Asalaam Aleiykum,
Imeteremka Quraan na mambo makubwa manne ambayo yametajwa katika sura ya Yunus aya ya 57, lakini huwezi kuyapata mambo hayo au kuyajua kwa ufasaha mpaka upite katika Sura ya Aaraf aya ya 204 inayosema.
"وَإِذَا قُرِئَ ٱلۡقُرۡءَانُ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُ ۥ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ"
"Inaposomwa Quraan isikilizeni, Ikisha tulieni ili mpate kurehemewa"
Jambo la kwanza linalotakiwa kutoka kwako Usikilize, Na kusikiliza kwenyewe sio unasikia kila kitu, huyu kazungumza, mawazo haya na yale, hujamaliza kufunga hesabu, fulani kasema nini, hivo utakua sio kusikiliza bali inakua kusikia, Na kusikia kutwa nzima unasikia kila kitu, Gari imepita unasikia, Ndege wanaimba unasikia, watu wanazungumza unasikia, lakini kusikia huko hakuna faida yoyote inayopatikana, Na hata kukumbuka kutwa umesikia nini hutambui sababu hakuna maana kusikia huku.
Lakini katika kusikiliza unaingia katika shughuli ilokamilika na kupatikana (Totality) yako kwa ukamilifu au kwa lugha nyengine (Attention).Katika kusikiliza Quraan kuna kitu kinatokea na leo tunataka kukizungumza hicho ambacho kitakua madhumuni ya Darsa yetu pamoja na hayo mambo manne, Ili tupate kujua nini kinatokezea?, kwanini kinatoke, Na inakuwaje mpaka kikatokea, na inapatikana nini katika matokeo hayo.
Umo katika kupata Maalumati haya yazingatie kwa makini sana na uwe mtulivu ili upate kupata mafanikio na faida hii ya Quraan, Aya tulioitaja hapo juu mbali ya kusema Sikiliza pia imesisitiza kutulia, basi ikiwa umepata kuyaona maji mtungini au kisimani yalivotulia na hivo ndio unatakiwa na wewe utulie inaposomwa Quraan, Utulize Akili yako(Usiutingishe mtungi)utulie Mwili wako(Usikisumbue kisima)iwe hakuna (Movement)yoyote, shuwari kabisa, pasiwepo kishawishi chochote, anasoma uzuri,katia shada, mbona hakuvuta pale, au nikimaliza hapa nataka niwahi dukani, au mara umemsalimia huyu na mara useme na yule, hapo utakua ushatingisha mtungi na hupati faida yoyote na unakosa kikubwa zaidi nako ni huko Kurehemewa.
Nini Kurehemewa?
Kurehemewa kuko kwa aina nyingi sana, kuvuta pumzi kurehemewa, kusamehewa pia Rehma, kusikia nayo ni Rehma, kuona Rehma, mpaka kunyanyua kwako mguu na hiyo pia Rehma, Na mpaka haya ninayosema mimi na kuyaandika pia hii ni Rehma, wewe unayesoma pia umepata Rehma, hiyo ni kuonesha Rehma ziko nyingi na wanazipata viumbe vyote, lakini hili la Quraan kulipata lazima utimize shuruti yake nayo hiyo,(Usikilize na uwe Umetulia)huna mawazo yoyote kichwani, huna tafsiri yoyote, na hapo ndio utaweza kuipata hiyo Rehma.
Haiwezekani kuipata Rehma kwa njia tuifanyavo hivi sasa, kama vile imegeuzwa kitabu cha kufanyia mashindano, (najua mashabiki watakuja na nguvu za hoja chungu nzima)kutetea wanavo fanya lakini siwezi kukaa kimya, lazima niseme sio kusudio lake, haikuletwa Quraan hii ili mtu apate kupata zawadi, imeletwa ili mtu apate Rehma, Kimegeuzwa kitabu hichi ndio njia ya (Past Time)nikiendesha gari ntaisikiliza, na wako watu hawasikilizi mpaka asome Sheikh Fulani, ndio anamkosha mpaka anapata usingizi, wengine wanasema siwezi kupika mpaka nitie Quraan, huku nasikiliza na huku napika, vipi unadhani Rehma itapatikana, ikisha unasema haikai hata aya moja siwezi kuhifadhi, vipi utajua maana yake na wewe huna utulivu, vipi utaipata nuru wakati hutaki kutoka kizani, sasa ukivipata viwili hivyo nini kinatokezea? Endelea part 2
No comments:
Post a Comment