Sunday, September 29, 2013

UZURI WA MAISHA PART 1

Asalaam Aleiykum,

Tunaishi katika Ulimwengu huu tukiwa tumegubikwa na dhiki, mateso, na tabu za maisha, Na kila siku ijayo kwetu sisi inakua nzito na ilojaa vitimbi vya kero.
Kwanini inakua hivyo jawabu utalikuta unalo mwenyewe lakini hujawahi kujiuliza, unaogopa kujiuliza kwa sababu unaona katika kuishi kwenye hizo kero, maudhi na tafrani za maisha zilojaa Akilini ni bora, kwa sababu kila mmoja anaona bora mie kuliko mwenzangu, yeye dhiki zimemzidi, yeye anahangaika, kwa kuona hivyo mtu anaona bora nitafute dawa za kunipa nafuu na matatizo haya, na hakuna dawa  za kunilaza mimi na kunipa raha ila Mirungi na Bangi, Mihadarati na ulevi mwengine ili nipate kuzungumza sana nijizubaishe na dhiki hizi za maisha, Wacha mimi nikazubaishe wakati kwenye Taraab, au ngoma ya mduara, mimi haijambo ninacho cha kunizubaisha angalau kwa muda mfupi kuyapata mazuri hayo, na yakimalizika narudi tena kama kawaida kwenye matatizo yangu ya (Dipression)na mengineyo.
Sasa huko tayari kama atakuja mtu akakwambia kuna dawa ya kutibu hiyo(Dippression), kuondosha hayo matatizo, kuponesha hayo maradhi yanokufanya usione (Uzuri huu wa Maisha), Basi toa nafasi tuchane (Kizoro ulichojifunika)ili tupate kukujulisha nini Uzuri wa maisha, na vipi utafanya ili uweze kuyaona maisha haya unayoishi ni mazuri.
Kukupeleka katika ufahamu huo itabidi kwanza urejee nyuma na kuangalia ndani ya Akili yako au kwa lugha nyengine utazame (Fikira)zako, lakini nakutahadharisha hizo fikira zitakuzungusha(Merry go round) zitakutesa fikira hizo usijue nini la kufanya kama ulivyo hivi sasa, zitaendelea kukuadhibu usipate kuona uzuri wa maisha, Ndio maana mwanzo nikasisitiza kuangalia au kuona kwa sababu katika kuona ni tafauti na kufikiri, Na ukiwa tafauti na fikira unaanza kuyaona maisha kwa njia nyengine(Pureness of life)njia ya uzuri wake, na ukiyaona kwa njia hiyo na wewe unageuka kuwa(Blissful).
Basi kwanza itabidi uangalie kwanini huoni maisha haya uzuri wake, Sababu kubwa ifanyavo hivyo ni kuwa Akili yako imetawaliwa na mabaya mengi, Kivipi? Jitizame wewe kwanini hukumbuki harusi yako lakini unakumbuka maradhi yako, kwanini hukumbuki mema 99 ila unakumbuka ubaya mmoja, kwanini unakumbuka mateso na hukumbuki furaha, kwanini unakumbuka machungu na hukumbuki raha, na mengi mengineyo mnayoyajua. Sasa nini kinatokea hapa? Endelea Part 2

No comments:

Post a Comment