Asalaam Aleiykum,
Napokea wingi wa malalamiko hususan kutoka kwa ndugu zangu Wanawake, wakinieleza masikitiko yao kuhusiana na kadhia hii ya mapenzi, Wanalalamika ndani ya majumba yao penzi limehama na halipo tena, au bado limebakia upande mmoja, walalamikiwa hapo ni Wanaume, wanataka ushauri nini kifanyike ili wapate na wao mapenzi kutoka kwa Waume zao, au kuna kosa gani wanatenda ili hata imewakuta hali kama hii. Nakuomba uzame katika Darsa hii ili ukitoka upate Lulu ya Mapenzi, ujue vipi utaitumia.
Wengi katika sisi tunajua neno mapenzi, lakini hatujui nini kitendo mapenzi, na kinapokuvaa unakua katika hali gani?, kwa lugha ya uchambuzi tunapata hisia za mapenzi, wote hiyo ni haki yetu, lakini hatujui hii hali ya Mapenzi inakuaje, na wengi inawatokezea wakati wa (Teen Age) tena kwa muda mfupi, baada ya hapo unaikandamiza hali hiyo unakua si mwenye kujua tena nini Mapenzi, na ina uzuri gani kuishi ndani ya hali hiyo, kinachobakia unaishi katika hali ya ujambazi wa mapenzi na huko ndio kubakiwa na neno tupu lisilokua na maana.
Lakini vizuri sababu usilolijua halikusumbui, leo hapa nataka nikuoneshe japo kidogo kiji njia ukiweza kupita hutorudi tena nyuma utayasaka mapenzi popote yalipo, na ujue hayapo popote ila yanateremshwa kutoka kwa Mollah wako, kinachotakiwa kwako ni subira. Kabla ya kwenda huko wacha tuwafahamishe pande zote mbili kinachowasibu ili yapate kuwapungua mateso, wapate kupandisha mbegu ya (Mahaba).
Kwanza Nawafahamisha hili, (Kupitia Mapenzi, Machungu hugeuka Furaha)
NINI Mapenzi?
Mapenzi ni kitu kilichojificha ambacho hakielezeki kama vile usivoweza kuileza nini Afya, Hali hii inatokea huko Mbinguni kama ilivo haidiwa kuwa inateremshwa pamoja na Rehma. Kwa ufahamu wetu sisi Mapenzi ni Hisia(Feeling) nzuri za furaha(Blissful) zenye kukusahaulisha kama wewe upo ila penzi ndio lenye kuishi, ukiijua hali hiyo wewe ushayajua mapenzi, au ukimpata mwenye kujua akakufahamisha basi huyo atakupeleka kwenye (Level) nyengine kirahisi kabisa kama utamsikiliza.
Mapenzi haya yana ngazi 99 mie leo nazitaja 3 lazima uzipite kufikia hali hiyo ya (Blissful)Furaha, hali ambayo utakua nayo huko Peponi, lakini hapa Ulimwenguni lazima uzipite uzitumie hizo ngazi tatu kufikia huko kwenye (Totality of Love).
Kwenye Mapenzi Mfalme anageuka kuwa Mtumwa,
Unapata kuzijua ngazi hizi tatu ili Umjue nani (Gigolo) na yupi (Lover Boy) na nini (Love).
Ngazi ya mwanzo kabisa na ndio ya chini iliopo baina ya magoti na kitovu ni (Sex) kwenye ngazi hii sana utawakuta wanaishi wanaume, na ikiwa mtu atajisahau hapa hapa, anakua hana tafauti na mnyama ambaye sote tuna (Share) naye hali hii ya utamanifu, na hapo inabidi ifanyike kazi kubwa ya kumsukuma (Dume) hili kwa kufahamishwa Bwana wee kuna (Lift) hebu panda uende ngazi ya pili uka (Enjoy) Ghorofa ya Pili ambayo ni nzuri zaidi kushinda hii ya kwanza unayopoteza nguvu(Energy) zako na kuzitumia bila ya
Hekima.
Kwanini nikasema hivyo kwa sababu ukimwachia Mtu wako katika (Energy) hii ya (Sex)ya machafuko hana matumaini ya kupasi mtihani, na hapo wengi wamefeli, hapo pana matatizo makubwa sana yanayotokea, na uharibifu mkubwa unapatikana hapo, na ndoa zote zinaanza kubomoka hapo kwa ajili ya (Kumcheza Kipole) unatokea uharibifu ambao hauwezi kufanyiwa ukarabati wa aina yoyote, yanazaliwa hapo magonvi yote ya kwenye ndoa, hapo ndipo linapouwawa penzi la kwenye Nyumba, hapo ndio yana sababishwa maradhi ya mfanyaji na anayefanyiwa, ndio maana mkaambiwa ama kwenye jambo hili msikurubie kabisa nyinyi hamna nguvu ya kutoka kwenye (Magnet) hii kama inavotajwa katika sura ya Israa aya ya 32"وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلزِّنَىٰٓۖ إِنَّهُ ۥ كَانَ فَـٰحِشَةً۬ وَسَآءَ سَبِيلاً۬ "
"Wala msikaribie Zinaa, hakika hilo ni jambo chafu na njia Mbaya"
Yenye kufungua chungu ya njia za mabaya, ukigusa una nasa, na ukinasa umekwisha, na ukisha unakua si mwenye kushugulika tena na Nyumba yako, penzi halikai tena moyoni mwako, yanabakia matamanio pekee yanokupeleka kwa yule asiye kuwa wako, na hata kama utashughulika kwa yule aliye wako, inakua kwa kitendo maalumu cha mahitajio yako, na huyo mwenzio ana hisi kuwa kwake yeye ni unata kitu kimoja wala si mwenye kushughulika na (Feeling) zake, na ukikwama katika ngazi hii vigumu kunasuka, unakua kama yule mwenye kutumia madawa ya kulevya, na hapo ndio unaanza Mushkel mkubwa, kutokana na maafa yaliyomo kwenye akili yako, mpaka uso unaondoka furaha, kwenye mawazo yako kuna kitu kimoja na wala hakiingi chengine abadan, unakua tafran, huna mapenzi mpaka kwa wanao, wala ya kitu chochote, umeambiwa hakika hilo jambo chafu na njia mbaya, maisha yanaanza kuharibika na unaselelea kwenye penzi la kitu kimoja tu nalo ni hio (Sex) Unakua huthamini utu wala huoni haya unageuka kuwa mnyama unayeishi na wanaadamu, na wala huna matumaini ya kupanda kwenda kwenye hiyo ngazi ya Pili ambayo sana wanaishi Wanawake na furaha za maisha ikiwa wanapata ukamilifu wa Mapenzi. huko ngazi ya pili kwenye haya Mapenzi kunatokea nini na kuna ladha ya aina gani kama utayapata mapenzi, na ufanye nini ili uyapate hayo mapenzi, na unajuaje kama sasa unaishi ndani ya mapenzi, kutaka kulijua hilo Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment