Asalaam Aleiykum,
Anayekusudia kwenda Mji Mtakatifu wa Mecca anakua na dhamiri ya kutenda Ibada ili kutimiza nguzo ya Kiislam ya kuitikia wito wa Mollah wake, Unapotaja nguzo umeshatia maana ya kua umeijenga kwa imara na kuweza kuhimili vishindo vyote, Ima viwe vya Kimbunga, au Mtetemeko wa Ardhi, au mvua na mafuriko, ikiwa kimoja katika hivyo chaweza kuiangusha nguzo yako basi elewa nguzo hiyo sio imara, Na wala usipate taabu kuijenga kwa nyumba ya Hajj itakua umeingia hasarani.
Sasa vipi Utajua kama nguzo yako Imara au imejengwa kwa matope matupu, Na hivyo vitu nilivovitaja hapo juu vya (Mafuriko na Mitetemeko ya Ardhi) ni hayo mambo yanayokutoa kwenye Ibadah au Ucha Mungu, na kuijua kama nguzo yako ni Imara inakubidi ufanye Hijja hiyo ya Moyoni, uende ukamuulize (Civil Engineer) jee Nguzo yako inaweza kuhimili Zege la Ibada, Na hutopata Muhandisi aliyebobea katika jambo hili la Ibadah kama ulivo Moyo wako, umefikiwa mpaka kutajwa na Mollah wako, Vipi?
"إِلَّا مَنۡ أَتَى ٱللَّهَ بِقَلۡبٍ۬ سَلِيمٍ۬"
Isipokua atakae kuja kwa Mwenye enzi Mungu na Moyo safi.
Moyo ulosalimika Amekwisha (Surrender) kawa na Alama nyeupe, nini nyeupe? Ukiichunguza Rangi nyeupe utakuta ni mkusanyiko wa Rangi zote ndio unaoifanya Rangi kuwa Nyeupe, Nyeupe ndio hiyo (Light) Nyeupe ndio hiyo (Nuru)Nyeupe ni hiyo (Peace)katika moyo wako, umeshafanya mambo yote sasa unasema mimi basi, mimi najisafisha na taka zote za moyo, na hakuna kujisafisha kuliko na ukamilifu kama huku kwenda Hajj, Lakini haupatikani ukamilifu huo mpaka kwanza uka Hajj kwenye Moyo wako.
Haipatikani Hijja kama Moyo utakua bado una machafu, hatukatai utakwenda Mecca lakini sio Makka, Utakwenda (Holiday)lakini sio (Holyday)lazima uzitafute tafauti zake uzijue, na tafauti yake ni kubwa sana baina ya maneno hayo na matendo yake, nini Tafauti yake? Unakwenda Makka, Maharusi yamekujaa moyoni lazima nikirudi nirushe Roho, unakwenda Makka ukirudi lazima Ujenge nyumba ya tatu, Unakwenda Makka lazima ukirudi ushinde Udiwani, Unakwenda Makka ukirudi watakutambua lazima uwapandishe Mahakamani, Unakwenda Makka unasema fulani lazima umpate, Unakwenda Makka unatoa Ahadi nikrudi nitakusaidieni lakini mniwekee zawadi yangu, unakwenda Makka ukirudi unahudhuria Sherehe za Taarab, Unakwenda Makka fulani hujamsamehe na wewe hujasamehewa, Unakwenda Makka huzungumzi na Fulani, Unakwenda Makka Familia yako inateseka na Njaa, Unakwenda Makka umechukua Mkopo, Unakwenda Makka umefurika Mali za wizi, vipi wewe unakwenda Makka, Sasa huko Makka Uende vipi? Endelea Part 2
No comments:
Post a Comment