Asalaam Aleiykum,
" نِّصۡفَهُ ۥۤ أَوِ ٱنقُصۡ مِنۡهُ قَلِيلاً" "(Fanya)Nusu yake au ipunguze kidogo" kama kweli ishakuwa huwezi basi umepewa nafasi usiwache kabisa fanya japo kidogo(ukiwa mgonjwa au unakwenda kazini) "أَوۡ زِدۡ عَلَيۡهِ وَرَتِّلِ ٱلۡقُرۡءَانَ تَرۡتِيلاً "Au izidishe na soma Quraan vilivyo(Kwa uzuri)basi ikiwa huwezi soma Quraan kwa wingi,
"إِنَّا سَنُلۡقِى عَلَيۡكَ قَوۡلاً۬ ثَقِيلاً"
"Hakika sisi tutakuteremshia kauli nzito" Hii ilokwisha teremka ni kauli nzito iloteremka kutoka kwa Mollah wako, basi fanya hima ujizoeshe kuipitia kila mara kauli hii na utaziona faida zake.
"إِنَّ نَاشِئَةَ ٱلَّيۡلِ هِىَ أَشَدُّ وَطۡـًٔ۬ا وَأَقۡوَمُ قِيلاً"
Hakika (Huko)kuamka usiku na (Kufanya Ibada)kunawafikiana zaidi na moyo, na Maneno (yake)yanatuwa zaidi. Kwanini hapo ukatajwa moyo, umetajwa moyo sababu hiyo Nuru inawaka ndani ya moyo wako na kuenea Mwilini kote, na kutaka kujua hilo wewe mwanzo ukiumbwa kitu cha mwanzo kinachofanya moyo wako upige ni hiyo(The electrical impulse from the SA node triggers a sequence of electrical events in the heart )Sasa ikiwa kumbe kwenye huo moyo wenyewe una umeme kwanini ushindwe kuuwasha ukakuongoza, na umeshaambiwa nyakati za usiku ndio kunawafikiana uzuri, sababu kiza kishaingia na maneno unayozungumza yanateremka kwenda kuiwasha hiyo(Taa) au nuru ya Ucha Mungu, kwa sababu maneno ni (Sound) na hiyo (Sound) karibuni itakuja kugundulika inatokana na (Electric) ndio maana ukaambiwa viwili hivi vinakubaliana,
"إِنَّ لَكَ فِى ٱلنَّہَارِ سَبۡحً۬ا طَوِيلاً۬"
"Hakika mchana una shughuli nyingi" Usije ukajidanganya utafanya Ibada mchana, huna nafasi hiyo, kuna mambo mengi yamekuzunguka, kama vile kazi au biashara, na mengineyo ya kelele za mpira na fujo za kisiasa, hupati utulivu, subiri watu washalala yatupe maguo yako uzungumze na Mollah wako akufungulie mlango wa Taqwa.
"وَٱذۡكُرِ ٱسۡمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلۡ إِلَيۡهِ تَبۡتِيلاً۬"
"Na litaje jina la Mollah wako na ujitupe kwake kwa ukweli",
Litaje jina la Mollah wako kwa wingi sana, fanya Dhikiri moyoni mwako mpaka iwe chochote unachotaka kukifanya mwanzo unamtaja Mollah wako, Ikisha jitupe kwake, na maana ya kujitupa(Sio Ulale)ila umtegemee yeye kwa kila jambo, uwe huna mpenzi mwengine ila yeye, iwe fikira zako kila wakati unamfikiri Mollah wako na kumkumbuka, na utakapodumu katika hali hiyo, ikaonekana ama kweli sasa umejitupa kwa Mollah wako, unakijua nini kinatokezea?
Hapo inawaka Nuru ndani ya kifua chako, na dalili za mwanzo utaona kitu kidogo japo cha kufurahisha machozi yana kumiminika kwa hali unayoihisi, huku moyoni unasema kumbe ndio hivi inavokua, jua hapo Nuru ishawaka, na Nuru ikiwaka giza linatoweka, jua likitokeza usiku unaondoka, hapo tena chochote kile unachofanya kinafuta makosa yako, na ushahidi wa hayo sura ya (Hud aya ya 114),
"وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ طَرَفَىِ ٱلنَّہَارِ وَزُلَفً۬ا مِّنَ ٱلَّيۡلِۚ إِنَّ ٱلۡحَسَنَـٰتِ يُذۡهِبۡنَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ ذَٲلِكَ ذِكۡرَىٰ لِلذَّٲكِرِينَ"
Na simamisha Sala katika Ncha mbili za Mchana(Aduhuri na Alasiri) na nyakati za usiku zilizo karibu na Mchana(Nazo ni Magharibi na Isha)Hakika ya Mema huondoa Maovu, Huu ni ukumbusho kwa wanaokumbuka. Ukijitupa kwa Mollah wako utakua unakumbuka na ukikumbuka ndio huko kuwasha Taa(Nuru)na taa ikiwaka hutendi maovu ila mema, na huko kusimama usiku kusali na kusoma Quraan ni mema matupu, na hapo ndio inapatikana lile kusudio la (Malipo ya Taqwa kusamehewa).
Ikiwa taa ya nje inatoboa siri zako na dhanmbi zako ulofanya hii
Taa ya ndani inapowaka inafuta dhanmbi zako, na inakufanya unakua (More Alert) ukinyanyuka usiku unavunja uwezo wa kutenda maovu, inateremka moyoni mwako neema hii ya (Taqwa) mpaka inageuka khofu, nini khofu? utashangaa nikikwambia khofu ni mapenzi, na hiyo khofu ni sawasawa na ushujaa, yote ni mapenzi moja penzi la ndani na la pili ni penzi la nje. katika kutafautishwa ndio moja likaitwa khofu na jengine kuitwa ushujaa, anopewa yote mawili anakua mwenye kufuzu, anakua (Shaahid) ndani anamuogopa Mollah wake na nje anajikinga na yale Aloharamisha Mollah wake, huyo kaipata (Taqwa) na huyo ni mwenye kufuzu.
Na nyinyi sasa mshazijua mbinu za kuwasha taa ya Ucha Mungu, na mnaingia katika mwezi wa kujilinda na vyote vilo haramishwa na Mollah wetu, basi zidisha juhudi mpaka ifikie kile cha halali unakiogopa kisije kuwa cha haramu, hiyo pia ni dalili za (Taqwa). Na ukifanya hivyo itakua Taa yako au Nuru uliyoiwasha moyoni itamurika katika kiza cha Madhanmbi, na huku unaendelea kuomba Maghfira kwa madhanmbi yako yote, Na hiyo ndio faida ya Taqwa.Usisubiri mpaka mtu akuamshe, nyanyuka mwenyewe upate kurehemewa , Nyanyuka usiku upate kusamehewa, simama kucha ulitaje jina la Mollah wako ili upate kunusuriwa na Moto wa Jahannam, Na hayo kwa ufupi ni baadhi ya malipo ya Taqwa.
No comments:
Post a Comment