Asalaam Aleiykum,
Mtizame yule ambaye anaishi kwa kutumia Akili, Vitizame visa vyake, kitu cha kwanza (Sex)Matamanio yakimalizika, sasa wewe ushachoka, wacha hizo nguvu zilobaki kidogo tuzigeuze kuelekea kwenye mapenzi, laa bali utamkuta anahangaika kwenye maduka ya madawa kutafuta dawa za kumtia nguvu za matamanio, anagombana na (Nature)makadirio ya Mollah wake, kwa sababu kanasa kwenye akili anakumbuka zamani kwa hiyo ana nasa kutamani (ndogo ndogo)ukimuona mtu kama huyo elewa hekima haijawasili hapo au kuzaliwa kwenye kichwa hicho.
Asiyekua na Hekima utamuona anapinga kila mabadiliko, mchunguze kiongozi wako utagundua hayo, popote pale ikiwa msikitini au kwengineko utaona wimbi hili la Akili linavopoteza watu, Utawaona wamebaki kwenye Historia na mambo ya zamani, siwenye kutaka maendeleo wa mabadiliko yoyote yatokee, wanangangania madaraka lazima waongozee sababu hekima hakuna, Na wanahofu kama hawaongozi watafanya nini, na hofu yote hiyo wanaona (Sex)inapotea (Wisdom)wakati wake ushapita, marafiki wanatoweka hawapo tena, maisha ya upweke yanatisha mtu peke yako, wana hofu watafanya nini na ukweli ushawadia, ndio maana wanakua ni wenye kupinga kila jambo, wagumu kukubali chochote kile, Na (Sex)ikipotea watageuka kuanza kulimbikiza mali, na akitokea kijana ana mawazo mepya atapingwa na kuzuliwa kila aina ya Fitna, na sababu kubwa hawana hekima, hawana mawazo, wamefilisika na wamefikia kikomo cha fikra, na sasa wameshindwa kuchupia Meli ya Hekima, utaona mazungumzo yote zamani tuliamua hivi,historia ilisema hivi, zama zilopita tulipanga hivi, hawataki kabisa kusikia, wenye hekima wanasemaje, sasa tufanye vipi, na siku zijazo tufanyeje.
Watizame waso hekima walivotawaliwa na hasira, chuki, mashaka ya maisha, na mwisho kabisa uchu wa nguvu za kutawala chochote kile iwe paka au mwanaadamu, sasa ikiwa unataka kujijua labda hekima imekuingia au kukushukia au imo mbioni kuchipua au unataka nikusukume kwenye bonde la hekima itabidi ujifanyie mtihani wa Hekima wewe mwenyewe, ili upate kujijua kama unayo mbegu ya hekima na uzidishe subira basi muombe mtu akuulize swali (Random),liwe la Dini au Siasa au la Kisomi, halafu tizama vipi utalijibu, ukitaka kutafuta (Refrence)au Hadidu Rejea basi jijue wewe bado, wewe ni (Copy)bado ni (Chori chori)lazima uibe pahala, hotuba lazima uandikiwe, basi jua bado Hekima haijafika, huna kitu, sio (Original)hakuna kitu kinachotokea katika (Being)yako, Lakini Mwenye Hekima(Wisdom) anajibu (Direct)hataki (Copy) hendi kwenye (History)hatumii Akili ila anatumia (Consciousness)yake. Na hiyo ndio Hekima, na huo ndio Uzee wenye manufaa,Na ukimuona mtu kama huyo mfanye Rafiki yako na wewe ufaidike kwa sababu ana kitu si kutoka kwenye Ulimwengu huu. Namuomba Mollah atujaalie Hekima itokanayo kwake. Amin.
No comments:
Post a Comment