Asalaam Aleiykum,
Tunaingia katika kumi la kuchukuliwa (Dhamana) na Mollah wetu, Dhamana hiyo ni kuepushwa na adhabu za kila aina, zikiwemo za kaburi, adhabu za maisha na ile adhabu kubwa iumizayo ya Moto wa Jahannam siku hiyoo ya Malipo, Lakini jee dhamana hii anaipata kila mtu? Jawabu utalipata ukizama katika darsa hii ili kujijua unastahiki hiyo dhamana, Jee umo katika fungu la walofunga? au unasubiri mshituko gani utaupata ikiwa hesabu zako zote zitaishia katika fungu la walokaa na njaa. Nini habari ya waliokaa na njaa? nakuchukua wewe msomaji ili ufikirie hali gani utakua nayo kama utaalikwa shughuli, upo hapa duniani fulani kakualika shughuli na wewe umehudhuria, Ikisha likatoka tangazo wenye kula biriani wasubiri kwanza, sababu unatolewa wali mweupe, halafu baada ya wali mweupe kumalizika, anatangaza mtangazaji walokula na wasokula nyote ahsanteni kwa kuhudhuria, Jitizame vipi utakua kisa kama hicho kikikutokea na wewe una njaa, na nyakati saa nane za mchana, jua linawaka kwa vishindo, vipi itakua hali yako? hali kama hiyo ndio itatokea siku ya Kiyama pale watapoitwa wale wote walokua wakifunga wapite mlango huu wa Rayyan, na wewe kwa vile unajiamini umefunga unafata, mara unasikia umekamatwa ngozi na (Malaika)unarejeshwa nyuma rudi, huku unadhani mie nilikua nafunga vipi leo mambo haya? ukisema mimi nilikua sili wala sinywi, unajibiwa hiyo ilikua sio saumu, wewe ulikua ukifanya(Diet).
Nani Walofunga?
Walofunga ni wale ambao walikua wakifanya (Taqwa)ipasavyo, Na yoyote yule alofanya Taqwa ikatimia kikweli hana haja ya kujijua, ukiona unaanza kujiuliza jee mimi nimefanya Taqwa basi jitilie wasiwasi, na ufanye haraka kufata muongozo wa darsa hii huko mwishoni ili uipate hiyo Taqwa. Mwenye kufunga kweli hana haja ya kujua kakubaliwa au kakataliwa, yeye huyo anakua kazama katika hisia za Taqwa na ana fahamu alitendalo kama anavofahamu hili jua, huu mwezi, na huu mchana, hana haja ya yeye kuambiwa huu mchana, sasa hivi wewe umacho, ukiwa macho moja kwa moja unajijua mimi ni macho, na kama hivo ndio anavojijua mtenda Taqwa, lakini alo lala usingizi yeye ndio hajui nini kimetokea, yeye yupo wapi, na kufunga ndio nini, sasa ikiwa umelala usione uchungu tutakuamsha upate kufunga japo hizo siku kumi za mwisho ili na wewe uipate (Swaum).
Nini Taqwa?
Maana ya Taqwa ni Mapenzi, na mapenzi ni khofu ya kuogopa usimkere Mollah wako aliyekuita katika Mwezi huu Mtukufu wa kumtii yeye ambao ni huu Ramadhan, Sasa jihadhari ikiwa umo katika lile kundi liloshindwa kwanza kabisa kuzuia Macho na mambo yote ya Haramu, (basi wewe utakua miongoni wa wale wenye kutaka kuwajua walofunga) Huna Taqwa, ila una njaa.
Na kama bado unapinga yakua Swaum unayo basi hebu jiulize umempa Mollah wako heshima kwa ajili yake ukajizuia na kujiepusha na maovu haya ya macho. Na katika huko kuona kuna namna mbili ile ya bahati mbaya Mollah wako anaijua, nini habari yako wewe ulofanya kwa kusudi? jee (Umo katika kundi la walofunga)majibu tambua mwenyewe. Wewe bado umebakia katika mwezi wa kula mchana, hujaingia kabisa katika Mwezi huu wa Ramadhan, Ama yule aliyekuwemo kwenye Ramadhan yeye anakua kashaigundua (Switch) na kama huijui hii (Switch) basi wacha nikujulishe ili na wewe upate kuitumia siku za mbele, na kama utaweza kuitumia nyenzo hii itakusaidia sana katika matendo yako ya Kuona, Wewe una (Switch) mbili lakini kwa muda huu huzielewi ziko wapi na zinatumika vipi, kuna hali mbili zinakutokea na ukitaka kuyajua hayo sasa endelea part 2
No comments:
Post a Comment