Sio wema (Taqwa)kugeuza shingo zenu Mashariki wala Magharib katika kusali, tizama ikiwa Sala mwanzo imekataliwa haimo katika (taqwa)mpaka vipatikane viungo vyake, nini habari ya Saumu yako wewe na mimi, Nini wema(Taqwa) Ni Kumuamini Mwenye enzi Mungu, Jee wewe Unamuamini (1)? (Funga Macho kabla ya kuendelea utupe vigezo vyako) Mimi nitakupa kigezo kimoja na vyengine utatafuta mwenyewe.
"Nakuamini Mollah wangu kwa kujijua mimi ni nani na nipo katika Ulimwengu huu kwa ajili gani, Nakuamini Mollah wangu pale ninapoangalia Ulimwengu huu na vyote viliyomo, hususan nikitizama vinyama, awe mdogo au awe mkubwa halafu najitizama na mimi mwenyewe kwa huu Uhai ulotujaalia sote, yananitoka machozi pale ninapoona umetupa sote Fahamu ya daraja kwa jinsi ya uwezo wetu, naona mimi vipi kinyama cha kila aina kinapotafuta Riziki yake na kuweza kujitosheleza, ukawapa fahamu pia yakujitafutia pahala pa kuishi, Ikisha kwa Rehma zako ukavijaalia vyote ikiwemo na mimi hii Neema ya Usingizi kuweza kulala na kuamka, Nautizama mpaka Mti Mollah wangu, nao unakula na kunywa na kulala, na kwa hilo Mollah wangu nasema umetukuka kwa sifa zote zisizo upungufu na mimi sina cha kutanguliza mbele yako isipokua kusema Alhamdullillah.
Nini wema (Taqwa)Kuamini siku ya Mwisho(2) ?(Fumba macho) Kwa ajili ya kuona kwangu katika Ulimwengu huu kila kitu kiko kwa muda, hakuna cha kudumu, kama mimi nilivokuja na kuna siku nitaondoka kama wenzangu walotangulia, hilo limenifikisha kuyakubali maneno yako yaliyomo kwenye sura ya Al-Rahman aya ya 26 "كُلُّ مَنۡ عَلَيۡہَا فَانٍ۬" Kila kilichomo juu yake kitatoweka(Ardhini na Mbinguni), basi kutokana na maneno hayo na matendo yako ya ishara yalodhihiri nina Imani pia kuna mwisho wa haya yote.
Kuamini Malaika (3)? (Fumba macho) Wacha nikuchukue nikupeleke ili ukajue vipi au wapi viumbe hawa unaweza kuwaona au kuona ishara zao kuwa wapo, hayo yote yanategemea wema wako (Taqwa) yako ilivyo, ili kuweza kufungua pazia hilo, usisubiri mpaka siku ya kutoka Roho ukaanza kusema mbona naona mtu kanisimamia, mbona haondoki, huyu nani kasimama,usisubiri kufunguliwa pazia, fungua mwenyewe kwa kuzidisha (Taqwa). Sasa kutana au iyone hiyo kazi ya hao Malaika wawili ili upate kuamini, unaambiwa katika sura ya Qaf aya ya 17"
"إِذۡ يَتَلَقَّى ٱلۡمُتَلَقِّيَانِ عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ قَعِيدٌ۬"
"Wanapopokea (Malaika)wapokeaji wawili, anayekaa kuliani na (anayekaa)Kushotoni"
Hao ndio wanoandika dhanmbi zako au thawabu zako, vipi utawajua ili upate kuamini, hakuna njia nyengine ila ujitizame kama unatenda dhanmbi kwa kusudi, nasema kwa kusudi kwa sababu ya bahati mbaya hutoweza kujua, ikiwa unatenda kosa ukalijua hili kosa, basi tazama upande wako wa kushoto nini kinatokezea katika (Mind)yako angalia sana kuna kitu utagundua, na pia kama unafanya jambo zuri angalia upande wako wa kulia kwenye (Mind) yako nini kinatokezea na vipi unakhisi, ukianza kuyagundua yanotokezea kidogo kidogo utaanza kuamini kumbe dooh kuna viumbe vimeniganda na vinaandika kila jambo.
Kuamini Kitabu chake(4)?(fumba macho) Wengine wanapoambiwa kuamini kitabu basi mbio mbio wanachukua Quraan na kuanza kuibusu kisha wanaitia kwapani huku wanaendelea kama kawaida kutesa wenzao, kudhulumu wenzao, kusengenya wenzao, wanavunja kila sheria iliyomo katika hicho kitabu, Maana halisi ilokusudiwa ya kuamini kitabu ni kuwa na Imani na maneno na amri alokupangia katika maisha haya, kakupa maisha ikisha kakuletea muongozo, sura ya Baqarah aya ya 2"
"ذَٲلِكَ ٱلۡڪِتَـٰبُ لَا رَيۡبَۛ فِيهِۛ هُدً۬ى لِّلۡمُتَّقِينَ"
Hiki ni kitabu kisichokua na shaka ndani yake, ni uongozi kwa wamchao Mwenye enzi Mungu.
Maana ya kuamini kitabu ni kutii na kufata yaliyomo katika hayo maandiko, na hayo ndio maisha alokutakia Mollah wako, umepewa Uhai na ukapewa muongozo wa kuifata njia ilonyooka, lakini ukijifanya jeuri au mjuaji ukachupa na kuingia msituni, basi hapo inakua ushapotea, na msitu kama unavoujua una miti mingi, una wanyama wa kila aina, na inabidi sasa utafute njia yako mwenyewe ili uipate tena njia ilonyooka, sasa katika kutafuta hiyo njia, ndio na wewe inabidi uandike Kitabu chako, lazima uje na Ramani lako la kutoka huko msituni, unatoka huko Simba washakuparura Kitabu kishachanwa, hapo unaambiwa katika sura ya Al Haaqqa aya ya 19"فَأَمَّا مَنۡ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُ ۥ بِيَمِينِهِۦ فَيَقُولُ هَآؤُمُ ٱقۡرَءُواْ كِتَـٰبِيَهۡ "
"Basi ama yule atakayepewa daftari lake kwa mkono wake wa kuume(kulia) atasema haya someni daftari langu". Mtu wa kheri hana cha kuficha maisha yake yote yako wazi, kakopia kitabu alicholetewa na Mollah wake,huyo atakua maisha yake yote ya Raha, ikiwa unaficha ficha basi jitilie wasiwasi siku hiyo usije ukawa kundi la wanopokea kwa mkono kushoto aya ya 25"
Endelea part 4
No comments:
Post a Comment