Sunday, August 25, 2013

SALA YA MSIKITINI PART 3

Asalaam Aleiykum,

Anahadithia Sahaba Abdulla bin Omar r.a "Siku moja wakati Bwana Mtume s.a.w ameshakufa" Ilitokea kuna mtu ambae hakumuwahi Bwana Mtume s.a.w katika uhai wake, lakini alipopita Sahaba mmoja alokua pamoja na bwana Mtume s.a.w katika uhai wake, alinyanyuka bwana huyu na kuuvamia ule mkono wa Sahaba na kuubusu, alipoulizwa kwanini ulifanya vile, akajibu hamkijui kilichonivuta mimi kwenye ule mkono, lakini nitakwambieni kimoja tu mkono ule umewahi kushikana na mkono wa Bwana Mtume s.a.w. Hivo ndivo (Energy) Inavobakia katika Ulimwengu huu, hiyo ndio Maana ya kuambiwa Sala ya Msikiti wa Makka na Madina ni (Bora) kuliko Misikiti mengineyo, na hivi ndivo tunavo wajibu wale wanotuuliza kwanini kila ukenda Unguja lazima ukasali Msikiti (Gofu)Msikiti huo wamepita Mabwana wazito wazito, na (Energy)zao zimebaki kama tutavoona huko mbeleni.
Unakwenda hatua baada ya hatua mpaka unawasili Msikitini, Hatua na (Energy) ulotengeneza kwa ajili ya Ibadah zinabaki katika Ulimwengu huu kama inavobaki Sauti yako, Ukisema Uongo unabaki, ukipiga kelele zinabaki, ukisoma Quraan inabaki, hakuna kinachopotea, kwa hiyo tahadhari sana vipi unatumia (Energy) yako, iwe ya kazi, sauti, au Ibadah.
Unaingia Msikitini kila tendo lako linatengeneza (Energy) ambayo inabaki ndani ya Msikiti, ni matendo ya Ibadah, ni sauti za kusabahi, ni matendo ya kutukuza,kuomba Dua na kusujudu yanaobaki Ndani ya Misikiti, Sasa nini kinatokea, unaingia Muumin mja wa kheri, mnasimama kusali Jamaa kwa pamoja, na hapo ndio inapatikana (Symbol) ya Sala ya Kiislam ilokusanya Sala za dini zote za (Ahlil Kitaab) ukiwa wewe (Mkiristo au Myahudi)zote zimo, ikiwa unasali kwa kusimama basi kwenye Uislam utasimama, ikiwa unasali kwa kukaa kwenye Uislam pia imo kukaa, ikiwa unasali kwa kusujudu pia kwenye Uislam Utasujudu, kwa kuwa Dini ya haki imekusanya Dini zote na kuifanya ni Dini kuwa Moja.
Sasa Mtizame khalifa wa kwenye hii Ardhi vipi anawakilisha kila kilichomo katika Ulimwengu huu, Anasimama Mbele ya Mollah wake Kwa Heshima zote akiachia mikono au akifunga, akinyanyua au akiiwacha chini, basi yeye Mbele ya Mollah wake ni mwenye kuwajumuisha Ndege, Milima, na Miti na vyote vilivyomo, amesimama kwa unyenyekevu wa Kumsabahi Mollah wake na anapo (Rukuu) anajumuisha na kujirejesha kwenye hali ya (Mnyama) anakubali kuwakilisha jinsia ya ukaribu na Umbile lake na la Wanyama wote, na anapo (Sujjudu) hapo anarejea kwa kutii amri ya Mwenye enzi Mungu aliowaamrisha Malaika na Majini kuitenda, Amri ya kusujudu ni (Surrender) Unayayuka kwa utiifu, kwa kutii Amri ya kuanguka kwenye Ardhi na kumsabahi Mollah wako na Kumtukuza kwa sifa kubwa kubwa, hiyo ndio (Symbol)ya Sala ya Kiislam, na hapo ndipo inapobakia hiyo (Energy)ya Ibadah, na ndio unapatikana Utukufu wa Ibadah ya Msikitini, na hupatikana hiyo (Rest-Energy) au (E=Mc2)ya Ibadah, huo ndio Ubora wa Msikiti, na kila Pakisaliwa (Energy) inaongezeka na unapatikana uzuri wa dua za msikitini na Mambo ya kheri yanofanyika humo na usafi wa Nyumba hizo za Ibadah, na uzuri wa kuitwa (Baitul-Sujjud).Kwa hiyo fanya umuhimu wa kuipata Sala ya Msikitini na Fadhila zake ili na wewe uwe umewacha (Energy) ya Ibadah katika Misikiti hiyo.
Na kama Wanasali watu wa Kheri katika Misikiti hiyo na wewe ni Mwenye kuijua (Energy) hii basi ukiingia kwenye Msikiti utahisi (Positive Energy) Itakujaa Furaha ya wewe kuwapo Msikitini hapo, Na kama Wanasali Watu wa Shari, Wanaabudu watu wa Dhuluma, au Wala Rushwa, basi Utahisi (Nagative Energy) na utataka utoke mbio, mara utaona Mahirizi na vituko vya kila aina, Nyumba ya Mungu inageuzwa sehemu ya Mikasa na jukwaa la mazungumzo, hilo si dhumuni lake na kama unajua maana ya Msikiti basi toka mbio usije ukawa mwenye kushiriki katika (Nagative Energy). Tunamuomba Mollah atujaalie kuyajua hayo na kuyaepuka.


No comments:

Post a Comment