Asalaam Aleiykum,
Umeshatulia kwa makini kusubiri nini kinatokezea, tukio gani la maajabu linakukuta mpaka ukaridhika na kusema ama kweli haya mambo sio bure, hivi ndivo inavokua, hivi ndivo inavotibu, namna kama hii ndio unapata Mawaidha, na kwa sababu hii ndio ina niongoza, na sasa nimeshagundua Rehma yenyewe basi kuanzia sasa sitoihama tena Quraan. "Yunus 57"
"يَـٰٓأَيُّہَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَتۡكُم مَّوۡعِظَةٌ۬ مِّن رَّبِّڪُمۡ وَشِفَآءٌ۬ لِّمَا فِى ٱلصُّدُورِ وَهُدً۬ى وَرَحۡمَةٌ۬ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ
"Enyi Wanaadamu yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mollah wenu, Na dawa katika yale yaliyomo kwenye vifua vyenu, Na muongozo na Rehma kwa walioamini"
Umepatikana uzuri wa kuonesha mpangilio wa ufanyaji wa kazi yake hii Quraan katika hiyo aya ya 57 ya Sura ya Yunus, Na kama tulivoona mwanzo imeanza na Wanaadamu wote na mwisho ikachagua (Select) kwa walio Amin pekee. Sasa mambo gani yalotajwa hapo ambayo leo yatupasa tuyaangalie kwa undani ili tupate maana halisi ya maneno haya tuweze kuyafanyia kazi.
Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mollah wenu, Nini Mawaidha? Mawaidha ni Nasaha, kujulishwa kwamba katika Ulimwengu huu unatakiwa ufanye jinsi kadhaa wa kadhaa ili upate kuishi kwa salama, Usiibe ujue ukiiba na wewe utaibiwa na kama hujaibiwa basi jua utateseka kwa njia nyengine kama sheria za mwizi zinavoamrisha, Na kukatwa mkono kuna dhahir na siri, unaweza usikatike mkono lakini ukakatiwa biashara, sasa kama mkono ulikua ukinyooka sasa haunyooki tena, Usidhulumu utadhulumiwa na kama hujadhulumiwa aloleta Nasaha hizi ataingilia kati kwa namna anoijua yeye ili na wewe Udhulumike hapa Ulimwenguni na huko Akhera uendako. Lazima Amri ya Hukumu ipite midamu keshaleta Nasaha na nyinyi hamkuzifata, Na ukipinga Sheria za Mollah wako na ukayadharau Mawaidha yake, ukapinga Nasaha zake, kama unavofanya kila siku, yanapita huku yakitokea kule hata sikio halishituki, imekua Quraan haifanyi chochote juu yako ndio akasema Mollah wako na kukupigia mfano huu wa aya ya ( 21) sura ya ( Al-Hashr)
"لَوۡ أَنزَلۡنَا هَـٰذَا ٱلۡقُرۡءَانَ عَلَىٰ جَبَلٍ۬ لَّرَأَيۡتَهُ ۥ خَـٰشِعً۬ا مُّتَصَدِّعً۬ا مِّنۡ خَشۡيَةِ ٱللَّهِۚ وَتِلۡكَ ٱلۡأَمۡثَـٰلُ نَضۡرِبُہَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ "
"Lau kama tungeiteremsha hii Quraan juu ya Mlima, Ungaliuona ukinyenyekea na kupasuka kwa sababu ya hofu ya Mwenye enzi Mungu, Na hii ni mifano tunawapigia wanaadamu ili (wapate)kufikiri"
Wapi leo hutaki hata kufikiri,inasomwa Quraan msahafu mzima ikimalizika unapiga makofi na hata (Mashaallah)inakushinda unasema (well done).
Sasa Vipi Inatibu?
Hilo ni ponyo(Dawa) kwa yalio vifuani mwenu, Matibabu yapo ya aina mbili yaani (Physical and Mind) na wataalamu wanatwambia 90% ya maradhi yetu yanatokana na Akili(Mind) na 10% ilobaki ndio hiyo (Physical) Quraan inatibu hayo yote mawili, vipi inatibu au huko kuponesha, itabidi urudi nyuma mwanzoni kabisa kwenye maudhui hii ili upate kujikumbusha pale ilipotajwa (kusikiliza na kutulia) Kusikiliza kunatokana na Sauti (Sound) kabla ya kuendelea nataka ujijue wewe mwenye umeumbwa kwa udongo utoao sauti (Al-Hijr 26)"وَلَقَدۡ خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ مِن صَلۡصَـٰلٍ۬ مِّنۡ حَمَإٍ۬ مَّسۡنُونٍ۬"
Na tulimuumba mwanaadamu kwa udongo mkavu unaotoa sauti, unatokana na matope meusi yalovunda.
Na hiyo sauti ndio mnatumia kufanya (Communication) na mambo mengine kama itavo onekana sehemu ya tatu.
Endelea Part 3
No comments:
Post a Comment