Asalaam Aleiykum,
Tumeshaona vipi mwenye kuendekeza matamanio haya ya mapenzi ya (sex)jinsi anavoteseka na kuwatesa wenzie, hatukatai yumo kwenye njia ya mapenzi lakini ni ya muda mchache sana, na anapomaliza haja zake anajikuta tafrani, hana furaha, na ili kujizubaisha inabidi aende mawindoni tena ili kupata furaha zake za muda mfupi, na hizo ndio zinakua shughuli zake mchana kutwa, muulizeni nini kila wakati kinaingia ndani ya kichwa chake, mawazo gani yanatawala senema yake kwenye akili, atakunyima jawabu lakini muda wote ni mawazo ya mapenzi ya utamanifu.
Huyu sasa anahitaji msaada, anahitaji kuambiwa sio kila kitu kinaanzia hapo na kuishia hapo kwenye ngazi ya mwanzo ambayo ya kitovuni na kwenye magoti. Huyu anataka kufahamishwa na apewe nasaha ya kwamba acha kujidhuru, jaribu kutunza (Energy)yako, jifundishe kusubiri, toa nafasi ya kutamani, jipe siku mbili tatu nguvu zikomae, halafu afahamishwe kuna ngazi ya pili ambayo utapata furaha, ashikwe mkono kuvutwa kwenye ngazi hiyo.
Ipi Ngazi ya Pili?
Ni ngazi ilotokea kitovuni kuelekea kwenye moyo, hapo inakaa furaha na utulivu, (kule kwetu Zanzibar)kuna ngazi nje, Ngazi ndani, na Ngazi mia, naifananisha hiyo ngazi ya mwanzo ni ngazi ya nje shughuli zako zote ni kwenda nje, ukikiona kile umekitamani, cha huyu unakitaka, cha yule umempokonya fujo tupu, ukiamua kuchupa kwenda kwenye hii ngazi ya pili ambayo ni ya ndani inabidi urudi kwenye Moyo wako na kufanya utafiti mkubwa, Ndio maana ukaona (Symbol)alama ya mapenzi ni Moyo, umechorwa kwa mfano wa kopa, kwenye hiyo kopa ukiitizama ina mifano mitatu, chini bonde, juu milima, ikisha alama hizo zilizo na mizani sawa zinakutana katikati kuifanya hiyo kopa, unajua kwanini ikawa hivyo, sababu katika hayo mapenzi kuna kushuka na kupanda na pia kuna kukaa sawasawa katikati, imekua hivyo sababu nyinyi kwenye hiyo nyumba au kitanda mnaishi watu wanne, (Kumbuka wewe una sehemu mbili Ubavu wa kushoto Mama yako na Ubavu wa kulia Baba yako, na mwenzio anakuja na mfano huo huo) kwa hiyo tafauti lazima iwepo, kama bahari mara imechafuka mara imetulia na hiyo ndio alama ya kopa, alama ya Mapenzi na kuonekana kwake kwa mfano wa Moyo.
Utizame moyo daima una furaha unacheza na kupiga mpaka siku yako ya kufa, ila wewe ndio unaoupelekea matatizo, hiyo ndio ngazi ya pili(Ngazi Ndani) na hapo sana utawakuta wanaishi wanawake, Moyo ni wenye kupokea hewa, unasukuma damu, na mapenzi yakishuka huko yatokako yanaanzia hapo na kusudio la mwanzo la hayo mapenzi ni kuipenda (Roho)Mapenzi ni (Sipiritual) nataka uwe na tahadhari kubwa, isije ikawa unashushiwa mapenzi yanakukuta unaangalia masofa,utakua mwenye kupenda (Furniture) usije ukawa unashushiwa mapenzi unaangalia mpira, mapenzi yako yote itakua mipira, na yasije kushuka mapenzi yakakukuta kwenye Taarab utaumia, utakua unakwenda bila ya kualikwa na ukiikosa harusi unakua mgonjwa, au yanakukuta (Disco) basi jijue utakua (Muflis)au umo kwenye kutizama mchezo wako senema itakua huna faida na jambo hilo, uchunge moyo wako hususan katika hili la kuteremkiwa na mapenzi, ni jambo adhimu sana.
Mwanamme penzi lake linaanzia kichwani ndio maana utaona mambo yake yote ni (Through action)kulieleza hili itabidi nikupeni kisa cha Nabii Musa a.s alipokua akikimbia kutoka kwa (Firauni)tizama jambo la mwanzo lilomtokea kwa kujawa na mapenzi na huruma kwa ajili ya watoto wa kike walokua wanataka kuwanywesha maji mifugo yao, (Through action)kaonesha mapenzi yake kwa njia ya huruma akawasaidia kisha akenda kivulini akarudi moyoni kwake akazungumza na Mollah wake na kumwambia maneno haya, al-Qasas aya ya 24
"" فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰٓ إِلَى ٱلظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّى لِمَآ أَنزَلۡتَ إِلَىَّ مِنۡ خَيۡرٍ۬ فَقِيرٌ۬ "
Basi (Nabii Musa)akawanyweshea, ikisha akarudi kivulini, na akasema Mollah wangu bila shaka mimi ni Muhitaji wa kheri utakayoniteremshia.
Elewa hakuna kheri kubwa kama mapenzi, (Through Love you find God)(Taqwa)Kwa hiyo na wewe kaa pembeni ufikiri moyoni mwako unataka kheri gani ikuteremkie. Kabla Nabii Musa a.s hajamaliza uzuri dua yake anarejea mtoto wa kike huku akicheka cheka na kuona haya na maneno haya.
فَجَآءَتۡهُ إِحۡدَٮٰهُمَا تَمۡشِى عَلَى ٱسۡتِحۡيَآءٍ۬ قَالَتۡ إِنَّ أَبِى يَدۡعُوكَ لِيَجۡزِيَكَ أَجۡرَ مَا سَقَيۡتَ لَنَاۚ"
Basi akamjia mmoja katika wale (Wanawake)wawili anakwenda na huku anaona haya, akasema Baba yangu anakuita ili akulipe ujira wa kutunyweshea (Mifugo). Na mpaka inapomalizikia aya.
Watoto wakike mapenzi yamewashukia moyoni, mtu hawamjui lakini wamemshauri Baba yao amwambie Nabii Musa a.s achague yupi atakaye kumuoa, Na Mtume wa Mwenye Enzi Mungu akamchagua yule yule alopangiwa na kuvutika nae kwa mapenzi akawa mkewe, na wewe huyo ulonaye ndio ulopangiwa kwa hiyo kakae na wewe kipembeni ukayaombe mapenzi muda bado unao pata (Experience)usitoke mbio huko uendako kuna mateso na siko ulikopangiwa. Sasa na wewe Dua yako ikipokelewa nini kitatokea.
Endelea Part 3
No comments:
Post a Comment