Asalaam Aleiykum
Naam Inapochafuka Bahari(Hamkani si shuwari tena) mashaka matupu yanatokea, hapo tena lazima Nanga ziteremshwe, ndipo hutumika njia mbili kuziteremsha nanga hizo, (Kumbuka tunaendelea na Darsa yetu ya Maradhi ya Matamanio, Tunaishi katika tendo la kuchafuka kwa maji ya Uhai).
Njia Mbili zinazopita maji hayo kwa Mwanaadamu moja ya Mwanamme inaitwa(Mahaladha) na kwa Mwanamke inaitwa(Muhuladha)hizo ndio zinazo tumika kusafirisha maji ya uhai,(Na kupita kwake ndiko kunapo kupa starehe), Maji yenye kutengeneza Binaadamu Mwenzio kiungo baada ya kiungo, Lau angejua Mwanaadamu hazina aliyobeba na matumizi yake asingekua anafanya mchezo mchezo wa kuyamwaga maji hayo bila ya utaratibu wa sheria au kwa mpango maalumu.
Sasa nini kinatokea mpaka unatokea msukosuko huu wa (Maradhi ya Matamanio) Tatizo kubwa siku zote bila ya kujijua wanaadamu tunalihusisha tendo hili na Akili wakati tendo hili halihusiani na Akili kabisa, tendo la Akili(Mind) kupenda, tendo la kuingiliana ni (Body) ndio utaona hata mnyama anayo bahati hii ya (Production) lakini Mnyama anasubiri mpaka (Body) itapohitaji ndio anatenda, lakini wanaadamu kwa kuwa (Mind) Akili ishachukua madaraka inaamrisha wakati wote (Body) kutenda kitendo ambacho lazima kitaarishwe kupitia (Process) zake, Na hayo Mataarisho ili Mwanaadamu uanze hiyo (Repaired) unahitaji masaa 48, lakini wapi, wee unajiona bingwa, unataka kutwa mara tatu na hapo ndipo yanapo anza (Maradhi haya ya Matamanio).
Sunday, January 18, 2015
MARADHI YA MATAMANIO PART 5
Asalaam Aleiykum
Maradhi yanaanzia hapo kwa ajili ya kutumika maji haya pasi na kiasi cha makadirio ya Mwili, kisima kisha kauka wewe unaendelea kuchota, kumbuka maji haya yanapita katika hizo njia, na njia hizi zikipata mazoea ya (Raha) Mwanaadamu hana njia ya nusura, ni lazima ataangamia, atasahau dini na kila kitu kilicho mbele yake, kwa sababu hizo njia zishajenga mahusiano na Akili, inakua kama unga(Opium)na (Brain), nyote mnakua wateja lakini wa fani mbili tafauti, huyu ana raha ya kulala usingizi akajidhuru Afya yake, na wewe una Raha ya Matamanio na kudhuru Afya yako, tafauti ni wakati, mmoja anachukua muda mfupi, na mwengine anachukua muda mrefu kujidhuru.
Kutokana na njia hizo kutoa Raha muda mfupi kwa Mwanamme na muda mrefu kidogo wa sekunde kwa Mwanamke, inakua mazoea sasa lazima zipatikane Raha hizo kwa njia yoyote, kwa hiyo hapo ndio Akili inatangaza Mamlaka kamili, saa zote unatawaliwa na mawazo ya uchafu Akilini, kwa hiyo unakua huwezi kufatilia chochote inakua Filamu zako za mapenzi, ukipumzika hili mara unatia Nyimbo, nyimbo ikisha unaimba mwenyewe, ukimaliza hizo nyimbo unatoka kwenda nje kutizama, hutulii huna (Balance) ya Akili mambo yamechafuka, huwezi hata kukaa peke yako, mara umekamata gazeti, Quraan inakutisha huitaki, basi inakua Akili yako fujo tupu, inapumzika ukihesabu pesa tu, lakini vyenginevyo unazunguka kama pembea, (Jitizame sana na kuyachafua maji hayo)Hapo ndio inatokea hiyo uloambiwa hakika hii ni njia mbaya.
Njia mbaya kivipi? Kila ukiyamwaga maji hayo ya Uhai bila ya mpangilio na (Body) Mwili wako unakufa kidogo kidogo, kwa sababu gani?, sababu yenyewe (Body) inabidi itengeneze tena hayo maji, na katika kutengeneza inabidi itumike mali ghafi, inabidi (Body) yako ijitoe Muhanga, ndio maana utaona ukimaliza hiyo shughuli unalala au kuwa Tafran lakini pale utakapotumia maji haya ya Uhai pasipo na uangalizi. na hiyo ndio njia mbaya uliyoambiwa usikurubie kila maji yakiendelea kutoka na wewe unamalizika kidogo kidogo, watu wanasema mbona kazeeka ghafla kumbe maji yashakwisha (Mwilini)kwa uzinifu. Huko ndiko kupatwa na Maradhi ya matamanio(Mind) ina Maradhi yake na (Body) ina Maradhi yake ya (Biology). Mbali yale ya kuambukiza na kuzaa vizazi ambavyo vitakua havina pakushika.
Sasa ufanye nini kama ndio ushapata Maradhi haya jee Dawa ipo?
Endelea part 6

MARADHI YA MATAMANIO PART 6
Asalaam Aleiykum
Naam Dawa zote mbili zipo, Ama ile ya (Mind) Akili inatakiwa uwezo wako wa kuweza kujiepusha na tabia za utazamaji na usikilizaji wako wa mambo machafu, Itabidi ubadilishe tabia yako kabisa kwa kukataa kwa nguvu zako zote kukurubia mambo machafu, ukifanikiwa kujizuia utaanza kuona kidogo kidogo unapona na Akili yako inatulia, na sababu kubwa hakuna tena (Information) za Uchafu zinazokwenda kwenye (Mind) yako.
Ama katika idara ya (Biology)kule utakapoona maji yashaanza kuchafuka au tuseme hamu imekushika, basi funga macho yako na tizama kwa ndani hamu hiyo iko wapi, ukifanya hivyo kwa utulivu wa dakika chache utaona hamu yote imekatika au kupotea, na hivyo ndivyo utavoweza kuyatunza maji ya Uhai na wala si vyenginevyo, kwani kutoka kwake ni sekunde chache na kutulia kwake vile vile ni dakika chache, wewe jaribu utalijua hilo, usifatishe kuwa nimeandika, ila fanya majaribio ndio utapata uhakika.
Sasa ikiwa utafanikiwa kutuliza (Mind) na hayo maji ya Uhai faida gani inapatikana? katika njia kuna matendo mawili kuna kwenda na kurudi, Kama ilivosema kwenye aya kuwa yanapita na kuteremka(Yakhruj)maji hayo katika njia zilotajwa, basi yakitulizwa yana njia nyengine maji haya baada ya kuteremka yanapanda, na hiyo ndio (Machenism) yake mwili wako yanapandishwa juu, sasa nini kinatokea maji haya yakipanda juu, yanafanya Ukarabati(Repaired) ya (Body) yako, na (Body) ikifanyiwa ukarabati utaona unaanza kupata utulivu(Peace of Mind)unapata (Tranquilty) unapata (Joy) ya maisha,unapata (Love)mapenzi kwenye moyo wako, na huruma zinazaliwa kwenye nafsi yako, na vyote hivyo vikikusanyika ndio (Mja unakua ushafanikiwa).(Ndio Maana mkaambiwa kwa mkato ili kujizuia na matamanio fungeni Saum).
Kwa hiyo ikiwa una nguvu zako kamilifu na una uwezo wa ku (control) maji hayo ya Uhai bila ya kutumia (Force) na kwa mafunzo ulopewa ya (Kufunga)Saum na mafahamisho haya nilokupa utagundua faida zake zisizo na mwisho. Lakini kama utaendelea kuyaachia Maji yako yamwagike ovyo ovyo bila ya kuangalia Afya yako, utakua mwenye hasara kubwa, utakua mwenye kujeruhiwa Akili yako vibaya sana, utakua huna mawazo mengine isipokua unatafuta njia za kuyatoa maji hayo, Na utakapoona una hali kama hiyo basi jijue una maradhi ya matamanio, kwa hiyo fanya haraka utibiwe ili usije ukadhurika.

Sunday, January 11, 2015
MARADHI YA MATAMANIO PART 1
Asalaam Aleiykum
Baada ya kupokea taarifa na takwimu hususia za Matendo machafu ya (Ngono)(Sex)yalivoenea na kuikumba jamii yetu ya leo nimeona kuna haja ya umuhimu wa kuzungumzia chanzo cha Maradhi haya yaloambukizwa na kuenezwa kwenye Mwambao wetu wa (East Africa) Na kwengineko.
Sio Kificho tena kuwa Jamii inaangamia, sasa pengine kuna uwezekano Mtu kakumbwa na Maradhi haya na hajui afanye dawa gani ili apate kupona. Basi Darsa yetu ya leo tutajaribu kukupa dawa asaa unaweza kupata nafuu au kupona kabisa, Kwanini nikasema nafuu, kwa sababu Maradhi haya ni ya siku nyingi, kwa hiyo ili upone kabisa unatakiwa utumie dawa hiyo angalau kwa miezi sita mfululizo, lakini ukitaka upone kidogo kidogo ndio nikatanguliza neno nafuu kwa kuwa huwezi kuitumia hiyo dawa mfululizo ni chungu sana, inataka ustahamilivu wa hali ya juu.
Sasa kabla ya kwenda kwenye hiyo dawa ambayo itatoka mwishoni wa darsa hii kwanza wacha twende kwenye chanzo na uchambuzi wa hili jambo la (Ngono)likoje, Sababu huwezi kutibu Maradhi bila ya kujua chanzo chake.
Sasa Jambo hili limeanzia wapi kwa Mwanaadamu? Jambo la Matamanio (Sex) lina sehemu tatu, leo ntazizungumza sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni ile ya (Mind) Akili (Al Imran 14 mpaka mwisho wa aya)زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ ٱلشَّهَوَٲتِ مِنَ ٱلنِّسَآءِ .
"Watu wamepewa huba ya kupenda Wanawake"
Hakuna kosa kiumbe unao udhaifu huo, ndio maana unaona wanawake wengi au wanaume lakini unamchagua mmoja mwenye (Macho ya duara na nyusi za kifungo) au Mwenye (Macho ya Ndege na Mashavu ya kopa)Unajua Mwenyewe ni kipi chenye kukuvutia, Na Mwanamke vile vile ana uchaguzi wake (Pengine anapenda (Baba la Miraba sita lenye nyusi za Mawimbi) au anapenda Mwembamba Mwenye pua ya Upanga.
Na Jambo la Pili ni (Physical) ni Hitimisho la tendo lenyewe(Sex) Ngono, ambalo ni (Biological). Na Jambo la tatu ni Mapenzi ambao ni moyo, Vikikutana vitatu hivi ndio linatokea tukio la (Mawadat wa Rahma) utaona kwa mpangilio wake vitatu hivi yaani (Mind)Akili ipo Juu,(Heart)Moyo upo kati na kiungo cha kutekeleza hilo tendo (Sex Organ) kipo chini kabisa.
Unapata Darsa kama hii usianze kuleta fikra zengine ila chukua chenye manufaa yenye kukuhusu ili upate kupona, usigeuze Darsa hii kuwa kama (Magazine).
Endelea Part 2

MARADHI YA MATAMANIO PART 2
Asalaam Aleiykum
Sasa nini kinatokezea ? huwezi kujua nini kinatokezea mpaka kwanza upelekwe(Lab)ukaoneshwe hicho kinachotokea, kamata kitabu chenye elimu zote ikiwemo hii ya (Biology)alokuja nayo "Mtume s.a.w"utizame inasema nini katia tukio hili(Quraan Tariq aya ya 5-7)
فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَـٰنُ مِمَّ خُلِقَ
"Na Ajitizame Mtu Ameumbwa kwa kitu Gani"
Mwanaadamu ana uwezo mpaka wakutizama kile alichoumbiwa, inatakiwa mtazamaji ana upeo gani wa kutizama, jee anajua kama hicho alichoumbiwa ni maji ya Uhai? anajua thamani ya Maji haya, kwanini yakawemo Mwilini mwake, yana kazi gani ndani ya huo Mwili licha ya kumuwezesha kiumbe mwengine kuumbwa?.
خُلِقَ مِن مَّآءٍ۬ دَافِقٍ۬
"Ameumbwa kwa Maji yatokayo kwa kuchupa"
Yanayopita katika njia mbili tafauti kutoka kwa Mwanamme na Mwanamke.
يَخۡرُجُ مِنۢ بَيۡنِ ٱلصُّلۡبِ وَٱلتَّرَآٮِٕبِ
"Yatokayo katikati ya mifupa ya Mgongo na Kifua"
Yanatoka kwa Mwanamke kwenye mifupa ya mgongo ndio maana yanachukua muda katika utokaji wake, Na hutoka kwa Mwanamme kwa wepesi kutokana na utokaji wake ni kifuani kwenye (Kitovu) ndio maana wawili hawa Starehe zao zikawa hazilingani, kwa Jambo hilo Mwanamke anaongoza kutokana na Uti wa Mgongo ni Mfalme wa (Body) ya Mwanaadamu.
Sasa kabla kwenda (Deep)nipeni ruhusa nirudi juu kwenye (Mind) ambako ndiko kwenye Maradhi yenyewe, Katika Ulimwengu wa leo kuna kila (Zana)nyenzo ya kuamsha Matamanio, kuanzia kwenye Nyimbo, Wanawake na Wanaume vivazi vyao, Kujipamba kila Mtu anamuamsha mwenzie alolala, Watu wanavo tizamana , halafu kubwa zaidi hi hizi (Filamu na Magazeti ya Uchi)mambo yote haya yanachangia kuamsha hisia usiku na mchana, ndio utakuta wakati wote watu mawazo yao yamo kwenye (Matamanio).
Mtu anafanya mambo bila ya kujijua anaamsha hisia za Matamanio kwa wenzake wengi wanafanya kwa makusudi na wachache wanafanya kwa bahati mbaya, Sasa nini kinachoamshwa?
Endelea part 3

MARADHI YA MATAMANIO PART 3
Asalaam Aleiykum
Kinacho Amshwa ni hayo Maji ya Uhai, iwe kwa Mwanamme au kwa Mwanamke, sasa nini habari yetu sisi wenye kucheza na maji haya ya Uhai?. Maji haya yakiguswa Mtungini yana shuruti mbili ima yatulizwe au mtu ayanywe yatoke, Hayana njia nyengine, ndipo pale utaona Maji haya yakichafuka ndani utaona Mtu nje anachanganyikiwa, Na hayo ndio Maradhi makubwa yaliyo ingia kwenye Akili zetu, kutokana na uchokozi wa maji hayo ndio wengi wamedhurika kwa (Video) za uchafu , kutokana na dhara hiyo wengine wanakamata watu kwa nguvu, kutokana na dhara hiyo wanaharibu watoto wadogo, hawa ni wagonjwa (Mental state zao) sio sawa wanatakiwa wapatiwe matibabu Akili hazijatulia kabisa.
Watu hawa wanatumia njia ya kuwa pamoja na jamii ili waonekane wako sawa, lakini tambueni kipimo cha Akili ni (very sensitive)unaweza kumkuta Mtu nje anacheka kumbe ndani analia, jamani nisaidieni lakini hasemi, kwa hiyo nini kifanyike Muandameni mkiomuona Mtu kakamatana na mwenendo huo mpaka akubali matibabu au aondoke katika Mitaa yenu, Kwani Mtu Mwenye Tabia hiyo anaharibu (Generation) nzima ya kizazi kijacho.
Naam hivyo ndio Majanga yanavotukuta ukicheza na Maji ya Uhai, ukipita ikawa wakati wote unaangalia mambo ya (Munkar) na huo ndio uchafu ulotajwa katika (Quraan) usiukaribie (Israa 32)
"وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلزِّنَىٰٓۖ إِنَّهُ ۥ كَانَ فَـٰحِشَةً۬ وَسَآءَ سَبِيلاً۬"
Wala msikaribie zina, hakika hiyo ni uchafu(Mkubwa)na ni njia mbaya.
Hakika huko kuchafuka kwa Akili ndio uchafu wenyewe, sio uchafu ambao unaweza kuusafisha kwa ufagio, ni uchafu uloingia kwenye Akili yako na kutawala sehemu zako mbili za (Male) na (Female),ndani mambo yamevurugika, unamtafuta mwanamke wa ndani kwenye Akili na unamtafuta wa nje kwenye Dunia, hata ukiwapata wanawake wote hutoridhika, kuridhika kwako mpaka umpate huyo wa ndani, hapo ndio unakua (Balance)lakini kama hajatulizana huyu ulomchafua ndani, hapo hakuna salama, vipi umeanza uchafuzi huu, angalia mambo yameanzia wapi.
Kila kitu unacho angalia kinapigwa picha na kupelekwa kwenye Akili kuhifadhiwa, sasa jitizame mambo mangapi machafu kwa siku tu unaona, Picha zote hizo zimo ndani na zinataka uchambuzi wako, unataka kusafisha Akili yako lakini haiwezekani uchafu mwingi, sio lazima uangalie alovaa sketi fupi, mpaka yule alovaa Buibui lilobana picha zake zimo na anaendelea kukushughulisha, unatizama nyama zinavyotingishika, Maskini alovaa kafunika mifupa tu kaachia nyama, na wewe mtazamaji umetoa (Camera) yako unachukua picha zako na hilo Buibui unakwenda kumvua baadae, unadhani nani ataokoka na mashaka hayo.
Na hivyo ndivyo machafu yafanyavyo kazi yake, kwa kuwa Maji hayo ni (Powerful) yanatawala mawazo yetu inakua kila unalofanya ni kwa ajili ya kutumikia machafu yaliyomo kwenye akili yako, Na kwa Mwanamke hali ni hiyo hiyo hakuna tafauti, Uchafu ulotiwa kwenye Mind lazima uchambuliwe (File)moja baada ya jengine, ikimalizika picha ya huyu inakuja ya mwengine, ndio maana utaona hata maji ya Uhai yakitulia unaendelea na uchambuzi kwa kuwa uchafu Akilini umekua mwingi, huna nafasi ya kuwaza jambo lengine, ukijiona una hali kama hiyo elewa hayo ni maradhi inabidi utafute dawa ya kujitibia, sababu sasa (Bacteria)wamezidi, kupona kwake sio rahisi, japo mbele za watu utajitahidi kukaza mguu, lakini kumbe ndani umeuregeza, ndio maana ukaambiwa usiukaribie uchafu huo kupona kwake sio rahisi.
Halafu sehemu ya pili ya hiyo aya ni njia mbaya , ni kitu gani hiyo njia mbaya?, Hapa itabidi nikutakeni ruhusa yenu ili nipate kukuchukua (Chumba cha Upasuaji) ili tujue inakuwaje hata ikaitwa njia Mbaya. Inaendelea part 4.

Sunday, January 4, 2015
DUNIANI KIPOFU NA AKHERA KIPOFU PART 1
Asalaam Aleiykum
Kuona kupo aina mbili, kuna kuona kwa Macho ambako kunashirikiana na (Body) ama tuseme Akili, Halafu njia ya pili kule kuona kwa Roho, kuona huku ni (Pure) ni kuona kwa kudumu na wala hakuna shaka ndani yake. Isipokua Mja Mwenyewe utake kufunga Macho yako ya Kiroho, lakini katika sifa ya kuona huko ni haki ya kila mmoja wetu.
Lakini Wanaadamu wengi wanachagua kuyafumba Macho ya Roho moja kwa moja mpaka siku ya kufa kwao ndio Mja anashtuka kumbe mimi naona, ukifika wakati huo inakua wapi ushachelewa huna wakukushika mkono tena, Na katika Ulimwengu huu ukiamua kuyafunga Macho yako ya Kiroho basi jijue ushaangamia, ushajipa upofu wa lazima kwenye Dunia hii, Na ukiyafunga Macho ya Roho pale pale Macho ya Akili yanachukua Mamlaka ya kukuongoza, na yoyote yule Mwenye kuongozwa na Akili anakua haoni kwa sababu Akili imejaa (Memory) ndio maana siku zote unajipiga na makuta, unapapasa viwambaza kwa kujigonga kutokana na mwenendo wako wakurudia mambo yale kwa yale sababu huna macho ya kuona, Siku zote unajikuta unafanya makosa unatubu na kurejea tena, Unadhulumu na kunyanganya ikisha unarejea tena, unalewa ukiamka unajuta unalewa tena, unakwenda kwa mganga hujafanikiwa unajuta unatubu unakwenda kwa mara nyengine, umezama kwenye biashara unahangaika halafu unaona haina maana lakini hujui la kufanya unaendelea tena kutafuta mali.
Hivyo ndio Macho yako yenye kutumia Akili yanavokutuma(Full of Memory) Na kama hujazinduka ukafungua tena Macho yako ya Roho ndio Quraan inakwambia(Al-Israa-72)
وَمَن كَانَ فِى هَـٰذِهِۦۤ أَعۡمَىٰ فَهُوَ فِى ٱلۡأَخِرَةِ أَعۡمَىٰ وَأَضَلُّ سَبِيلاً۬
"Na aliye Kipofu katika (Dunia)hii, Basi atakua Kipofu katika Akhera, Na (Huko atakua)aliye potea zaidi njia"
Watu wanaelekea peponi wewe huyo unaongoza njia kuelekea motoni kwenye mateso sababu huoni.
Sasa ufanye nini unatakiwa ujipime uelewe mimi Kipofu au naona ili wasiwasi uniondoke?, Inabidi tukuletee mifano, na mifano iko mingi kwa hiyo ukijiuliza swali hili la mimi kipofu au naona, basi ushajitilia wasiwasi, lazima unajijua unapapasa viwambaza kwa hiyo itabidi nikupe mkongojo(Fimbo) ili upate kujua Alaa kumbe mimi ni kipofu kweli, Na Mkongojo wenyewe ni huu wa kukuzindua kwamba wewe si Kipofu lakini umeamua kwa hiyari yako ku (Cheat) kudanganya kwa makusudi, umefunga macho Yallah Maskini kumbe unaona, Sasa macho haya umeanza kufunga lini? Endelea Part 2

DUNIANI KIPOFU NA AKHERA KIPOFU PART 2
Asalaam Aleiykum
Macho haya ya Roho yameanza kufungwa kuanzia miaka Saba, kabla ya hapo ulikua unaona vizuri kila kitu kwako maajabu na hivyo ndivyo inavoona Roho (Crystal Clear)ndio maana ukaona mtoto mchanga anatizama kitu kisha anacheka, Na kwa kuwa huu Ulimwengu ni (Vast) Mkubwa maajabu hayeshi, lakini kuanzia miaka saba kila mtu katupa (takataka zake kwenye macho yako ya Kiroho)yakafumbwa na Majirani, jamaa, School, Marafiki, University, College,Tv,Games, kila ukionacho katika Ulimwengu huu ambacho umepitia shughuli yake kubwa ni kukusahaulisha kwamba wewe unayo macho mengine ya Kiroho lakini huna haja ya kujua, umejaa (Memory) tupu, wewe jiangalie utalijua hilo, hujapata hata siku moja kufungua macho ya Roho ukaangalia jee Roho inaona nini? Quraan inapiga kelele usiku na mchana lakini wapi, unaweza kuhifadhi Msahafu mzima lakini upo kwenye Akili, unasalisha watu wanaona Raha lakini wewe na wao hakuna aliyeijua hata aya moja kwa njia ya Kiroho, ndio maana utaona yule ambaye hakusoma inakua rahisi sana kwake kutumia Macho ya Roho, kuliko wewe mwenye kujinata umesoma na una mahadith mia kadhaa umehifadhi, tafauti yenu wewe una (Memory) yeye macho yake ya wazi akitajwa Mtume s.a.w machozi yanamtoka wewe unashangaa huyu naye, anajifanya anampenda sana Mtume, sio hivyo yaweza kuwa wewe umemtaja Mtume yeye kaikumbuka hii Quraan aloachiwa na Mtume inasema nini? Na machozi yake yaweza kuwa analia kwanini hakuwepo kipindi cha Mtume s.a.w akayatumikia maneno haya kwa wakati ule, hilo ni jicho la yule mwenye kuona kwa Kutumia Roho, ita Imani au upendavyo lakini hakika huyo kama anavyo ona hapa na hukoAkhera ndivyo atakavyo ona bila ya kizuizi. Sasa Quraan inakuhimiza vipi ufungue macho?
Endelea Part 3

DUNIANI KIPOFU NA AKHERA KIPOFU PART 3
Asalaam Aleiykum
Quraan daima inakuhimiza ufungue macho yako ungali uhai, inakwita kwa mambo mengi tafauti, lakini baada ya kukufungua macho ya Kiroho wewe unazidi kulala kwa sauti nyororo, na hiyo sio kazi yake, kazi yake ni kukuamsha, lakini kwa kuwa pengine Akili imejaa (nyimbo) ikisomwa vizuri unatingisha kichwa kwa mfano wa nyimbo, Quraan kazi yake ni kufumbua macho yalofumbwa na Akili, uone kwa uwazi na upeo wa hali ya juu, nitatoa mifano miwili mitatu ili uanze mazoezi yakufumbua macho yako ya Kiroho na hiyo ndio(sipirituality) au (Faith) Iman utakvo taka kuita, anza taratibu kidogo kidogo utaanza kuona vyengine, utapata (Change)mabadiliko mpaka kwenye Sala zako iwapo utaanza kufungua Macho ya Roho.
Inasemaje Quraan, Quraan inakwita kwa kukwambia (Na atizame)Mwanaadamu chakula chake anacho kula, sasa kwanini uambiwe utizame kwani huoni, si unaona chakula, lakini kutizama huku ni kwa njia ya Roho, Na Roho na Akili vyote viwili vikiona kwa pamoja ndio Ucha Mungu unazaliwa.
Roho inaona vipi? Umeambiwa utizame chakula na kuelezwa nani mwenye kukifanya na mfumo wake unavofanywa, kawaida utaishia hapo lakini kuna kitu cha zaidi aya inasema (Sisi) ndio wenye kukifanya, sasa nani Mwenye kuona hiyo sisi, Baina ya Kutizama kuna chakula na wewe mtazamaji, lakini kuna huyu wa tatu Mwenye kujua huyu kajificha, huyu ndio wewe, huyo ndio hilo jicho la Roho ambalo Quraan linasisitiza ufungue, uone kutumia Roho sio Akili.(فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَـٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِ)
Lakini huwezi kukubali bado umezama kwenye (Taraab)bado (Bongo Fleva)imekushika unaipenda Dunia hii imekufunga macho hujijui kabisa umo katika kukusanya mali na sherehe hizi na zile,mpaka umekua kama Kipofu kweli, na Mwenye enzi Mungu anasema katika sura ya Yaasin aya ya 9.
وَجَعَلۡنَا مِنۢ بَيۡنِ أَيۡدِيہِمۡ سَدًّ۬ا وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ سَدًّ۬ا فَأَغۡشَيۡنَـٰهُمۡ فَهُمۡ لَا يُبۡصِرُونَ
Na Tumejaalia(Kuweka)kizuizi mbele yao na kizuizi nyuma yao na tumewafunika(Macho yao) kwa hiyo hawaoni.
Sasa fanya hima uondoshe kizuizi, anza kuangalia kwa Roho utajua vizuizi gani vinavyokufanya usimuabudu Mollah wako, na kwanini hata ukimuabudu hupati mapenzi yake, Fungua macho yako anza kupunguza kuangalia mambo kwa kutumia Akili, soma Quraan ikupe muongozo, inasema Quraan tukaujaalia Usingizi kama kufa, tukajaalia usiku kama guo, tukajaalia mchana ni wakati wa maisha, jee umepata kuviangalia hivyo vyote kwa kutumia Roho yako, ikiwa umefanya hivyo wewe ushapata (Faith) Imani, vitu hivyo vinakupa (Mwanga) uhakika wa mambo ambayo hayana shaka ndani yake, sasa hivi Imani yako ya kushikiwa bado hujapata Ithbati, Tizama kwa kutumia Roho yako utayaona mambo hayo.
Zipo Njia nyingi za kuijua Roho yako na ukaona mambo kwa kutumia Macho ya Roho nitakupa moja mengine tafuta mwenyewe, hayana idadi, mwanzo wala mwisho, japokua mwanzo utapata tabu na kutishika lakini usiogope jambo la mwisho litotokea ni kufa, sasa unaogopa nini? kwa siku wanakufa karibu watu laki nne sasa hujioni wewe una bahati umebakia ili uyatafute mapenzi ya Mollah wako. Nini cha kufanya kutaka kuyajua kweli macho haya ya Roho yapo, Leo ukenda kulala lepe lepe la usingizi linakuja ushafumba macho ndani una uwezo wa kubakia macho, subiri kuna kipindi cha sekunde chache baina ya kulala kwako kuna vitu vinabadilika unatoka kwenye dunia ya Fahamu unakwenda kwenye dunia ya Usingizi vyote hivyo utavishuhudia mambo yatakushangaza lakini na wewe utabadilika (Forever)utakua ushaondosha (Cover) utakua huoni tena kwa kutumia macho ya Akili, utakua ushagundua siri ya (Maisha)utakigundua kile chenye kuiona ndoto wakati umelala, nje utabakia kama kawaida lakini ndani atakua anaishi Mcha Mungu, na huko ndiko Quraan inapotuita tuone ukweli wa mambo tupate ushuhuda wa mambo, tuthibitishe Imani zetu, lakini kama umeamua kuwa Kipofu hiyo ni hiyari yako, na utakapofufuliwa usije ukalalama mbona sioni kitu, wenzako wanakwambia huoni Rehma za Mungu unajibu sizioni, kwa sababu ya kuwa kipofu hapa Duniani, Fata nyayo za Wacha Mungu upate kuongoka, acha kukamata mambo ya mpito yatakupofua macho hapa na huko Akhera, shikilia vile venye kudumu upate furaha ya Milele.

Subscribe to:
Posts (Atom)