Asalaam Aleiykum,
Umekaribia mwezi mtukufu wa Ramadhan na sisi bora tuanze kujiandaa kwa kumkaribisha mgeni wetu huyu kwa unyenyekevu ulio mkubwa kabisa, Wacha tuanze kuzikosha (Roho) zetu kwa maneno yenye nuru, maneno ya Muangaza. Katika darsa hii tutajifunza mambo muhimu ili tupate kuifanya Ramadhan yetu ya mwaka huu iwe tafauti na zote zilopita, fatana na mimi nikushike mkono ili nikuoneshe wito huu wa Mollah wetu unakuelekeza pahala gani, Na kwanini ukaitwa?, Na wewe uloitwa ni nani?.
Katika safari hii kuna mambo yatakuzindua ili upate kujijua kama wewe ni mtu (Special) kwa Mollah wako, Darsa hii madhumuni yake ni kuwasha (Taa) ya (Roho) yako ambayo katika kipindi hiki cha miezi kumi na moja kwa makusudi umeizima, Najua unaweza kushangaa mbona darsa hii tafauti na (Sheikh) wangu, kusudio langu mimi ushangae, Na ukishangaa ndio ushakamata hiyo (Switch)na sasa ushawasha hiyo (Taa).
Sababu tumeshachoka na vigoma vya kuamsha daku, kila tukipiga huamki unazidi kulala(fofofo), unapata darsa hii yenye kufungua na kupenya kwenye (Akili) yako ili upate kujua nini (Funga-Swaum)?na kwanini ufunge?
Nimetanguliza darsa hii kwa sababu kuna watu (Shetani)kashawavamia ili watengeneze maradhi ya kubuni, kuna wanowaza (Ulcer) ndio zinaanza kuchipua magonjwa haya na yale yanaanza kujitokeza katika mwezi huu wa Shaaban, ili itapoingia Ramadhan mtu aendelee kuuchapa (Mpunga)kama kawaida yake.
Leo hapa nataka kueleza nini hasa dhumuni la hiyo funga(Swaum) lakini kabla ya kufanya hivyo hebu tuiangalie (Funga) jee ni kweli (Maumbile)yetu. "Ewe Mwanaadamu amka(Washa Taa) ujue yakwamba wewe unafunga kila siku lakini upo gizani hutambui" Sababu umelala na sasa wacha nikuamshe uone vipi unafunga katika haya masaa (24) ya Uhai wako, "Wewe una dasturi ya kufunga masaa (21) kutokana na (Basic Nature) ya kiwiliwili chako", Nikisema hivyo najua wengine watajiuliza mbona nakula (Chewing gum), mbona navuta Sigara, mbona nakunywa (Juice) na amali zengine unazozifanya mwenyewe ambazo unazijua, zote hizo ukizichunguza ni tabia lakini sio (Basic Nature) yako, Mwili wa binaadamu hautaki ziada ila (Akili) yako ndio yenye kutaka ziada, jitizame unakula ukiwa na njaa au unakula kwa mazoea.
Mwanaadamu unaivunja Ibadah hii ya Swaum kutokana zile nyakati unazokula unakua pia umetawaliwa na mazungumzo pengine ya siasa, au unakula huku unazungumzia Mpira, au sherehe za harusi ndio zimetanda wakati wa kula, Chakula hukipi heshima yake, unasahau chakula kimetokea wapi hata kukufikia wewe mezani kwako, unasahau Nani alokitia Ladha, Nani alokifanya kiwe kitamu, jiangalie vipi unakula utaona unatupa kapuni, hujui hata ladha ya chakula, unakula bila ya njaa, unakula kwa kufata tabia, imefika saa saba ni (time) ya kula, hata ikiwa huna njaa wewe unakula, hata iwe nusu saa ilopita ushapiga bakuli la (Urojo).lakini hukubali na ugali lazima utie kapuni.
Lakini ikiwa utakula kwa kufata mwito wa Njaa basi utagundua kila siku ya maisha yako ni (Swaum) kwako, vipi inakua hiyo Funga.
Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment