Asalaam Aleiykum,
Nini Kutubu? Kutubu ni kukumbuka kuwa yupo aliyeniumba, namie kwa heshima zote narejea na kugaragara chini ya Enzi yake ya kusamehe, nikitaraji yale yote nilotenda Mollah wangu atanisamehe, Na mimi nimo kwenye mwezi Mtukufu wa Ramadhan, katika mwezi huu nimo katika kukumbuka, basi wacha nijiunge na wale walotajwa katika sura ya Al-Imran 135
وَٱلَّذِينَ إِذَا فَعَلُواْ فَـٰحِشَةً أَوۡ ظَلَمُوٓاْ أَنفُسَہُمۡ ذَكَرُواْ ٱللَّهَ فَٱسۡتَغۡفَرُواْ لِذُنُوبِهِمۡ وَمَن يَغۡفِرُ ٱلذُّنُوبَ إِلَّا ٱللَّهُ وَلَمۡ يُصِرُّواْ عَلَىٰ مَا فَعَلُواْ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ
Na ambao wanapofanya Uchafu, au kudhulumu nafsi zao, hukumbuka Mwenye Enzi Mungu na kuomba Msamaha kwa Dhanmbi zao, Na Nani anayeghufiria dhanmbi isipokua Mwenye Enzi Mungu, Na(Wala)hawaendelei na (Mijidhanmbi)waliyoyafanya, hali wanajua.
Wametajwa kwenye hiyo aya wale wanofanya Uchafu, kwa kumaanisha dunia hii ni safi, njia imenyooka, ila wewe ndie unaekuja na visa na mikasa, ukauchafua Ulimwengu huu kwa dhanmbi chungu nzima, na kila ukiona watu wanasafisha kila ukichafua, basi hapo tena unarejea nakuanza kudhulumu nafsi yako mwenyewe kwa mambo chungu nzima yalokuzunguka, lakini ukitanabahi na kujua yupo aloniumba mimi na anastahiki kuabudiwa na kuombwa Msamaha, basi hakuna mwengine atakaye kusamehe isipokua yeye Mollah wako, kama walivosamehewa wengine walopita kabla yako.
Basi wakumbushe kisa cha Nabii Daud a.s pale alipompenda Mwanamke akaamua kumpeleka mume wa Mke huyo ambaye aliyekua Jeneral wake vitani, huku akijua fika hatorejea yuko hai, jikumbushe nini kilitokea, Quraan sura ya Sad aya ya 21-25
" وَهَلۡ أَتَٮٰكَ نَبَؤُاْ ٱلۡخَصۡمِ إِذۡ تَسَوَّرُواْ ٱلۡمِحۡرَابَ"
Na jee imekufikia habari ya wagonvi walipopindukia(Ukutani)chumbani(Kwa Nabii Daud). Nabii Daud alikua na jeshi lenye nguvu na ulinzi Mkali, walipoingia (Hawa Malaika wawili)ilikuaje.
"إِذۡ دَخَلُواْ عَلَىٰ دَاوُ ۥدَ فَفَزِعَ مِنۡہُمۡۖ قَالُواْ لَا تَخَفۡۖ خَصۡمَانِ بَغَىٰ بَعۡضُنَا عَلَىٰ بَعۡضٍ۬ فَٱحۡكُم بَيۡنَنَا بِٱلۡحَقِّ وَلَا تُشۡطِطۡ وَٱهۡدِنَآ إِلَىٰ سَوَآءِ ٱلصِّرَٲطِ"
Walipomuingilia Daud na (yeye)akawaogopa, Wakasema Usiogope, (sie ni )wagombanao wawili, Mmoja wetu amemdhulumu mwenziwe, basi (sasa)tuhukumu,(toa uamuzi baina yetu)Kwa haki wala usipendelee, na utuongoe katika njia iliyo sawa.
Na nyinyi pia wenye madaraka, viongozi, wenye uwezo, mawakili mnajiwa na watu na kesi kama hizi, wanakujieni maofisini na majumbani watu kudai haki zao ili , Muhukumu kwa njia ya haki, tena wanakwambieni nisaidieni mimi nimedhulumiwa nini unamjibu, Huna jawabu ila kula Rushwa, huna Jawabu ila kuchangia dhuluma, huna jawabu ila kuleta fisadi ndani ya mji.
"إِنَّ هَـٰذَآ أَخِى لَهُ ۥ تِسۡعٌ۬ وَتِسۡعُونَ نَعۡجَةً۬ وَلِىَ نَعۡجَةٌ۬ وَٲحِدَةٌ۬ فَقَالَ أَكۡفِلۡنِيہَا وَعَزَّنِى فِى ٱلۡخِطَابِ"
Hakika huyu ni ndugu yangu, yeye ana kondoo majike tisini na tisa, na mimi nina kondoo mmoja tu jike,lakini amesema, nipe huyu wako nikufugie, Na amenishinda katika maneno.
Na nyinyi hali kadhalika anakuja mtu pengine ana viwanja 99 lakini kakipenda kile kimoja hakiwezi kukikosa, basi hapo unamtilia Mawakili na vitisho hivi na vile, mpaka mnamshinda maskini yule kwa maneno ikisha hao mnakichukua kiwanja au kitu chengine mlofanikiwa kukipata kwa njia ya wizi.Tena mnaruhusu wengine ndugu kudhulumiana, kwa kuwa ana uwezo na kashakupa chai.
" قَالَ لَقَدۡ ظَلَمَكَ بِسُؤَالِ نَعۡجَتِكَ إِلَىٰ نِعَاجِهِۦۖ وَإِنَّ كَثِيرً۬ا مِّنَ ٱلۡخُلَطَآءِ لَيَبۡغِى بَعۡضُہُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٍ إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَقَلِيلٌ۬ مَّا هُمۡۗ وَظَنَّ دَاوُ ۥدُ أَنَّمَا فَتَنَّـٰهُ فَٱسۡتَغۡفَرَ رَبَّهُ ۥ وَخَرَّ رَاكِعً۬ا وَأَنَابَ "
Akasema kweli amekudhulumu kwa kukuomba kondoo wako kuongeza katika kondoo wake, Na bila shaka washirika wengi hudhulumiana wao kwa wao, isipokua wale waloamini na kutenda mema, na hao ni wachache:Na mara Daud akaona kwamba tumemtia mtihanini(Na amefeli)Akaomba maghfira kwa Mollah wake, na akaanguka (Kwa)Kunyenyekea na Akaelekea kwa (Mollah wake).
Haijambo huyu Mtume wa Mwenye Enzi Mungu, kapata ukumbusho na kuzinduka, Na wewe pia unapata ukumbusho kama huo ila tafauti yake wewe unaendelea na vitimbi vyako, na hivi ndivo ilivo dhihiri mambo ya dhuluma, kila mtu katoka kwenye dini yake, kila mtu anataka mali, hakuna huruma, watu wamesahau hata kuomba msamaha ni kitu gani, hiyo ni habari ya dhuluma na kutubia kwa Mtume wa Mwenye enzi Mungu, na kuna kisa cha Musa a.s yeye alivompiga mtu ngumi akamuua akamuomba Mollah wake amsamehe sura ya Qasas aya ya 16"
"قَالَ رَبِّ إِنِّى ظَلَمۡتُ نَفۡسِى فَٱغۡفِرۡ لِى فَغَفَرَ لَهُ ۥۤۚ إِنَّهُ ۥ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ "
Akasema Mollah wangu, bila shaka nimedhulumu nafsi yangu, basi (Naomba)nisamehe, Naye (Mollah)akamsamehe, (Sababu hakufanya kwa kusudi) hakika yeye ni mwingi wa kusamehe (na)kurehemu. hilo pia tendo la Mauaji, na kama utarudi kikweli kwa Mollah wako basi utamkuta yeye mwenye kukusamehe.
Sasa endelea part 3 ukapate hayo maneno yakuombea toba na ujue yalianzia wapi.
No comments:
Post a Comment