Asalaam Aleiykum,
Sasa tizama kama utafata utaratibu ulopangiwa wa kula inapokushika njaa vipi itakua (Swaum) yako. Tuseme unaanza kula saa mbili asubuhi ukala na kukipa heshima na adabu zake zote chakula, Basi Mja wewe una uwezo wa kutokula mpaka saa nane ya mchana(Umepata masaa 6)unamaliza kula saa (8) mchana huli tena mpaka saa (1) usiku, na ukimaliza hapo huli tena usiku kucha mpaka alfajiri yake, usishtuke funga zipo za aina nyingi na hizo ni (Sunna)zilokubalika zengine zinajulikana zengine zimefichikana na moja wapo katika hizo ni ile ya (Bibi Maryam) alipoambiwa katika sura ya (Maryam) aya ya 26"
"فَكُلِى وَٱشۡرَبِى وَقَرِّى عَيۡنً۬اۖ فَإِمَّا تَرَيِنَّ مِنَ ٱلۡبَشَرِ أَحَدً۬ا فَقُولِىٓ إِنِّى نَذَرۡتُ لِلرَّحۡمَـٰنِ صَوۡمً۬ا فَلَنۡ أُڪَلِّمَ ٱلۡيَوۡمَ إِنسِيًّ۬ا"
"Basi ule na unywe litue jicho lako(Furahi) Na kama ukimuona mtu yoyote(Akauliza habari ya mtoto huyu) Sema, hakika mimi nimeweka nadhiri (Kwa Mwenye enzi Mungu)Mwingi wa Rehma ya kufunga, kwa hivyo leo sitosema na mtu"
Naam hiyo ndio faida ya kula na kunywa , ikishe utulie ufurahi sasa ushashiba, sio tena ukipita ule hichi halafu ule kile wacha tabia ya (ulafi) weka (Balance) na mtu akikukaribisha mwambie mie nimefunga sili tena mpaka usiku, zote hizo ni (nadhiri) na kufanya hivyo kutakupelekea saa zote kumkumbuka Mollah wako, jaribu japo wiki utaona raha yake, utaona wapi unaelekea, Na ukiweza kufanya hivyo ukawa unakumbuka kwa muda wa miezi mitatu tu itakujia fahamu yakujua ama funga ndio (Nature) yangu, na kuanzia siku hiyo ikikujia fahamu hiyo utaweza kuupata (Ucha Mungu) na kuweza ku(Control)tabia yako, na wala hali hiyo haitokutoka tena, kumbuka (Funga)ni Maumbile yako, maisha yote wewe uko katika (Swaum)lakini sahau tu ndio ilo kushika na umezongwa na maisha na mambo mengine mengi takriban miezi kumi na moja, Sasa Ramadhan imeletwa kwa ajili gani?.
Katika mwezi wa Ramadhan unapatikana huo (muamsho) au wito maalum kwa Waumin kuitwa na Mollah wao watoke katika kusahau, katika kipindi hiki sasa wawashe taa na kuijua faida ya hii (Funga)"Al Baqarah 183"
"يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡڪُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِڪُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ"
"Enyi Mloamini mmelazimishwa kufunga kama walivo lazimishwa waliokua kabla yenu ili mpate kumcha Mungu"
Sasa nini kinatokea kwa Muumin mwenye kuukubali wito huu, "Enyi Mloamini wito huu ni (Special) kwenu nyinyi waja wangu kujijua nyinyi ni nani na mko hapa kwa madhumuni gani, miezi 11 yote mmeshughulika na Biashara au Siasa, mmeshughulika na mambo ya Ofisi au Maharusi na mengineyo, Mwezi huu mnatakiwa katika siku hizi chache kama nyinyi Waumin wa kweli basi sahauni kila kitu, Ikisha mfanye nini? Jitafautisheni na hicho kiwiliwili(Body) juweni nyinyi ni muungano wa vitu viwili (Ardhi) Kiwiliwili na hicho cha pili ni hiyo (Roho) na hii Ramadhan ndio hiyo Ustaadh wa kuilea hiyo (Roho) Vipi italelewa hiyo Roho?
Katika kipindi hichi cha mwezi wa Ramadhan, tumo katika kufanya uchambuzi wa (Swaum) kwa njia ya (Tawhid) naomba mnistahamilie ili twende kidogo kidogo upate kuifahamu"
" كُتِبَ عَلَيۡڪُمُ ٱلصِّيَامُ"
Sasa nakuamrisheni kufunga, Nini kufunga? Kufunga ni Maumbile yenu, siku za kawaida mnafunga bila ya kujifahamu, bila ya kukumbuka mefunga, ila mwezi huu mmeamrishwa mkumbuke, nini kinafanyika hapo, hayo masaa matatu niloyataja mwanzoni mnayo kula na kunywa, moja linaondoshwa na yale mawili yalobaki yanabadilishwa mwenendo kutoka mchana kwenda usiku
" ثُمَّ أَتِمُّواْ ٱلصِّيَامَ إِلَى ٱلَّيۡلِۚ"
"Ikisha itimizeni Swaum mpaka usiku"
Nini kinatokezea, wewe chunguza (Mwili au Body) inaponyimwa chakula kinapatikana kitu (Awareness) Ufahamu, au kukumbuka au (Dhikr) ikipatikana fahamu hii sasa Waumin wanaitumiaje?
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment