Sunday, August 4, 2013

KWAHERI RAMADHAN KARIBU UCHA MUNGU PART 3

Asalaam Aleiykum,

tizama mapenzi ya Mwenye enzi Mungu yanavomiminika juu yako, kakupangia (Circle)Maalum, kama utaifata kwa utiifu utakua huna mashaka katika maisha yako, na hiyo ndio (Taqwa), Kwanza kabisa jiulize umetokea wapi?(Original)yako. Umetokea kwake yeye Mollah wako, Kwa mapenzi yake kakuumba mwanaadamu akakufanyia njia ya kuja katika Ulimwengu huu kupitia kwa wazee wako, Akakuweka kwenye Tumbo la mama yako miezi 9, ukawa (KKB)kula na kulala bure, (Al-mursalat 21)"فَجَعَلۡنَـٰهُ فِى قَرَارٍ۬ مَّكِينٍ" "Ikisha tukayaweka mahali pa utulivu"
Huna hofu mpaka siku ya kutoka tumboni na kuja duniani, hapo tena kwa mapenzi makubwa anakukabidhi kwa wazee wako wawili, anawatia mapenzi wanakulea kwa mapenzi makubwa na uangalifu, na unapofikia ujanani anakuongoza Mollah wako ukapata mwenzio wakupendana katika ndoa yenu, akakupeni kizazi ikisha ukiwa mtu mzima anawatia mapenzi kizazi chako cha kukupenda na kukutizama kwa mapenzi na huruma kubwa, Na wewe kama una Imani utajua toka mwanzo mpaka mwisho, umo kwenye (Taqwa)au mapenzi ya kuenziwa kiumbe wewe, kwanini leo Mwenye enzi Mungu kakurejesha  katika hiyo Taqwa na wewe unajiandaa kutoka tena. Basi kabla ya kutoroka nyumbani izingatie aya ya 70 sura ya Bani Israel inakukumbusha nini?

 وَلَقَدۡ كَرَّمۡنَا بَنِىٓ ءَادَمَ وَحَمَلۡنَـٰهُمۡ فِى ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِ وَرَزَقۡنَـٰهُم مِّنَ ٱلطَّيِّبَـٰتِ وَفَضَّلۡنَـٰهُمۡ عَلَىٰ" ڪَثِيرٍ۬ مِّمَّنۡ خَلَقۡنَا تَفۡضِيلاً۬"
"Na hakika tumewatukuza wanaadamu na tumewapa vya kupanda barani na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewatukuza kuliko wengi katika wale tuliowaumba kwa utukufu ulio mkubwa"
Kwanza kabisa aya imeanza kwa kutukuzwa, wewe special lakini maskini hujijui, halafu ukapewa vya kupanda vya Bara na Baharini ili usihangaike, na tafauti ya kupewa na kuruzukiwa moja imefichikana na nyengine inaoneka kupewa ni (Form) Kuruzukiwa ni (Formless) Kupewa ni (Known) kuruzukiwa (Uknown) Kupewa ni (System)Maalum, Kuruzukiwa ni (Indivisual) hiyo ndio (Life) ilivyo, asizuke mtu na kusimama hichi haramu kile haramu, umeruzukiwa vitu vizuri tena vya kila aina, furahia wala usijikere ila usivuke mipaka, na wewe mwenye kuijua unajua hichi kibaya na hichi kizuri, umepewa utajiri shukuru ufurahi nao, utendee wema utajiri wako, umepewa uzuri furahi Mollah kanichagua mimi niwe zaidi basi ondosha kiburi, umepewa elimu furahi umechaguliwa wewe, sio unapita soda haramu, simu haramu , inakua Sheikh (Full of Haram) haijaja dini kukupiga marufuku kuishi, ishi lakini kama umo kwenye Swaum, Ishi ukiwa na Taqwa yako, hiyo ndio dini, sio kusema TV haramu ukiipata kwa siri unatizama (Programme)yote huo unafiki, napia napenda ujue hakuna makosa kuwa tajiri makosa kumsahau Mollah wako, na kwanini uyakanushe maneno hayo ya  vitu vizuri, wakati wewe katika maisha yako ni vingi vizuri ulivokutana navyo kuliko vibaya, kwa sababu wewe malezi yako yote unalelewa kwenye hiyo Taqwa ya Mwenye enzi Mungu, sasa jichunguze maishani mwako yote ulosikia na kuona mengi yepi mazuri au mabaya? jee hivyo vya harufu ulivonusa vipi vingi vibaya au vizuri? ikisha kukujulisha zaidi kama unaishi ndani ya Taqwa Mollah wako kwa Mapenzi akakufundisha elimu ya kila aina mpaka ya kumjua yeye kwenye ulimwengu huu, ili akupe yakini ya kuwepo kwake, akakufanya uwe (Master), Mtukufu kila kilichomo kwenye Ulimwengu huu anakufungulia siri zake, kwa kukujulisha elimu zake kimoja baada ya chengine, na vyote hivo umevimiliki kwa ujuzi, vipi leo wewe unakimbia katika jumba la Taqwa. 
Hayo kwa ufupi ndio mapenzi ya Muumba juu yako, hiyo ndio Taqwa ambayo umeshajiandaa kuikimbia siku itakapo malizika Ramadhan, Na Taqwa ishakwisha. Mollah wako hakutaka chochote kutoka kwako isipokua anakwambia nirejeshee mapenzi kwa kuniabudu na kufata amri zangu, kwani kama hunitii amri zangu na kufanya Ibadah na unaendelea kufanya maovu basi huwezi kunipenda mimi, sasa yaangalie majibu ya Kiumbe kilichofanyiwa hayo yote kinakuja na majibu yepi. Endelea part 4 uone manyago.

No comments:

Post a Comment