Asalaam Aleiykum,
Mollah wetu ametuumba wanaadamu ikisha akatufanya si wenye kuepuka vitendo vya Dhanmbi, akatutenganisha viumbe sisi kuwa tafauti na Malaika, ikisha tena akatuwekea njia ya Mitihani katika mambo mawili, la kwanza ni Amali za kheri na la pili zile amali za shari, Ikisha akamfahamisha tena jambo la tatu nalo hili la kufanya Taqwa, kwa ajili ya kumtizama kama kweli kiumbe changu kina mapenzi na mimi Mollah wake Muumba, Na jambo la nne akamjulisha hiyo shughuli ya matamanio huku akiwa anamjua udhaifu wa kiumbe chake, kutokana na kufahamu vyema udhaifu huo ndio akamuekea hili la tano nalo ni zawadi ya kumsamehe.
Jambo hili la Msamaha leo ndio tunaingia katika kumi lake, hii ni sehemu maalumu ilotengwa kwa wale watotaka kuomba msamaha, Sasa kwanini Mwezi huu na hususan ndani ya kumi hili?.
Sababu kubwa mwezi huu ikiwa kweli umefunga kwa dhati na Imani ilothibitika wa hiyo (Taqwa) basi ni lazima kumi la mwanzo lilopita ushapata hiyo Rehma, kwa Maana hiyo umesha safishika na sasa uko tayari kurejea kwa Mollah wako(Usishtuke sio kufa maana yake hilo mnaogopa sana)kurejea hapo ni kusudio la hiyo (Toba) Tayari sasa mapenzi yashakuvaa katika mambo ya kidini, tayari ushaanza kuonea huruma viumbe wenzako, Na sasa umeingia katika (Stage) ya kuitakasa Roho yako kwa kuomba (Maghfira)Msamaha kwa Mollah wako.
Msamaha wenyewe kwa yale yote ulotenda dhidi ya Mollah wako na pia kwa Viumbe wenzako, Hivi sasa wewe Umeshagundua kuwa Dhanmbi zimekuzunguka kila upande, yaweza kuwa dhanmbi za Husda au Chuki, umezifanya za Ufisadi au zile za Uhasama, Umetenda dhanmbi za wivu na zile za Macho na Masikio, kuna zile ulizo zisahau, na hizo unazozikumbuka. kuna zile za Ulimi na hata hizo za Mawazo machafu au mabaya zote hizo zinatakiwa ziombewe Samahani, Na ukijitia Ujabari huombi Msamaha siku ya Hukumu utafungwa nazo shingoni huku unapelekwa kuhudhuria mbele ya Enzi ya Mollah wako.
Kwanini Usitubu? Wakati Bwana Mtume s.a.w anasema katika hadith(Sharif)"Enyi Watu Tubuni kwa Mollah wenu, hakika mimi mwenyewe kwa siku natubu mara mia moja". Inawezekana wewe Mpaka leo ya kumi hujatubu hata mara tano, sasa leo umeingia hili kumi la (Maghfira)Kusamehewa, basi kama hujaanza, basi anza leo kutubu na kama umeshaanza basi zidisha idadi na mara zako za kutubu ili uwe mwenye kufanikiwa, Ewe mja anguka kwa Mollah wako utoke chozi, halafu ujute kwa yote uliyoyatenda, na wala usione unayefanya ni wewe bali hata mitume wa Mwenye-Enzi-Mungu na wao wamefanya makosa na wakatubu, na kama unataka ushahidi wa hayo na vipi kupata maneno ya Toba endelea Part 2
No comments:
Post a Comment