Asalaam Aleiykum,
Kwanza wacha nifafanue nikisema unatakiwa uwe shahidi namaanisha nini kama utanifahamu, mwanzo kabisa nilitaja kitendo cha kuona, kuona kwenyewe kunakua hivi.
Ulipokua mdogo unayaona maisha lakini huyajui uzuri wake, Ulipofikia Ujana uliyajua lakini huyafahamu, na sasa Uko Uzeeni unayafahamu maisha uzuri wake lakini huyajui tena, maneno yasikuchanganye kwani kujua kunatokana na (Mind) Akili, na kufahamu kunatokana na Roho(Soul) Ulipokua kijana unajua kukoga wala huogopi kokote unachupa, lakini sasa hivi Mzee unafahamu loo nikichupa msuli ukibana nimekufa, huko ndiko kufahamu, au nitoe mfano mwengine kwa wale walocheza mpira au dance watafahamu vipi unapocheza kandanda (Mind) Akili inavo (Stop)hukumbuki mke wala jamaa unabakia wewe na mpira, unakua (Totally)pale umewasili, au mcheza ngoma huwezi huku unacheza ukawa unafikiri nitakula nini (style) zitakupotea, kwa hiyo kuna vitu vinakufanya usahau hiyo (Akili) na ukiisahau wakati ule ndio unakua Shahidi(Then you are)ukiweza kuhisi hivyo ndio utaona uzuri wa maisha.
وَٱلضُّحَىٰ
"Naapa kwa Mchana"
Aya imeanza moja kwa moja kwa Mchana,(Light)Mchana ni wenye kumurika, mchana ni wenye kuleta furaha, Mchana unakupa mwanga.
وَٱلَّيۡلِ إِذَا سَجَىٰ
"Na kwa usiku unapotanda(Kutulia)"
Hapo vimetajwa vitu viwili unavo vishuhudia, wewe unapita katika viwili hivi kimoja unakua mcheshi unaruka ruka chengine unakua mkimya tayari kwa kulala, usiku unakuvunja kasi(Dark night) ndio maana huku Ulaya unaona watu na Tafrani sana za maisha wakati wa (Winter)kutokana na (Dark night) hapo vimetajwa viwili vyote ili upate kujua haya maisha na kujaa na kukupwa, kuna furaha na machungu, kuna kuzaliwa na kufa, kuna mabaya na mzuri, kuna utajiri na umasikini, kuna kupata na kukosa kuna maradhi na afya wewe pita katika hayo yote ukiwa Shahidi ndio utaona uzuri wa maisha haya.
مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ
"Hakukuacha Mollah wako wala hakukasirika"
Na maneno haya kila mmoja yanamuhusu wengine wanalaumu dini, wanaacha kuabudu, anapita mtu kusema nasali siku zote mbona sipati, vipi Mollah wako akutupe na yeye ndiye aliyekupa nafasi hii ya uhai, na hiyo riziki unayoitafuta kwa nguvu zako zote, vipi akukasirikie na wewe kiumbe chake dhaifu, anakupa ukimuasi na hata ukimkimbia usimuabudu yeye anakusubiri anajua utarudi kwake, vipi akukasirikie, kutokana na pupa zako wewe ndie mwenye kukasirika, jiangalie uzuri usimtafute mchawi ni wewe mwenyewe.
وَلَلۡأَخِرَةُ خَيۡرٌ۬ لَّكَ مِنَ ٱلۡأُولَىٰ
"Na wakati ujao (Utakua) Bora kwako kuliko ulotangulia"
Kila mmoja wetu mwenye kufikia dhamana ya Akili yake anafahamu hili, vipi alivopita kwenye misukosuko ya maisha mpaka kufikia hii leo, Tumepita sisi katika hali ngumu za maisha, matatizo ya kila aina, lakini kila siku zikenda unapata nafuu na utulivu wa maisha haya na kuzingatia (Uzuri wake) Kama umefahamu uzuri basi huna haja ya kuanza kufikiri zamani ilikua raha, tulikua hivi na vile, tukistarehe, maisha yalikua mazuri, hiyo utakua unafikiri (Collective) kwa ujumla, kwanini sasa hivi yasiwe mazuri, sababu kubwa unaishi sasa lakini (Mind) Akili yako ipo kwenye zamani na hayo ni matatizo, Ishi maisha ya sasa Utayaona Uzuri wake, dunia haijabadilika wewe ndio umebadilika, Ndege ndio wale wale, kunguru bado wapo, Bahari iko vilevile, mawingu ni yaleyale, hebu ishi usijitie dhiki, tizama uzuri wa maisha, kumbuka wakati ndio ulopita, sasa hivi sio wakati wako, Vijana ndio wakati wao, waache wao wafurahi na wewe furahi, nenda katika maisha haya ukiwa umeridhika, shukuru na wewe umepewa nafasi mpaka leo unaishi na unashuhudia maisha haya, videge vinaruka, mawingu yamependeza, mvua imenyesha, leo umekula vizuri, umeamka unaumwa kidogo yote hayo ni sehemu ya maisha, lazima uridhike na upite ukiwa (Present) Shahidi, sio upite (Automatic)ukiulizwa jana umekula nini hujui, vipi utaona Uzuri wa maisha, Shukuru umepangiwa usipate zaidi, cheka moyoni kuwa umeigundua (Qadar) ya Mwenye enzi Mungu na huna pingamizi nayo. Tizama Ulimwengu wako ulivyo, panua uangalizi wako wa Shuhuda uwe unaona mambo kwa kutumia moyo wako sio macho, na kama unatumia macho pekee ndio utaona huishi kununa, unaishi kwenye hasira, lakini ukitumia kuona kwa kupitia moyo basi wewe unakua shahidi wa kweli, ukipewa mkono na mtu unahisi mpaka umoto wake, mtu akikupa kitu ona kakupa kwa mapenzi, na wewe ukitoa kitu usisubiri shukurani ona umetoa kwa mapenzi, ukifanya hivyo kidogo kidogo utaanza kuona Uzuri wa maisha.
Endelea part 4
No comments:
Post a Comment