomfata Sheikh, maradhi makubwa yameingia katika jamii, dini inaondoka kabisa katika mioyo ya watu, na hivi ndivo tulivojitaarisha kutoka kwenye Taqwa pale tutakaposikia mwezi umeandama. Basi ikiwa unataka kubaki katika ucha Mungu kwanza kabisa yakumbuke mambo haya manne yanokufanya uukimbie Ucha Mungu.
Mambo yenyewe ni haya (Mali, Sex,Ulimi, na Tamaa) kama unataka uwe Mcha Mungu jikinge sana kuyashiriki mambo hayo, yasije yakakutoa katika zile siku za mwanzoni tu ukafukuzwa kwenye ufalme wa Mwenye enzi Mungu, Na kikubwa kinachofanya mambo haya ni kukusahaulisha njia ya Mollah wako nayo ni njia ya Taqwa.
Sasa Unajiuliza mimi nataka nibakie kwenye Taqwa nifanye nini?
Mollah wako kwa kuwapenda waja wake kawaletea vitu viwili ndani ya Ramadhan, lakini si watu wengi wenye kuvielewa, viwili hivyo ni (Swaum na Taqwa)Swaum ni yenye kukuweka kwenye (Awareness) ndio maana unaona njaa (siku zote njaa huijui ni nini)unajizuia kula na kunywa, unajikinga na matusi, na maasi yote hiyo ndio (Awareness) halafu ukishakua makini kwa hayo yote unateremshiwa (Love) Taqwa, Mapenzi, nimefunga kwa ajili ya Mollah wangu, mie namuheshimu na kumuogopa Mollah wangu, najizuia na kutii amri za Mollah wangu, hapo tena inakushukia upole na huruma, imani ya kuwasaidia wenzio na mengi mengineyo mazuri mazuri na hiyo ndio Taqwa na hayo ndio Mapenzi, sasa ikisha Ramadhan unatakiwa viwili hivyo ubakie navyo na ukishindwa viwili basi japo kimoja, ikiondoka (Awareness)bakia na (Love)ikiondoka Swaum bakia na Taqwa, Na najua tabu sana kubakia na Swaum (Awareness) lakini unaweza kubakia na Taqwa, na hapo yanatakiwa mabo haya manne ukiyaweza utaupata Ucha Mungu pasi na shaka yoyote, mambo hayo ni (Simplicity+Humility+Devotion Equal Remeberence) 
Nini (Simplicity)?Sio kosa kumuomba Mollah wako chochote, lakini ukimwachia akupe mwenyewe hiyo ni (Simplicity). (Humility) ni kuwa kiongozi lakini ukawa mtiifu na kujihisi mtumishi sawa kwa wote hiyo ndio (Humility). (Devotion) kama vile unavosali wakati wa shida ndio iwe hali yako wakati wote kwa ajili ya Mollah wako, na hiyo (Rememberence) unakutana nayo kwenye Sura ya Aaraf aya 205,
"وَٱذۡكُر رَّبَّكَ فِى نَفۡسِكَ تَضَرُّعً۬ا وَخِيفَةً۬ وَدُونَ ٱلۡجَهۡرِ مِنَ ٱلۡقَوۡلِ بِٱلۡغُدُوِّ وَٱلۡأَصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡغَـٰفِلِينَ "
Na Mtaje  Mollah wako moyoni mwako kwa unyenyekevu na khofu na bila ya kupiga makelele katika kauli, mkumbuke Mollah wako (Umtaje)asubuhi na jioni, wala usiwe miongoni mwa walioghafilika.
Hapo ndio kwenye Taqwa yenyewe, hiyo ndio ile mbegu nilokwambia kama itaota moyoni mwako wewe mcha Mungu, ukiwa jela, ukiwa mahabusu, ukiwa kazini, ukiwa nyumbani, ukiwa University ukiwa mpirani, ukiwa popote pale isikutoke fikra hii ya Mollah, Elewa wakati wote wewe upamoja na Mollah wako, kidogo kidogo utakua unaitwa Nyumbani na ukifika Nyumbani wewe umefuzu, ukiwa Mkutanoni upo na Mollah wako, Ukiwa Harusini upo na Mollah wako, Shetani akikukaribia anayayuka, na umkumbuke wakati wote wala huna haja ya kujijulisha mimi Mcha Mungu, mimi nina msimamo, mimi hivi, mimi vile laa kimya kimya wala hupigi kelele, wala usije ukaghafilika, kumbuka ukighafilika ina maana umesahau, na ukisahau shetani kafika anakupa jina lake, anakupa mambo yake, unajiunga na kabila lake. huko ndiko kubaki kwenye Taqwa. Namuomba Mollah wetu atudumishe daima katika Ucha Mungu, atukurubishe sisi na watu wema, atupe yalo mazuri ya duniani na akhera, atuondoshee tamaa ya haya maisha ya muda hapa duniani, Mollah wasamehe wazee wetu, uwasamehe Ndugu zetu, wasamehe viongozi wetu, wasamehe maadui zetu, wasamehe masheikh zetu, wasamehe walotukosea, wake na waume, walo hai na walokufa utupe sisi fadhila za mwezi huu mtukufu kama ulivo wapa Waumin wako walotangulia kabla yetu. Tuteremshie Amani ilojaa Rehma zako, utujaalie sote tuwe waja wa Peponi. Amin.

No comments:

Post a Comment