Asalaam Aleiykum,
Tahadhari na kinachotokea hapo, usije ukaomba dua ikawa hujijui penzi likadondoka kutoka kichwani na kwenda magotini utaingia hasarani, hutopata msaada, usicheze na nguvu ya (Sex).
Ama kwa upande wa Wanawake wao moja kwa moja linaporomoka moyoni na ndio maana utaona kajaa mapenzi, mwenye huruma, rahisi kusamehe, shujaa wa kupokea mazuri na machungu, mstahamilivu na mwenye kuonesha mapenzi yake kupitia hisia (Feeling).
Anaonesha mambo yake kwa njia za hisia akitaka kujulikana kakasirika ananuna inakua hakuna (Communion)wala(Communication).
Sasa vipi Wawili nyie mfanye mpate furaha ya mapenzi. La kwanza kabisa kufanyika inabidi umpe mkono mwenzio ili apande kwenye ngazi ya pili iliyopo moyoni, Na akifika muombe hebu tujaribu japo miezi mitatu kuwa tutafanya mambo yetu pamoja, Pia umfahamishe tafauti ya (Likes) na (Love)Mapenzi maana yake ni (Sharing)ndio ukaambiwa wapende maskini, wapende mayatima, na pia ukamuona mama anavo (Share)mapenzi yake kwa watoto wake wote, Kwa hiyo na wewe (Share) Na Mumeo au Mkeo, na mapenzi yanataka mbolea, na mbolea yenyewe ni hiyo (Action) ndio nikasema fanyeni mambo yenu pamoja, tokeni pamoja, nendeni kutembea pamoja, shirikianeni katika kila jambo linalohusu wawili nyinyi,Nendeni Baharini mkakoge pamoja, shikaneni mikono sasa mnaona haya za nini wakati nyinyi ni mke na mume, ukiona wenzio wanamtizama alo wako jitupe begani, unaogopa nini na wewe umevaa (Niqab)fanya uhakika kila uendapo awe pembezoni mwako, Wakiristo wao wanavaa pete, wewe mvae mumeo au mkeo, usisubiri ukiweza mfate mpaka kazini, sio kama mnavofanya hivi sasa utawakuta mtu na mkewe wanafatana mmoja yuko mbele mmoja yuko nyuma utadhani mke wa mkulima, mbona mnakimbiana kuna nini, ikisha mnauliza mbona hakuna mapenzi.
Mkirudi nyumbani kazi zenu ziwe za ushirika, ukimuona mwenzio anavua soksi kimbilia upate kuzivua wewe,Mfungue vifungo vya shati au zipu, Mbebeleze japo hajalia, Somaneni tabia kama anatabia inakukera(Mfano)anavuta sigara toka ukamnunulie kinyonyo, akisema hee mbona kinyonyo mwambie Sheikh Baja kasema (Kinakuachisha kuvuta sigara baada ya wiki tatu tu). Zitizameni kauli zenu,isiwe ukisema kitu hichi changu hichi chako, lazima mtumie kauli ya chetu, jueni kwamba ulimi kama mshale neno likisha kutoka halirudi nyuma, pia tambueni (Kwamba Ulimi umeumbwa na Mate kuteleza kazi yake)asiseme mtu kitu ndio ikawa sababu ya (Talaka), Fanyianeni (Surprise)Mnongoneze kwenye simu leo utakuta kitu kizuri, akija mpe ndizi mbivu alaa anataka nini tena, Fukiza nyumba yako, unajua maana ya kufukiza, ni kuondosha Tafrani na kuituliza akili, kufukiza ni dawa ya Akili, sio harufu nzuri pekee bali ni dawa ambayo kama utakua na desturi ya kufikiza kila siku utaona nyumba yako inavopata utulivu wa upendo. Ukimaliza toka wende ukanunue maua, unaijua siri ya Maua, Nini maua? Maua ni chembe ya mpenzi, ndio maana unaona Wapenzi wanapeana maua, Maua yana uwezo wa kutibu moyo ulojeruhiwa(Si unajua Nyuki anafonza Maua kutengeneza Asali) na unaelewa Asali ni Dawa, Na mimi nakwambia ipo dawa nyengine maua inayotoa nayo (Through Communion) Yamwage Maua ima chumbani au Ukumbini umualike mgeni mapenzi ili upate mafanikio yake. Mwenzio kakaa kwenye sofa usende kukaa sofa la pili kaa nae, umemkuta mwenzio anapika kivamie kitunguu ukikate wewe, ukimkuta anakogesha watoto, basi wewe nenda kapige deki, unaona haya nini wakati Nabii Musa a.s kateka maji. Kwenye (Love)Mapenzi Akili (Mind)inatoweka na ikisha kutoweka hujali tena kama unaibiwa, au unajenga Ghorofa, wewe mfalme au unacheo cha Ubalozi, au umevaa Majuba ya Sheikh, hiyo ndio hali inayokukuta ukiteremkiwa na mapenzi. Ama yule alokua hana mapenzi yeye kutwa anapanga akuuibie vipi, atakudanganya namna gani, ukijiona umo katika hali hiyo jijue huna mapenzi ila wewe ni (Cheater)unamdanganya mwenzio na kujidanganya mwenyewe, na hakuna maradhi makubwa kama kujidanganya mwenyewe.Ikiwa kweli hamu yako na nia yako ni mapenzi na unayata kwa dhati,
Ukionekana msimamo wako huo Basi Mwenye enzi Mungu atakuteremshia hicho kiitwacho mapenzi, na yakisha kushuka hayo mapenzi ndio unapata hiyo (Eternal Happiness)Furaha ya mapenzi na ukiyapata hayo, wewe unayayuka kabisa (In love you Disappear only Beloved remain) unakua hupo kabisa, anobakia ni mpenzi, unafanya kila kitu kwa ajili yake, inakua raha moyoni mwako ukimuona mpenzi wako kafurahi, na hata huko kuona kunaondoka yeye anageuka kuwa wewe, na kama yeye pia anarejesha hayo mapenzi kama unavohisi wewe, hapo nyote wawili mnakua wabarikiwa nyote mnayayuka(Disappeared)na (Only love Remain)hapo yoyote atokuja nyumbani kwenu, atakae kuwa karibu na nyinyi anapata (viberation)ya mapenzi yenu, na hapo inapatikana salama mpaka ya vizazi vyenu kutokana na mapenzi mnayopendana na daima mnakua furahani, na penzi likishamiri mpaka siku zinapotea, hamuulizi hata wakati, (No time no limit)na mnapata ufunguzi wa muono wa mambo kwa njia nyengine kabisa, sasa mnajua kuwa kila kitu katika Ulimwengu huu ni mapenzi, tafauti yenu na wasopendana ni ile wao wanajua kupenda chakula, kupenda mtu, kupenda maji, nk, lakini nyinyi mnakua mnajua kwamba vitu vyote hivyo vinaishi ndani ya mapenzi kama mlivo nyinyi, na chengine kabisa mnachogundua kuwa mnayo (Raw Material)yaani hiyo (Sex Energy) Sasa mnafahamu kuwa tukipumzika tukapeana nafasi basi inakua siku tunayokutana ni kama siku ya sikukuu, na katika kipindi hichi cha mapumziko mapenzi yetu yanazidi sana, Sasa kuna siri gani ya mahusiano haya ya (Raw Material) na mapenzi? Endelea Part 4
No comments:
Post a Comment