Asalaam Aleiykum,
Sasa Nenda Makka uko huru wewe msafi, ondoa shaka ingia kwenye mji huu ukiwa na Imani utapokewa kwa mapenzi na Mollah wako, huku machozi yakikumiminika.
Al-Imran 96-97,
"إِنَّ أَوَّلَ بَيۡتٍ۬ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِى بِبَكَّةَ مُبَارَكً۬ا وَهُدً۬ى لِّلۡعَـٰلَمِينَ"
Kwa hakika Nyumba ya kwanza iliyowekwa kwa ajili watu(kufanya Ibadah)ni ile iliyoko Makka, yenye Baraka na Uongozi kwa ajili ya Walimwengu wote.
Sasa ushabadilika na umekua msafi nenda kwenye nyumba hii ya Ibadah, Ikiwa umeweza kuhijj kwenye Moyo wako ukagundua mambo yanotokea kwenye nafsi yako, basi sasa itakua rahisi pia kuyaona na kuhisi Baraka za mji huu wa Makka zinavoshuka, Na Baraka zipo za aina nyingi, Machozi yakikumiminika elewa hizo ni Baraka, Kuona siri za mji huo hiyo ni Baraka, kukubaliwa Ibadah zako hiyo ni Baraka, na huo Uongozi ni kuhudhuria kwako sehemu hiyo na kupata jina maalum la kukumbusha kuwa wewe ulokwenda ni kiongozi wa mfano kwa wenzio wote walokua bado hawajenda kwenye mji huu Mtukufu wa Makka, kwa hiyo ongoza kwa Mfano, sio ukirudi tu unakua kama walokua hawajenda, unakua kiongozi wa Rusha Roho, kiongozi wa mapambano ya siasa, mkuu wa upokeaji Rushwa,Mdhalilishaji wa viumbe wenzio, utakua huna Hijja na ni muflis kabisa.
"فِيهِ ءَايَـٰتُۢ بَيِّنَـٰتٌ۬ مَّقَامُ إِبۡرَٲهِيمَۖ وَمَن دَخَلَهُ ۥ كَانَ ءَامِنً۬اۗ وَلِلَّهِ عَلَى ٱلنَّاسِ حِجُّ ٱلۡبَيۡتِ مَنِ ٱسۡتَطَاعَ إِلَيۡهِ سَبِيلاً۬ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَنِىٌّ عَنِ ٱلۡعَـٰلَمِينَ"
Humo mna ishara zilizo wazi, mahali alipokua akisimama Nabii Ibrahim (a.s) Na anayeingia (Mji Huo)anakua katika Salama, Na Mwenye enzi Mungu amewajibishia(Wajib) watu wafanye Hijja katika Nyumba hiyo, yule awezaye kufunga safari kwenda huko, Na atakae kanusha(Kupuuza), Basi Mwenye enzi Mungu si Muhitaji wa Walimwengu.
Katika mji huu kuna Ishara zilizo wazi lakini mtu anakwenda mpaka anarudi hazioni wala kuzihisi mpaka anarudi, vipi leo atagundua zilizofichika, na yoyote yule anayeingia mji huu keshaipata Salama kutokana na hiyo(Special Energy) ya mji huu, vipi unaipata salama hiyo?.
"Anahadithia Jabiri r.a" "Kwamba Bwana Mtume s.a.w "Kasema hakika hii nyumba ni (Alama)nguzo katika nguzo ya Uislam" Mwenye kuhijj au kufanya Umra anaipata Dhamana kutoka kwa Mollah wake, Atakapokufa anaingia peponi,(Ndio maana nikakwambia kwanza Kahijj moyoni)usije ukenda na kesi za kudhulumu na mauaji ukategemea utachukuliwa Dhamana, Na akirejea kwa watu wake anakua mwenye ujira kwa Mwenye enzi Mungu, na Baraka (Zinamiminika)". Jua wewe unarejea na Baraka maalumu umepata Special (Energy) basi fanya ubaki nayo kwa kuwa Mcha Mungu. Na akaendelea kusema Bwana Mtume s.a.w "Anaekufa njiani ikiwa anakwenda au anarudi akawa (hajachafua hijja yake kwa jambo ovu au kuondoa heshima yake)Basi Humsamehe Mollah wake" Na kwanini usisamehewe na wewe ushajisafisha kabla ya kwenda na ukiwa unarudi. Na hiyo ndio Hijja unayotakiwa uitekeleze kuitikia wito wa Mollah wako useme:
Laabaiyka Allahumma Laabaiyka Laa Sharika Laka Labaiyka.
Mollah awakubalie wote wenye nia ya kwenda kufanya Hajj na warejee kwa salama wawe wenye mafanikio na kuishi na hizo Baraka.Amin
No comments:
Post a Comment